Monday 22 July 2013

Diamond kufanya Collabo na Fuse ODG wa Azonto

Msanii wa bongo fleva, Nassib Abdul a.k.a Diamond Platnumz weekend hii ameonesha picha akiwa na Fuse ODG wa Antenna na Azonto, Nana Richard Abiona a.k.a Fuse ODG kutok nchini Ghana...kitendo hicho kiliwafanya wengi na wadau wa muziki kuhisi jamaa hawa wako mbioni kutoa ngoma.

Diamond ameweka picha hiyo kupitia mtandao wa Instagram akiwa na mkali huyo ,Fuse ODG na kuonyesha wawili hao wana lengo la kuchanganya Bongo flava na Radha ya muziki wa Ghana.

Diamond aliandika... “Let’s see what we can Get if we Mix #Bongoflavour from Tanzania and #Azonto from Ghana…. here wit maboy @fuseodg ..the ANTENA hit Maker..!”

Basi kama kutakuwa na collabo ya wakali hao, si jambo la kushtua sana kwakuwa kampuni inayommanage Fuse ODG ilionesha interest ya kumchukua Diamond na huenda mambo ya mikataba yameshakamilika.

Diamond amekuwa msanii mwenye mafanikio makubwa kutokana na kupata deal nyingi za show na matangazo. Mnamo tarehe 17 mwezi huu website moja maarufu ya Kenya “Ghafla” iliandika habari “Why Diamond is East Africa’s Biggest Crowd-Puller” na kudai kuwa umaarufu wake umeuzidi wa Jose Chameleone.

CHANZO: Mwanahabariuswazi_Blog

No comments: