Monday 22 July 2013

Mjengo mpya wa P Square uko kwenye hatua za mwisho

Kama ulishawahi kusoma baadhi ya mitandao ya Nigeria au ya Afrika Magharibi nadhani utakuwa usha kutana na habari zilizoelezea kuhusu utajiri wa wakali hao wa Nigeria (P-Square), "Peter Okoye na Paul Okoye". Mbali nakuwa na bihashara nyingi zinazowaingizia kipato mbali na kazi wanayofanya ya Muziki, pia walishajiingiza kwenye biashara ya mafuta mwanzoni kabisa mwa mwaka huu.
Ville Mansion-II(kwenye hatua za awali)
Pia mwezi March mwaka huu walipost picha za mjengo wao mpya walioupa jina la "SQUARE-VILLE-II" ambao ulikuwa kwenye hatua za awali...mjengo huo uliogharimu gharama kama za "SQUARE-VILLE-1" waliojenga huko Omole Estat.
Ville Mansion-II(Hatua za mwisho)
Wakali hao walioweza kununua kiwanja cha mjengo huo kwa pesa za kinigeria N200Million huko Parkview Estate, jana walipost picha ya mjengo huo ambao uko katika hatua za mwisho.
P-Square na Akon kwenye Ville - I

No comments: