POLITICS

CCM YAIBUKA KIDEDEA

BAGAMOYO BADO YA CCM
  • KIBINDU: Matokeo ya jumla:

CCM- kura 1682(75%),CHADEMA-kura 548(25%).
  • MAGOMENI: Matokeo kwa jumla:

CCM 1183, CUF 708, CHADEMA 347.




 Kagame, Museveni na Kenyata wakutana juu 

ya kuimarisha miundombinu na biashara

Mkutano uliowaleta pamoja Rais Paul Kagame wa Rwanda, Yoweri Museveni wa Uganda na Uhuru Kenyata wa Kenya uliohusu kuamua juu ya kuimarisha miundombinu ya Afrika Mashariki na biashara, na masuala mengine.Mkutano huo uliofanyika mjini Entebbe, Uganda umekuja wakati wafanyabiashara wakilalamika juu ya kuongezeka kwa Ushuru ambao wanasema uingilia kati na biashara zao. Maraisi wote walikubaliana juu ya kuondoa vikwazo vya ushuru ili kuleta ushirikiano wa kiuchumi na kuleta mavuno na ukuaji endelevu wa uchumi. Juu ya suala la hilo hasa, Wakuu wa Nchi walikubaliana kwamba kuondolewa kwa kodi ambayo kodi itatakiwa kulipwa katika hatua ya kuingia kama Mombasa au miji mingine.Hii inatarajiwa kupunguza harakati za siku kutoka siku 18-5 kutoka Mombasa hadi Malaba nchini Uganda. Mkutanoni pia walikubaliana kufufua Reli ya Afrika Mashariki line ambayo inatumika Rwanda kwa urahisi juu ya usafirishaji wa bidhaa na watu katika kanda kwa gharama ya chini.Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari baada ya mkutano wa kufungwa, kati ya marais hao watatu na technocrats kutoka nchi hizo tatu ambapo Rais Museveni ndiye alikuwa mwenyekiti wa mkutano, walisema kuwa wamekubaliana kujenga mabomba mawili ambayo yataweza kusafirisha bidhaa za mafuta.Moja kutoka Mombasa hadi Eldoret utatumika Kampala na Kigali bomba itakuwa kimeundwa kuwa na utaratibu wa nyuma na line nyingine bomba kwa ajili ya uokoaji ya mafuta ghafi. Bomba ghafi kuleta pamoja Uganda, Sudan Kusini na Keya.Rais Museveni alisema kwamba viongozi waliamua kwamba kusafishia mafuta kuwa yalijengwa katika Uganda kuboresha mafuta kunyonywa kutoka nchi za EAC.Mkutano pia walikubaliana juu ya kutafuta njia ya kuzalisha umeme zaidi na kazi juu ya matumizi ya nishati mbadala kwa ajili ya uendelevu.EAC moja ya kitambulisho, moja ya utalii na kufuatilia kwa haraka shirikisho EAC yalikuwa kati ya masuala muhimu ambayo yalijadiliwa wakati wa mkutano.Kwa ajili ya maslahi ya ufanisi, kila moja ya nchi tatu walipewa masuala fulani ya kufuatilia kwa bidii, na ilikubaliwa kwamba kutakuwa na mikutano ya kila miezi miwili ya kutathmini suala walikubaliana juu. mkutano wa kwanza watakuwa mjini Nairobi na moja baadae mjini Kigali.

CHADEMA WADAI KUNASA WARAKA WA SIRI WA CCM

slaa-2 
Aliyekuwa mgombea UWT Taifa, Maryrose Magige akionyesha kadi ya Chadema aliyokabidhiwa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Wilbrod Slaa wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika Viwanja vya Shule ya Msingi Ukombozi Manzese Dar es Salaam .
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimedai kunasa waraka wa siri wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) unaokwenda kwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya, Jaji Joseph Warioba, ukimshinikiza kukubali mapendekezo yao.
Waraka huo wa CCM uliosainiwa na Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini, Jitu Vrajilal Soni una lengo la kupinga mapendekezo mbalimbali yaliyomo katika Rasimu ya Mabadiliko ya Katiba Mpya iliyozinduliwa Juni 3 mwaka huu.
Makamu Mwenyekiti wa Kanda ya Mashariki na Pwani, Mabere Marando akihutubia mkutano wa chama hicho uliofanyika katika viwanja cha Shule ya Msingi Ukombozi, Manzese jijini jana alidai waraka huo una lengo la kuvuruga mchakato wa kupata Katiba Mpya yenye manufaa kwa Watanzania wote.
Marando akisoma baadhi ya mapendekezo ya CCM yaliyomo katika waraka huo kwenda kwa Jaji Warioba kumtaka kuviondoa vipengele vilivyomo ndani ya Rasimu ya Mabadiliko ya Katiba Mpya vinavyohusu Tunu ya Taifa, kuwa bila kufanya hivyo hakutakuwa na tija ya uwajibikaji.Kusoma zaidi bofya
Alizitaja tunu hizo za taifa kuwa ni kuwa utu, uzalendo, uadilifu, umoja, uwazi, uwajibikaji na lugha ya Taifa ambazo Chadema wanaziunga mkono zipite na kuwa sheria.
“Sisi Chadema tunaona zinafaa kutokana na umuhimu wake lakini CCM wamemwambia Warioba aondoe neno uwazi wakiwa na maana ya kuwa wanataka mambo yao yasiwekwe wazi,” alisema Marando.
Marando ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho alisema, Jaji Warioba amependekeza utajiri wa taifa uendelezwe na kuzuia mtu kumnyonya mwenzake jambo ambalo CCM wamelipinga.
“CCM katika waraka huo ibara ya 11.2 na 11.3 wamemwambia Warioba viondolewe, sasa viongozi wa CCM na Chadema ni kina nani wanawapenda wananchi wake,” aliwauliza wananchi waliojitokeza katika mkutano huo na kujibiwa na kelele kuwa ni Chadema.
Marando alisema katika kipengele cha maadili ya taifa na jamii kinachosema viongozi wanatakiwa kuzingatia uongozi, utoaji wa huduma, kufanya usawa na kupiga vita rushwa mapendekezo ambayo yakipita kuwa sheria yatasaidia kupunguza tatizo la rushwa la utoaji wa huduma uliotukuta.
“CCM ambao hawaonyeshi dhamira ya kumkomboa mwananchi wake, wamemwambia Warioba kuyaondoa maadili hayo kwani hayafai, sasa kupiga watu, kula rushwa kweli liondolewe? Hawa CCM kweli hawataki tupate katiba ya kuwakomboa wananchi,” alisema Marando na kuongeza:
“Kama hiyo haitoshi wamesema kitendo cha wananchi kumwajibisha mbunge wao kama hatakuwa anatimiza majukumu yake nao wamesema mapendekezo hayo hayafai. Kweli CCM hawataki tupate Katiba Mpya.”
Chanzo:Mwananchi

MATOKEO YA UCHAGUZI WA MADIWANI ARUSHA

wafuasi-2
MATOKEO NI KAMA IFUATAVYO
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), `kimefunika’ katika uchaguzi mdogo wa madiwani uliofanyika kwenye kata nne za Jimbo la Arusha Mjini uliofanyika jJumapili.
Matokeo katika vituo mbalimbali vya kata hizo nne ambayo kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), yalionyesha Chadema ikiongoza kwa idadi kubwa ya kura zilizopigwa kwenye vituo 136 vya kupigia kura huku kikifuatiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Matokeo kamili katika vituo hivyo yalikuwa kama ifuatavyo:-

KATA YA KALOLENI:
Matokeo ya jumla Chadema 1,470, CCM 530, CUF 275 na Demokrasia Makini 2, Kwa matokeo hayo Emmanuel Kessy wa Chadema alitangazwa mshindi.
Kituo kidogo A, Chadema kilikuwa kimenyakua kura 51, CCM 25 na CUF 11.
Kituo B1, Chadema 68, CCM 19 na CUF 17 huku katika kituo A4, Chadema kilipata kura 67, CCM 20 na CUF 9, Kituo A3 Chadema kura 57, CCM 25 na CUF 7.
Katika kituo cha B4, Chadema kura 54, CCM 30 na CUF 9, B3 Chadema 54, CCM 15 na CUF 9, wakati B2 Chadema kilipata kura 73, CCM 9 na CUF 4 na kituo A2, Chadema 69, CCM 21 na CUF 8.
Kituo cha A1, Chadema kura 60, CCM 15 na CUF 11 na B6 Chadema kura 41, CCM 21 na CUF kura 9.
Katika kituo cha B5, Chadema kilipata kura 50, CCM 22 na CUF 10.
Katika kituo cha AICC Nursery School, kituo kidogo cha A2 Chadema kura 58, CCM 18 na CUF 17, A4 Chadema kura 62, CCM 22 na CUF 6, A3 Chadema 44, CCM 22 na CUF 5, E2 Chadema 58, CCM 22 na CUF 4, E3 Chadema 53, CCM 20 na CUF 5.
Aidha, katika kituo cha E4 Chadema 40, CCM 20 na CUF 5, B1 Chadema 57, CCM 18 na CUF 9, A1 Chadema 60, CCM 24 na CUF 5.
Kituo cha Shule ya Sekondari Kaloleli, A1,Chadema 52, CCM 17, CUF 15 huku katika kituo cha A2, Chadema kura 97, CCM 23, CUF 19 na kituo A3, Chadema 46, CCM 20 na CUF 20.
Kituo cha A4 Chadema 46, CCM, 16, CUF 16, kituo B1 Chadema 56, CCM 10, CUF 16 na kituo B2 Chadema 42, CCM 23 na CUF 15.Kituo B3, Chadema 53, CCM 17 na CUF 11, kituo B4 Chadema 38 CCM 16 na CUF 13

KATA YA ELERAI
Katika Kituo cha Shule ya Sekondari Kata ya Elerai, Ofisi ya Katibu Tarafa, pia Chadema kimeendelea kuongoza katika matokeo ya awali.Matokeo ya jumla Chadema kura 2,047, CCM 1,471, CUF 302, CCK 3, na TLP 1. Mshindi ni Mhandisi Jeremiah Mpinga wa Chadema.
Kituo A1, Chadema kura 37, CCM 17, CUF 3, TLP na CCK 0. Kituo A2, Chadema kilipata kura 28, CCM 13, CUF 2, CCK na TLP 0.Kituo A3, Chadema kura 31, CCM 19, CUF 2, CCK na TLP 0 huku katika kituo A4 , Chadema 21, CCM 12, CUF 6 , TLP na CCK 0.
Vituo vingine katika kata hiyo ni pamoja na B1 ambacho Chadema waliongoza kwa kura 42, CCM 15, CCK na TLP 0 huku katika kituo C1, Chadema 42, CCM 15, CCK na TLP 0.
Kwa upande wa kituo cha C2, CCK 0, CCM 12, Chadema 35, CUF 3 na TLP 0, Kituo kingine cha Katibu Tarafa Ofisi, CCM kilipata kura 26, Chadema 25 na CUF huku cha B1 Chadema wakijipatia kura 43, CCM 23, CUF 5.
Kituo B2, Chadema 34, CCM 24, CUF na TLP 0, kituo B3 CCM kura 26, Chadema 32, CUF 3, kituo cha Shule ya Msingi Burka B2, CCM ilinyakua kura 31, Chadema 30, CUF 2 na kituo B3, CCM ikipata kura 41, Chadema 43, CUF 5 wakati CCK na TLP wakiambulia patupu.
Aidha katika kituo hicho cha Shule ya Msingi Burka,B4 CCM ilipata 32, Chadema 28, CUF 3, TLP na CCK 0, vituo vya C1, CCM kura 26, Chadema 43, CUF 5 na kile cha C2, CCK 0, CCM 31, Chadema 43, CUF 7 na TLP 0.

KATA YA KIMANDOLU
Katika Kata ya Kimandolu kwenye kituo Shule ya Msingi Suye, CCM na Chadema ndivyo pekee vilisimamisha wagombea.
Katika kituo cha A1, CCM ilipata kura 15, Chadema 47, A2 CCM 24, Chadema 39, kituo A3 CCM 14, Chadema 35, kituo B1 CCM 25, Chadema 56, kituo B2 CCM 25, Chadema 48, kituo C2 CCM 30, Chadema 39 na kituo C1 CCM 11, Chadema 48.
Kituo cha ofisi ya Kata ya Kimandolu, kituo A1 Chadema ilipata kura 97, CCM 22, kituo A2 Chadema 88, CCM 29, kituo A3 Chadema 81, CCM 31, kituo A5 Chadema 90, CCM 41, kituo A6 Chadema 87, CCM 28, kituo A7 Chadema 70, CCM 35, kituo B1 Chadema 84, CCM 27 na kituo B2 Chadema 82, CCM 27.
Kituo B3 Chadema 78, CCM 37, kituo B4 Chadema 87, CCM 36, kituo cha B5 Chadema 69, CCM 23, kituo C1 Chadema 97, CCM 28, kituo C2 Chadema 103,CCM 21, kituo C3 Chadema 79, CCM 32, kituo C4 Chadema 84 CCM 42 na kituo C5 Chadema 87 CCM 41.
Kituo cha Shule ya Msingi Kimandolu kwenye kituo A1 CCM ilipata kura 34, Chadema 64, kituo B2 CCM 26, Chadema 66, kituo B4 CCM 37, Chadema 74, kituo A5 CCM 48, Chadema 58, kituo A3 CCM 48, Chadema 53, kituo B5 CCM 24, Chadema 65, kituo C1 CCM 27, Chadema 74, kituo C3 CCM 36, Chadema 64, kituo C5 CCM 31, Chadema 78, kituo A2 CCM 27, Chadema 87, kituo A4 CCM 33, Chadema 57, kituo B2 CCM 30, Chadema 77 na kituo C2 CCM 30,Chadema 65.

KATA YA THEMI
Katika kata hiyo iliyokuwa na vituo 12, Chadema ilinyakua jumla ya kura 674, CCM 326 na CUF 307. Waliojiandikisha walikuwa 6,387, waliopiga kura 1,319, kura halali 1,307 ambapo zilizoharibika 12, kwa mujibu wa Msimamizi wa Uchaguzi wa kata hiyo, Eveka Mboya ambaye pia alimtangaza mshindi kuwa ni Kinabo Edmund wa Chadema.
Matokeo kwa baadhi ya vituo yalionyesha kuwa katika Kituo cha Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Themi, CCM 9, Chadema 36, CUF 0, kituo A2 CCM kura 13, CUF 3 na Chadema 23, kituo cha A3 , Chadema 33, CCM 16, CUF 2 na katika kituo A1, CCM ikijipatia kura 44, CUF 1, Chadema 53.Katika kituo A2, CCM 29, Chadema 57 na CUF 4 huku kile cha A3 CCM iki
 

TAMKO LA MH. RAIS KUHUSU MLIPUKO WA BOMU ULIOTOKEA ARUSHA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa ya tukio la leo, Jumapili, Mei 5, 2013 la mlipuko kwenye Kanisa Katoliki la Mt. Joseph Mfanyakazi la Olasiti Jijini Arusha. Tukio hilo la kigaidi limesababisha mtu mmoja kupoteza maisha na wengine 40 kujeruhiwa. Rais Kikwete analaani vikali shambulio hilo lililofanywa na mtu au watu katili, waovu na wenye dhamira mbaya na nia mbaya kwa Tanzania na watu wake. 

Rais Kikwete ameagiza vyombo vya usalama nchini kumsaka mtu au watu waliohusika na kitendo hicho kiovu na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria. Vile vile Rais Kikwete amewataka wananchi wote kuwa watulivu wakati Serikali na vyombo vyake inaendelea kufuatilia tukio hili. Tutawasaka popote walipo na kupambana nao bila huruma. Aidha, tutakabiliana na aina yoyote ya uhalifu nchini iwe ni ugaidi au aina yoyote ya uhalifu wa namna hiyo au wa namna nyingine, uwe na chimbuko lake ndani ya nchi ama nje ya nchi yetu. Kamwe hatutakubali kuwaacha wavuruge amani na usalama wa Tanzania na watu wake. Rais anaamini kuwa Serikali, kwa msaada na ushirikiano wa wananchi, watu hao watapatikana na kuadabishwa ipasavyo.

Aidha, Rais Kikwete anatoa rambirambi za dhati ya moyo wake kwa wafiwa na wale wote ambao wamejeruhiwa katika tukio hilo. Anaungana nao katika machungu na msiba. Rais pia anawaombea wote walioumia katika tukio hili wapate nafuu ya haraka na waendelee na shughuli zao za ujenzi wa taifa.

Rais Kikwete vilevile anatoa pole nyingi kwa viongozi na waumini wa Kanisa Katoliki kwa tukio hili la kusikitisha na kuvurugika kwa ibada na shughuli yao muhimu ya uzinduzi wa Kanisa lao.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU,
DAR ES SALAAM
5 Mei, 2013

MAFUNZO YA MUDA MFUPI KWA VIONGOZI

 Rais Jakaya Kikwete Afunga Mafunzo ya muda mfupi kwa viongozi yumo mbunge wa kigoma kaskazini-Chadema Zitto Kabwe,Mbunge wa Kinondoni-CCM Iddi Azani,mbunge wa kawe-Chadema Halima Mdee,Mbunge wa Biharamulo-CCM,Dk Athanas Mbassa,Mbunge wa Mtera Mh. Livingstone Lusinde na mbunge wa viti maalum Ester Bulaya


Baadhi ya Wabunge walikuwa wakichukua mafunzo ya muda mfupi kwa viongozi katika Kambi ya Mgambo kikosi cha 835 wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na waheshimiwa wabunge waliohitimu mafunzo maalumu ya JKT
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe, akiapa mbele ya kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Muhingo Rweyemamu, hayupo pichani, wakati wakimaliza mafunzo ya JKT, katika Kambi ya Mgambo kikosi cha 835 wilayani Handeni Mkoa wa Tanga. 

 

 ZIARA YENYE KUDUMISHA MAHUSIANO MAZURI BAINA YA TANZANIA NA CHINA

Rais Dkt Jakaya Mrisho kikwete wakigonganisha Glasi na Rais Xi Jinping wa China wakati wa dhifa ya kitaifa iliyofanyika ikulu jijini Dar Es Salaam juzi jioni.Rais Xi Jinping wa China yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.Ni ziara yake ya kwanza barani Afrika tangu achaguliwe kuliongoza taifa la China hivi karibuni na Tanzania inakuwa nchi ya kwanza kuitembelea barani Afrika

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais wa China Xi Jinping wakiweka mashada ya maua katika makaburi ya wataalamu wa China waliofariki wakati wa ujenzi wa Reli ya TAZARA.Viongozi hao waliweka mashada hayo ya maua katika makaburi hayo yaliyopo katika kijiji cha Majohe,Ukonga jijini Dar es Salaam.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na mke wa Rais wa China Mama Peng Liyuan wakiweka maua katika makaburi ya wataalamu wa China waliofariki wakati wa ujenzi wa Reli ya TAZARA huko katika kijiji cha Majohe,Ukonga nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam huku Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wa Rais Xi Jinping wakishuhudia
Rais Jakaya Kikwete na Rais wa China Xi Jinping Waweka Shada la Maua katika makaburi ya wataalamu wa China waliofariki wakati wa ujenzi wa Reli ya TAZARA

Tume ya kukusanya maoni ya Katiba yaendelea kukusanya maoni 26-07-2012

Bi. Aziza Juma (27), mkazi wa Wilaya ya Kishapu,
 mkaoni Shinyanga akitoa akitoa maoni yake kuhusu 
Katiba Mpya kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba 
ilipofanya mkutano kijijini hapo juzi (Alhamisi, Julai 26)
Wananchi wa Kijiji cha Maganzo, Kata ya Songwa, 
Wilayani Kishapu mkoani Shinyanga wakifuatilia mkutano
 wa kukusanya maoni ya wananchi kuhusu Katiba
 Mpya juzi (Alhamisi, Julai 26, 2012)
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mstaafu
 Joseph Warioba katika picha ya kumbukumbu na 
wanafunzi wa Shule ya Msingi Michungwani iliyopo 
 kijiji cha michungwani, Kata ya Segera wilayani 
Handeni mkoani Tanga mara baada ya mkutano wa
 kukusanya maoni kuhusu Katiba Mpya.

Taarifa ya CCM kwa umma kuhusu posho za Wabunge  
11/12/2011
Hivi karibuni kumeibuka mjadala juu ya ongezeko la posho za wabunge kwa karibu ya asilimia mia mbili (200%) kutoka shilingi Elfu sabini mpaka shilingi Laki Mbili.

Malipo hayo yaliyoibua mjadala baina ya wadau mbalimbali, ni yale yanayohusisha posho ya kikao cha bunge kwa siku.

Chama Cha Mapinduzi kimefuatilia kwa ukaribu suala hilo la nyongeza ya posho hiyo ya wabunge kama lilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari na baadae kutolewa maelezo na Katibu wa Bunge Dokta Thomas Kashilila na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa ANNE MAKINDA.
Kwa namna suala lenyewe linavyopewa msukumo, CCM imeona si vema kuliacha bila kutoa msimamo wake kama ifuatavyo:-

i. Linapotekelezwa jambo lolote kwa kigezo cha ugumu wa maisha au kupanda kwa gharama za maisha, ni lazima jambo husika lilenge kutatua ugumu huo wa maisha kwa makundi yote katika jamii na si kwa makundi machache ndani ya jamii.

ii. Kwa kuongeza kiwango hicho cha posho kwa wabunge ni kuongeza pengo/tofauti ya mapato kati ya wenye nacho na wasionacho katika jamii yetu hasa kwa kuegemea baadhi ya makundi.

iii. Bunge ni chombo muhimu cha kutunga sheria, kinapoibuka na madai kama hayo yaliyoainishwa na Spika wa Bunge kuwa sababu za kuongezeka kwa posho hizo kunatokana na kupanda kwa gharama za maisha mjini Dodoma, ndiko kulikosababisha hofu na mashaka miongoni mwa watanzania. Na kwakweli swali kubwa hapa inakua je, maisha yanapanda Dodoma pekeake na kwa wabunge tu?

Hivyo basi CCM inashauri kwa kuzingatia masilahi mapana ya nchi na jamii yetu kwa ujumla, waheshimiwa wabunge wetu na mamlaka zingine zinazohusika na swala hili, kulitafakari upya jambo hili. Tunaamini busara itatumika kuachana na jambo hili, kwani kuendelea nalo kunaweza kutafisiriwa ni kuwasaliti watendaji katika sekta nyingine wakiwemo Walimu, askari, Madaktari na wengineo.

Ni muhimu ifahamike kuwa kuongoza ni kuonesha njia, hivyo si sahihi kwa wabunge kuonsha njia kwa kujiongezea posho peke yao kwa kisingizio cha ugumu wa maisha huku wakiwaacha wananchi ambao ndiyo wanaowawakilisha bungeni wakikosa nafasi ya kupunguza ugumu wa maisha unaowakabili, jambo ambalo ni hatari.

Katika hatua nyingine Chama Cha Mapinduzi Kinawapongeza sana watanzania kwa ujumnla wao, bila kujali tofauti yao, kwa kushiriki kwa amani na utulivu, maadhimisho ya miaka hamsini ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Ushiriki wao kwa pamoja, umeyafanya maadhimisho hayo yafane sana. CCM inaamini kuwa maadhimisho haya ya miaka hamsini yatatumika kuendelea kujenga uzalendo, umoja na mshikamano wan chi yetu katika kufikia maendeleo.

Imetolewa na:-
Nape M. Nnauye,
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA
ITIKADI NA UENEZI
11/12/2011
Hotuba ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuahirisha Mkutano wa Tano wa Bunge la Tanzania mjini Dodoma  
19/11/2011
UTANGULIZI,

Mheshimiwa Spika,
1. Kwanza kabisa napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa Rehema kwa kutufikisha salama siku ya leo tunapohitimisha Mkutano wa Tano wa Bunge lako Tukufu ulioanza tarehe 08 Novemba 2011. Tuna kila sababu ya kumshukuru kwa kuwa tumetekeleza majukumu yote yaliyopangwa kwenye Ratiba kwa Amani, Utulivu na Ufanisi Mkubwa. Ninawashukuru Waheshimiwa Wabunge wote, kwa kuwa, kwa pamoja tumefanikisha Mkutano huu.

Mheshimiwa Spika,
2. Napenda nitumie nafasi hii ya mwanzo kabisa kumpongeza Mheshimiwa Dkt. Dalaly Peter Kafumu kwa kuchaguliwa kuwa Mbunge Mpya wa Jimbo la Igunga kwa kura nyingi kupitia Chama Cha Mapinduzi katika Uchaguzi Mdogo uliofanyika tarehe 02 Oktoba 2011. Kuchaguliwa kwake kunadhihirisha imani kubwa waliyonayo Wananchi wa Igunga kwake na kwa Chama Cha Mapinduzi. Vilevile, kunadhihirisha kwamba Chama Cha Mapinduzi bado ni Chama imara, Chama cha Wakulima na Wafanyakazi na Chama chenye Mvuto Mkubwa kwa Watanzania. Napenda pia kumpongeza Mheshimiwa Mohammed Said Mohammed kwa kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Bunge la Muungano kupitia Baraza la Wawakilishi la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Mheshimiwa Spika,
3. Tangu tulipohitimisha Mkutano wa Nne wa Bunge lako Tukufu, kumekuwa na matukio mbalimbali yaliyosababisha majeruhi na kupoteza maisha ya ndugu, jamaa na marafiki zetu. Napenda kutumia nafasi hii kuwapa pole wote walioathirika kwa namna moja au nyingine kutokana na matukio hayo. Aidha, kwa wale waliopoteza maisha,

namwomba Mwenyezi Mungu aziweke Roho za Marehemu wote Mahali Pema Peponi. Amen. Kipekee, napenda kutumia nafasi hii pia kuwatakia kheri Waheshimiwa Wabunge wote ambao katika kipindi hiki wamepata misukosuko ya maradhi na baadhi yao bado wako Hospitalini Ndani na Nje ya Nchi kwa matibabu. Napenda kuungana na Familia zao kumwomba Mwenyezi Mungu awaponye haraka na awape nguvu ya kurejea katika afya zao ili waweze kujiunga na Familia, Wapiga Kura wao na Watanzania wote kwa ujumla katika ujenzi wa Taifa letu.

Maswali

Mheshimiwa Spika,
4. Katika Mkutano huu wa Tano, jumla ya Maswali ya Msingi 123 na ya Nyongeza 289 yalijibiwa na Serikali. Aidha, Maswali 8 ya Msingi na 5 ya Nyongeza yalijibiwa kwa utaratibu wa Maswali ya Papo kwa Papo kwa Waziri Mkuu.

Miswada

Mheshimiwa Spika,
5. Katika Mkutano huu, Waheshimiwa Wabunge walipata fursa ya kujadili Miswada ifuatayo:
i) Muswada wa Sheria ya Ununuzi wa Umma wa Mwaka 2011 [The Public Procurement Act, 2011]; na

ii) Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa Mwaka 2011 [The Constitutional Review Act, 2011].

Taarifa Mbalimbali

Mheshimiwa Spika,
6. Vilevile, katika Mkutano huu, zilitolewa Taarifa mbili ambazo ni Taarifa ya Kamati ya Nishati na Madini juu ya Uendeshaji wa Sekta Ndogo ya Gesi Nchini na Taarifa ya Kamati Teule ya Bunge.

Kauli za Serikali

Mheshimiwa Spika,
7. Katika Mkutano huu pia, Serikali ilitoa Tamko kuhusu Fujo na Vurugu Zilizojitokeza hivi karibuni katika Mikoa ya Mbeya na Tabora.

8. Nitumie fursa hii kuwashukuru Waheshimiwa Wabunge wote walioshiriki katika Mijadala ya Miswada na Taarifa hizo.

Hotuba ya Mheshimiwa Rais ya Tarehe 18 Novemba 2011

Mheshimiwa Spika,
9. Nianze kwa kumshukuru sana Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Hotuba aliyoitoa jana tarehe 18 Novemba 2011 katika Ukumbi wa Karume, Viwanja vya Mwalimu Nyerere - Barabara ya Kilwa, Dar es Salaam. Mheshimiwa Rais amefafanua kwa kina maeneo muhimu yanayohusu Mwenendo wa Uchumi katika Nchi yetu, hususan Mfumuko wa Bei, Kushuka kwa Thamani ya Shilingi na kupanda kwa Bei ya Mafuta na Chakula katika Soko la Dunia. Vilevile, alielezea vizuri suala la matumizi ya Fedha za Kigeni katika ununuzi wa bidhaa na huduma mbalimbali hapa Nchini.

10. Kama alivyoeleza Mheshimiwa Rais, suala la Mdororo wa Kiuchumi uliopo na kupanda kwa Bei ya Mafuta na Chakula katika Soko la Dunia kumeathiri siyo Tanzania pekee, bali Nchi nyingi Duniani zikiwemo za Ulaya na Afrika, na hata jirani zetu. Ili kupata uelewa mpana kuhusu suala hili tumekubaliana kwamba Gavana wa Benki Kuu ataandaa Semina kuhusu masuala hayo itakayofanyika wakati wa Mkutano wa Sita wa Bunge ambapo tutapata fursa ya kujadili kwa kina hali ilivyo ya Mwenendo wa Viashiria vya Uchumi wa Nchi yetu athari zake na hatua zinazochukuliwa na Serikali.

Mheshimiwa Spika,
11. Katika Hotuba yake, Mheshimiwa Rais alizungumzia pia kwa kina Mchakato wa Maandalizi ya Mabadiliko ya Katiba ambapo Bunge lako Tukufu limepitisha Muswada wa Sheria wa Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011 jana tarehe 18 Novemba 2011. Ninaamini kwa dhati kabisa kuwa maelezo yale ya Mheshimiwa Rais yatatoa Majibu sahihi na uelewa wa pamoja kwa Watanzania wenzangu kuhusu Mchakato wa Mabadiliko ya Katiba.
Uelewa huo wa pamoja, kwa maoni yangu, utatuwezesha Watanzania wote kujiandaa na kushiriki kwenye hatua zinazofuata katika Mchakato huo kwa Utulivu, Amani, Umoja na Mshikamano.

12. Kwa namna ya pekee, napenda kukushukuru wewe binafsi Mheshimiwa Spika kwa jinsi ulivyoongoza Mjadala huu. Ninawashukuru pia Wenyeviti wa Bunge kwa jinsi walivyosimamia na kuongoza Mjadala pale ulipojadiliwa.

Mheshimiwa Spika,
13. Muswada tulioupitisha ulisimamiwa kwa umahiri mkubwa na Kamati ya Kudumu ya Katiba, Sheria na Utawala ya Bunge. Kwa moyo wa dhati naishukuru Kamati kwa kazi nzuri ya kuchambua na kutoa ushauri kwa Serikali na hivyo kuonesha njia iliyo bora katika kutekeleza jukumu hili muhimu tulilohitimisha jana. Kipekee, ninawashukuru Mheshimiwa Pindi Chana, Mbunge na Mwenyekiti wa Kamati; na Mheshimiwa Anjellah Kairuki, Mbunge na Makamu Mwenyekiti wa Kamati kwa kuongoza na kusimamia mjadala wa kuandaa Muswada uliopitishwa jana na Bunge lako Tukufu. Hawa wote ni kina Mama na kina Mama wakipewa nafasi wanaweza.

14. Napenda pia kuchukua nafasi hii kuishukuru kwa moyo wa dhati kabisa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa ushirikiano mkubwa iliyoutoa wakati wote wa uandaaji na Mjadal wa Muswada huo.

15. Napenda pia kuwashukuru Mheshimiwa Celina Ompeshi Kombani, Mbunge wa Ulanga Mashariki na Waziri wa Katiba na Sheria; na Mheshimiwa Jaji Frederick Mwita Werema, Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kazi kubwa waliyoifanya katika kipindi chote cha maandalizi na Majadiliano ya Muswada huo. Ninawashukuru pia Watendaji wote wa Wizara ya Katiba na Sheria kwa utaalam na ushirikiano mkubwa waliouonesha ambao uliwawezesha Viongozi hao kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi mkubwa.

16. Mwisho lakini siyo kwa umuhimu, Muswada huo ulipitiwa pia na Wasomi, Wanataaluma, Makundi mbalimbali ya Jamii na Wadau wengi ambao siyo rahisi kuwataja wote hapa. Itoshe tu kusema, Serikali inawapongeza Wadau wote kila moja kwa nafasi yake kwa namna walivyoshiriki katika kufanikisha mjadala wa Muswada uliopitishwa na Bunge lako Tukufu jana.

17. Kwa ujumla wenu mmeandika historia mpya katika kulitumikia Taifa letu kwa kufanikisha hatua ya Mwanzo na ambayo ninaamini ilikuwa ngumu katika kuelekea Uundaji wa Katiba Mpya. Katiba ambayo kama alivyosema Mheshimiwa Rais, itaendana na Mafanikio na Changamoto za Miaka 50 ya Uhuru, Miaka 47 ya Mapinduzi ya Zanzibar, Miaka 47 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Katiba ambayo italipeleka Taifa letu Miaka 50 mingine ijayo kwa Utulivu, Amani, Umoja na Mshikamano. Niwashukuru Waheshimiwa Wabunge wote kwa kazi kubwa mliyoifanya katika kujadili Muswada huo na hatimaye kuupitisha.

Kazi tuliyonayo mbele yetu ni kutekeleza yale ambayo Mheshimiwa Rais ameyaelekeza kwa Watanzania wote kushiriki kikamilifu katika hatua zinazofuata.

Mheshimiwa Spika,
18. Nitumie nafasi hii pia kuwaomba Watanzania wote kwamba sasa tuungane kwa pamoja kutekeleza hatua itakayofuata ambayo ni kutoa Maoni yetu kwa Tume itakayoundwa na Waheshimiwa Ma-Rais wetu wa pande zote mbili – Tanzania Bara na Zanzibar. Aidha, nawaomba Viongozi na Wanachama wa Vyama vyote vya Siasa kupongeza hatua iliyofikiwa na kukubali Muswada huu ambao tayari umepitishwa kwa maslahi ya Taifa letu.
Wito wangu kwa Wananchi wote ikiwa ni pamoja na Vyama vya Siasa ni kuungana kwa pamoja katika hatua muhimu inayokuja ambayo itahusisha Watanzania wote ya kutoa Maoni ya Katiba tunayoitaka. Nawasihi Watanzania wenzangu kuzingatia yale yote aliyotuasa Mheshimiwa Rais katika Hotuba yake ili hatua zote kueleza Katiba Mpya zifanyike kwa Amani na Utulivu. Kwa pamoja tutaweza kufikia lengo tulilojiwekea na kuandika historia mpya ya Nchi yetu.

HALI YA CHAKULA

Mheshimiwa Spika,
19. Nchi yetu imekuwa ikikabiliwa na hali ya ukame wa mara kwa mara kwa muda mrefu, hususan tangu mwaka 2006. Hali hii imesababisha upungufu wa Chakula katika baadhi ya Mikoa ambayo imekuwa ikiathirika zaidi na ukame. Hata hivyo, Chakula ambacho kimekuwa kinazalishwa katika maeneo yenye Mvua za kutosha kimewezesha Nchi yetu kuendelea kujitosheleza kwa Chakula, kwa kiwango kikubwa. Kwa mfano, katika mwaka 2010/2011 uzalishaji wa mazao ya Chakula unakadiriwa kufikia Tani Milioni 12.81 ikilinganishwa na mahitaji ya jumla ya Tani Milioni 11.50 za Chakula kwa mwaka 2011/2012. Uzalishaji huu unatosheleza mahitaji ya Chakula kwa Asilimia 111, sawa na ziada ya Tani Milioni 1.31. Ziada hiyo kwa kiasi kikubwa inatokana na mazao yasiyo ya Nafaka. Hivyo, uhaba wa Nafaka ni kiasi cha Tani 410,000 Nchini kote na upungufu huo wa Nafaka upo zaidi kwenye baadhi ya Mikoa inayokabiliwa na ukame.

20. Tathmini ya kina ya hali ya Chakula na Lishe Nchini iliyofanywa mwezi Agosti na Septemba, 2011 inaonesha kuwepo kwa jumla ya Watu 1,062,516 katika Wilaya 52 za Mikoa 15 wanaokabiliwa na upungufu wa Chakula (Acute Food Insecurity) kwa viwango mbalimbali.
Wananchi hao wanahitaji Tani 38,843 za Chakula cha msaada kwa kipindi cha Miezi mitatu kuanzia Mwezi Oktoba hadi Desemba 2011. Hadi tarehe 31 Oktoba 2011, jumla ya Tani 13,905 za Chakula zilikuwa zimechukuliwa kutoka maghala ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) na kusambazwa katika maeneo hayo yenye uhaba wa Chakula, na kazi hiyo inaendelea.

Mheshimiwa Spika,
21. Pamoja na jitihadi za Serikali za kupeleka Chakula cha Msaada katika maeneo yenye upungufu wa Chakula, natoa Wito kwa Wananchi kwenye maeneo yaliyo na upungufu wa Chakula kutumia Mvua kidogo zinazonyesha Nchini hivi sasa kulima Mazao yanayostahimili ukame kama vile Mtama, Viazi, na Mihogo ili kujiongezea Chakula.

HALI YA UNUNUZI WA MAHINDI

Mheshimiwa Spika,
22. Serikali inazingatia kuhakikisha kunawepo na akiba ya kutosha ya Chakula kwa ajili ya kukabiliana na upungufu wa Chakula Nchini. Hadi tarehe 30 Juni 2011, Wakala wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA) ulikuwa na akiba ya Tani 154,506 za Mahindi na Tani 1.96 za Mtama. Wakala umelenga kununua Tani 200,000 za Mahindi katika kipindi cha msimu wa mwaka 2011/2012.
Hadi kufikia tarehe 30 Oktoba 2011, Wakala ulikuwa umenunua jumla ya Tani 114,117 kutoka Mikoa iliyozalisha ziada ya Nyanda za Juu Kusini. Katika kipindi hicho, jumla ya Tani 49,792 za Mahindi zilikuwa zimepelekwa kwenye Mikoa yenye upungufu wa Chakula inayohudumiwa na Maghala ya Wakala yaliyopo Arusha, Shinyanga na Dodoma na kazi hiyo inaendelea.

Mheshimiwa Spika,
23. Zoezi la kununua, kuhifadhi na kusafirisha Mahindi kutoka maeneo yenye ziada kwenda maeneo yenye upungufu linakabiliwa na changamoto mbalimbali. Changamoto hizo ni pamoja na ufinyu wa Bajeti, uwezo mdogo wa kuhifadhi nafaka zinazonunuliwa na kasi ndogo ya kusafirisha Mahindi kutoka katika maeneo yenye ziada kwenda kwenye maeneo yenye upungufu.

Mheshimiwa Spika,
24. Bajeti iliyotengwa na Serikali katika Mwaka wa Fedha 2011/2012 kwa ajili ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) haitoshi kutekeleza malengo ya Wakala. Kati ya Tani 114,117 za Mahindi ambazo zimepokelewa katika Vituo vya ununuzi, Wakala umeweza kulipia Tani 80,615 tu na kushindwa kulipia Tani 33,492 zilizopokelewa.
Kufikia tarehe 30 Oktoba 2011, Wakala ulikuwa unadaiwa jumla ya Shilingi Bilioni 13.62 na Wakulima waliouza Mahindi yanayohifadhiwa na Wakala katika Vituo vya Makambako, Songea na Sumbawanga.

Mheshimiwa Spika,
25. Ili kukabiliana na changamoto hiyo, Serikali imeiruhusu NFRA kukopa Shilingi Bilioni 20 kutoka katika Mabenki ya Biashara Nchini na mazungumzo na Mabenki hayo yanaendelea. Pamoja na hatua hiyo, Serikali pia imeiruhusu NFRA kuuza Mahindi Tani 50,000 kwa Shirika la Chakula Duniani (WFP), ambapo tayari Tani 10,000 zimenunuliwa. Pia NFRA imeruhusiwa kuuza Tani 40,000 kwa Wafanyabiashara Binafsi.

26. Hatua hizi zitawezesha Wakala kulipia madeni ya Wakulima, kuendelea na ununuzi, uhifadhi na usafirishaji wa Mahindi kwenda katika maeneo yenye upungufu wa Chakula. Kuhusu kasi ya kusafirisha Mahindi, Serikali inaangalia uwezekano wa kuiwezesha Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) kuongeza kasi ya kusomba Mahindi kutoka kwenye Maghala ya Sumbawanga na Mpanda kwenda Shinyanga. Aidha, Serikali inaangalia uwezekano wa kutumia magari ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika usafirishaji wa Mazao haya. Ni imani ya Serikali kuwa jitihada hizi zitasaidia kukabiliana na uhaba wa Chakula kwenye maeneo yenye ukame.

MPANGO WA UWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA KILIMO, NA USALAMA WA CHAKULA (TAFSIP)

Mheshimiwa Spika,
27. Ili Nchi yetu ijitosheleze katika Chakula na Lishe na kuongeza kipato katika Kaya pamoja na Kukuza Uchumi wa Nchi, Tanzania inatekeleza Mpango wa Uwekezaji katika Sekta ya Kilimo na Usalama wa Chakula yaani “Tanzania Agriculture and Food Security Investment Plan” (TAFSIP). Huu ni Mpango wa Miaka 10 kuanzia mwaka 2011/2012 hadi 2020/2021 ambao unawaleta pamoja Wadau wote katika Sekta pana ya Kilimo Tanzania Bara na Visiwani.
28. Utekelezaji wa Mpango huu utaiwezesha Sekta ya Kilimo kukua kwa Asilimia 6 au zaidi kwa mwaka. Katika kufanikisha mpango huu, Serikali imeridhia kuongeza Bajeti ya Kilimo hadi kufikia Asilimia 10 kwa kuzingatia utekelezaji wa Azimio la Maputo la mwaka 2003 ambapo Wakuu wa Nchi za Afrika ikiwemo Tanzania walikubaliana kuwa kila Nchi itaongeza Bajeti yake katika Sekta ya Kilimo angalau kufikia Asilimia 10 ya Bajeti ya Serikali.

Mheshimiwa Spika,
29. Wadau mbalimbali walishiriki kuandaa Mpango huu ikiwa ni pamoja na Taasisi mbalimbali za Umma na Binafsi, Wadau wa Maendeleo wa ndani na nje ya Nchi, Wanataaluma mbalimbali, Jumuiya za Uchumi za Kikanda, Umoja wa Afrika, Ubia Mpya wa Maendeleo ya Afrika (New Partnership for Africa’s Development-NEPAD) na Programu ya Kuendeleza Kilimo Barani Afrika (Comprehensive Africa Agriculture Development Programme-CAADP). Aidha, mchakato wa kutengeneza Mpango huu ulihusisha mikutano mbalimbali ya kukusanya maoni katika Kanda zote Tanzania Bara na Visiwani ambapo wadau mbalimbali walipata nafasi ya kuchangia katika uundwaji wa mpango huu.

30. Serikali, Wadau wa Maendeleo wa ndani na nje ya Nchi, Sekta Binafsi, NGOs, Jumuiya za Uchumi za Kikanda na Wakulima wadogo kwa wakubwa watashiriki katika utekelezaji wa Mpango huu. Katika kipindi cha miaka mitano (5) kuanzia mwaka 2011/2012 hadi 2015/2016, Mpango huu unategemea kutumia kiasi cha Shilingi Trilioni 8.75, sawa na Wastani wa Shilingi Trilioni 1.7 kwa mwaka. Uwekezaji huo utakuwa katika maeneo yafuatayo:

i) Kuongeza uzalishaji, tija na Kilimo cha Kibiashara (Shilingi Trilioni 6.22);

ii) Kutekeleza mipango ya Umwagiliaji na Matumizi Bora na Endelevu ya Ardhi na Maji (Shilingi Trilioni 1.2);

iii) Kufanya Maboresho ya Sera na kujenga uwezo wa Taasisi mbalimbali (Shilingi Bilioni 681.13);

iv) Kuendeleza Miundombinu ya Vijijini, Masoko na Biashara (Shilingi Bilioni 357.26);

v) Kuwezesha kufikiwa kwa Usalama wa Chakula na Lishe (Shilingi Bilioni 211.4);

vi) Kukabiliana na mabadiliko ya Tabia Nchi na Majanga ya Asili (Shilingi Bilioni 66.31); na

vii) Kuendeleza Sekta Binafsi (Shilingi Bilioni 15.56).

Mheshimiwa Spika,
31. Hivi karibuni Mkutano wa Kazi (Business Meeting) kwa ajili ya Mpango wa Uwekezaji katika Sekta ya Kilimo (TAFSIP) ulifanyika tarehe 10 – 11 Novemba 2011, katika Hoteli ya Blue Pearl, Dar es Salaam. Mkutano huo uliongozwa na Mheshimiwa Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hapo tarehe 10 Novemba 2011 na Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 11 Novemba 2011. Mkutano huo ulihudhuriwa na Wadau mbalimbali toka Wizara na Taasisi za Serikali, Taasisi za Wakulima, Sekta Binafsi, Mashirika ya Kiraia na Wabia wa Maendeleo.
Katika Mkutano huo makubaliano yalifikiwa kuhusu maeneo ya Kipaumbele ya Mpango, gharama za Mpango na Ratiba ya Utekelezaji wake. Katika Mpango huu, mbinu na msukumo mpya kupitia uratibu, ukusanyaji wa Rasilimali na ushirikishaji wa Sekta Binafsi vitatumika katika kuongeza kasi katika utekelezaji wa Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Nchini (Agricultural Sector Development Programme – ASDP) pamoja na Miradi na Programu mbalimbali zinazoendelea kutekelezwa katika Sekta ya Kilimo hapa Nchini.

Mheshimiwa Spika,
32. Kama ilivyo katika utekelezaji wa Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Nchini (ASDP) kwa upande wa Tanzania Bara na Mpango wa Sekta ya Kilimo (ASP) kwa upande wa Tanzania Zanzibar, utekelezaji wa Programu ya TAFSIP utahusisha kwa karibu Mipango ya Maendeleo ya Wilaya kama ilivyo sasa. Ni matumaini ya Serikali kwamba utekelezaji wa Mpango huu utaiwezesha Sekta ya Kilimo kuchangia katika Ukuaji wa Uchumi Nchini, Kuongeza Pato la Mkulima na kuhakikisha kwamba Taifa linajitosheleza kwa Chakula na Lishe.

MAANDALIZI YA MSIMU WA KILIMO WA MWAKA 2011/2012

Mheshimiwa Spika,
33. Serikali imefanya Maandalizi muhimu ya Msimu wa Kilimo wa Mwaka 2011/2012 ambapo imejikita katika upatikanaji na usambazaji wa Mbolea na Mbegu, maandalizi ya Vocha kwa ajili ya Pembejeo za Ruzuku na upatikanaji wa Madawa ya Kudhibiti uharibifu wa Mazao.

Upatikanaji na Usambazaji wa Mbolea

34. Mahitaji ya Mbolea Nchini yanakadiriwa kufikia Tani 400,000 kwa mwaka. Hadi kufikia tarehe 3 Novemba 2011, jumla ya Tani 246,454 za Mbolea, sawa na Asilimia 61.6 ya mahitaji zilikuwa zimesambazwa katika Mikoa mbalimbali Nchini. Kati ya hizo, Tani 81,294 ni Mbolea ya kupandia ambayo inatosheleza mahitaji ya Wakulima wa Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini pamoja na Mikoa ya Kigoma, Kagera, Manyara na Mwanza ambayo Wakulima huanza kupanda mwezi Novemba kila mwaka. Kwa Wakulima wa Mikoa inayopanda mwezi Januari na Februari kila mwaka, Tani 129,711 za Mbolea ya kupandia zitakazotumika katika Mikoa hiyo zinatarajiwa kupatikana kabla ya mwisho wa mwezi Desemba 2011.

Upatikanaji na Usambazaji wa Mbegu Bora

Mheshimiwa Spika,
35. Mahitaji ya Mbegu Bora za Nafaka na Mikunde Nchini yanakadiriwa kufikia Tani 30,000 kwa mwaka. Hadi tarehe 3 Novemba 2011, jumla ya Tani 23,437, sawa na Asilimia 78 ya mahitaji zilikuwa zimesambazwa katika Mikoa mbalimbali Nchini. Kiasi cha Mbegu kilichopo kinatosheleza mahitaji ya Wakulima wanaopanda Mazao hayo katika mwezi wa Novemba kila Mwaka. Aidha, Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika inaendelea kuwasiliana na Makampuni ya Mbegu ili kiasi cha Mbegu kilichobaki kipatikane kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Utekelezaji wa Mpango wa Ruzuku ya Pembejeo za Kilimo

Mheshimiwa Spika,
36. Katika msimu wa Kilimo wa mwaka 2011/2012, jumla ya Tani 18,157 za Mbegu bora za mazao ya Mpunga na Mahindi zitasambazwa kwa Wakulima kwa utaratibu wa Vocha. Vilevile, Tani 180,000 za Mbolea ya kupandia na kukuzia mazao hayo zitasambazwa kwa utaratibu huo huo kwa Wakulima 1,800,000. Mapendekezo ya mgawanyo wa Vocha katika Mikoa 20 na Wilaya 96 zinazohusika na Ruzuku hiyo yamekamilika na wahusika wameshapatiwa taarifa. Vilevile, Ruzuku ya Mbegu Bora za Mtama kiasi cha Tani 356 zitatolewa kwa Wakulima 127,300 wa Mikoa yenye ukame ya Singida, Shinyanga, Mwanza, Tabora, Dodoma na Mara. Pia, Ruzuku ya Mbegu bora za zao la Alizeti kiasi cha Tani 50 zitatolewa kwa Wakulima 10,392 wa Mikoa ya Singida na Shinyanga. Jumla ya Vocha 5,400,000 zitasambazwa katika Mikoa 20.

Mheshimiwa Spika,
37. Pamoja na taarifa hii, naomba nitumie fursa hii kutoa Taarifa ya Upatikanaji na Usambazaji wa Mbegu za Pamba kwa Msimu wa 2011/2012. Hadi kufikia tarehe 16 Novemba 2011, Tani 15,000 za Mbegu za Pamba zimesambazwa Vijijini, kati ya Tani 20,000 zilizopangwa kusambazwa msimu huu.

38. Pamoja na hali hii, limejitokeza kundi la Walanguzi wa Mbegu za Pamba katika Wilaya za Bariadi, Maswa, Magu, Meatu na Kishapu ambao wanapita Vijijini wakinunua Mbegu za Pamba walizosambaziwa Wakulima kwa kuwapa bei kubwa ili kununua Mbegu hizo na kuuza kwa bei kubwa. Kwa kuwa Mkulima akishauza Mbegu zake hawezi kupata mbegu zingine tena; jambo hili ni la hatari sana kwa Wakulima, zao la Pamba na Uchumi wa Taifa. Aidha, kwa Mkulima mwenyewe, kuuza mbegu yake ya Pamba ni kujiua yeye mwenyewe.

39. Mbinu nyingine inayotumika ni kwa Walanguzi wa Mbegu na baadhi ya Viongozi kupanga watu wengi katika Vituo vya kununulia Mbegu wakijifanya kuwa ni Wakulima, kwa lengo la kuwakusanyia mbegu nyingi ili waiuze kwa bei kubwa.

Mheshimiwa Spika,
40. Serikali imepokea majina ya Walanguzi wengi wa Mbegu katika Wilaya za Meatu, Bukombe, Bariadi, Bunda, Magu na Kishapu na operesheni ya kuwakamata inaendelea. Hivyo, Serikali inawatahadharisha wote (Walanguzi, Wakulima na wengine) wanaoshiriki katika hujuma hii, kuacha mara moja. Hatua kali za Kisheria zitachukuliwa kwa wote wanaouza na wale wanaonunua Mbegu za Pamba kinyume cha Sheria.

Madawa ya Kudhibiti Uharibifu wa Mazao

Mheshimiwa Spika,
41. Hadi tarehe 3 Novemba 2011, tayari lita 3,072 za Madawa ya kudhibiti Viwavi Jeshi, Lita 2,000 za Madawa ya kudhibiti Ndege aina ya Kwelea Kwelea na Kilo 1,200 za kudhibiti Panya zilikuwa zimesambazwa katika Mikoa mbalimbali Nchini. Aidha, Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika imeandaa zabuni itakayowezesha kuingizwa Nchini Lita 4,000 za Dawa za kudhibiti Ndege aina ya Kwelea Kwelea; Lita 7,000 za kudhibiti Nzige Wekundu; Lita 5,000 za kudhibiti Viwavi Jeshi; na Kilo 1,400 za kudhibiti Panya.

Mheshimiwa Spika,
42. Kwa kuzingatia maandalizi hayo ya Kilimo yaliyofanyika na ili kupata ufanisi katika uzalishaji katika msimu wa Kilimo wa mwaka 2011/2012, suala la usimamizi wa dhati litazingatiwa. Viongozi kuanzia ngazi ya Wizara hadi ngazi ya Vijiji wasimamie upatikanaji, usambazaji wa pembejeo na upatikanaji wa ushauri wa kitaalam kwa Wakulima wetu Vijijini. Vilevile, Wataalam wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, TAMISEMI na Halmashauri zote Nchini wanapaswa kutoka Maofisini waende Vijijini kufuatilia na kusimamia Kilimo. Mikoa na Halmashauri yenye Maafisa Ugani wengi katika ngazi ya Makao Makuu wahamishiwe kwenye ngazi ya Kata na Vijiji ili kuwasaidia kwa karibu Wakulima Vijijini.

HALI YA AJIRA

Mheshimiwa Spika,
43. Viongozi na Jamii kwa ujumla wamekuwa wakizungumzia tatizo la Ajira hasa kwa Vijana. Athari za ukosefu wa Ajira hususan kwa Vijana ni kubwa na ni mbaya katika mustakabali wa Taifa letu. Tatizo hili linachangia kwa kiasi kikubwa umaskini Nchini kwani yeyote asiyekuwa na Ajira hana kipato. Watu wasio na ajira ni rahisi kujikuta wanaishi kwa njia zisizokubalika katika Jamii zikiwemo za Wizi, Unyang’anyi, Biashara za Ngono, Matumizi ya Dawa za Kulevya, Uhalifu na kadhalika.

44. Katika mwaka 2001, kiwango cha ukosefu wa Ajira Nchini kilikuwa Asilimia 12.9. Kwa matokeo ya utafiti wa Nguvu Kazi na Ajira ya mwaka 2006, Nguvu Kazi Nchini ilikuwa Watu Milioni 18.8. Kati yao, Watu Milioni 2.2 walikuwa hawana ajira sawa na Asilimia 11.7 ya Nguvu Kazi yote Nchini. Makadirio ya kiwango cha ukosefu wa Ajira Nchini katika mwaka 2011 ni Asilimia 10.7 ya Nguvu Kazi ya Taifa ya Watu Milioni 22.2. Kwa kiwango hicho inakadiriwa kuwa Idadi ya Watu wasiokuwa na Ajira kwa sasa ni Milioni 2.4.

Takwimu pia zinaonesha kuwa mwaka 2006 wakati wa utafiti wa Nguvukazi (Labour Force Survey) Watu Milioni 14.9 walikuwa wameajiriwa kwenye Sekta Rasmi na Watu Milioni 1.7 walikuwa wameajiriwa katika Sekta Isiyo Rasmi. Kwa mwaka 2011 inakadiriwa kuwa Watu Milioni 17.3 wameajiriwa kwenye Sekta Rasmi na Watu 2.5 wameajiriwa kwenye Sekta Isiyo Rasmi. Sekta ya Kilimo (kwa tafsiri pana) ndiyo inayoongoza kwa kuajiri Asilimia 75 ya Nguvu Kazi. Sekta Isiyo Rasmi inaajiri Asilimia Tisa, Serikali Asilimia 2.4 na Mashirika Asilimia 0.4.

45. Utafiti unaonesha pia kuwa ukosefu wa ajira unawaathiri zaidi Vijana wa umri kati ya umri wa miaka 15 hadi 24 ambao wanamaliza Sekondari, Vyuo vya Kati na Vyuo Vikuu. Aidha, tatizo hili ni kubwa zaidi kwa Wanawake kuliko Wanaume. Ongezeko kubwa la Watu wasiyo na kazi linatokana na kasi kubwa ya ongezeko la Watu wenye umri wa kufanya kazi ikilinganishwa na kasi ndogo ya ongezeko la nafasi za ajira ambalo limekuwepo kwa miaka mingi sasa.

Mheshimiwa Spika,
46. Hata hivyo, suala hili la ukosefu wa Ajira siyo la Tanzania tu, bali ni la Nchi nyingi Duniani. Kwa mfano, kwa mwaka 2011, wakati kiwango cha ukosefu wa Ajira Tanzania ni Asilimia 10.7, Nchi ya Afrika Kusini ni Asilimia 25.0, Hispania Asilimia 21.5, Ureno ni Asilimia 12.4, Iran ni Asilimia 11.5, Ufaransa ni Asilimia 9.5, na Marekani ni Asilimia 9.

Mheshimiwa Spika,
47. Serikali inatambua kuwepo kwa mahitaji makubwa ya ajira Nchini. Sera ya Taifa ya Ajira ya mwaka 2008 inatambua kuwepo kwa tatizo la ukosefu wa ajira. Sera hiyo inalenga pamoja na mambo mengine kuandaa mazingira wezeshi kwa wasiokuwa na ajira kujiajiri wenyewe na kuainisha maeneo ya kiuchumi yanayoweza kukuza ajira na kuweka mikakati ya kutumia maeneo hayo kukuza Uchumi. Aidha, Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2010 inalitambua suala hili. Kwa mfano, Ibara ya 77 ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi inaeleza ifautavyo:

“Chama Cha Mapinduzi kinatambua kwamba katika kipindi hiki suala la ajira hususani Ajira ya Vijana imekuwa nyeti. Hii ni kwa sababu idadi ya Vijana wanaofuzu Elimu ya Msingi, Sekondari, Vyuo na Vyuo Vikuu kila mwaka ni kubwa sana. Idadi hiyo inakuzwa pia na Vijana wanaomaliza Mafunzo ya JKT. Vijana wote hawa ni Nguvukazi ya Taifa ambayo inaweza kutumika katika kazi na shughuli halali za ujenzi wa Nchi”.

Aidha, Ibara ya 78 inaainisha mambo yanayotakiwa kushughulikiwa na Serikali ili kujenga fursa za Ajira hasa kwa Vijana.

Mheshimiwa Spika,
48. Serikali ya Chama cha Mapinduzi inafanya juhudi kubwa kukabiliana na tatizo hili. Serikali yenyewe imekuwa ni miongoni mwa Waajiri wakubwa Nchini na itaendelea kuajiri Vijana wengi kadri hali ya kiuchumi itakavyoruhusu. Aidha, Serikali itaendelea kujenga mazingira ya kupunguza ukosefu wa ajira kwa kuchukua hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuimarisha Sekta ya Kilimo ambayo inaajiri Asilimia kubwa ya Nguvu Kazi na kuchangia katika kutoa huduma za Ardhi, kupanda, kuvuna, kutunza na kuuza mazao. Hatua nyingine ni kupanua mafunzo ya VETA; kupanua na kuboresha Elimu ya Msingi, Sekondari, Vyuo vya Ufundi na Vyuo Vikuu na kuimarisha mitaala ya Elimu ili Wahitimu waweze kujiajiri. Vilevile, Wananchi watahamasishwa kujiunga katika SACCOs na VICOBA na kuwawezesha kimtaji, kuweka mazingira mazuri ya kukuza Sekta Binafsi na Uwekezaji, na kuvutia Wawekezeji wa Ndani na Nje ya Nchi. Aidha, Serikali itandelea kuwawezesha Waajiri na wale wanaotafuta kazi kupata taarifa za hali ya Soko la Ajira.

49. Ningependa tukumbushane kuwa tunapozungumzia ajira hatuna maana ya ajira za kulipwa mishahara tu bali ni pamoja na ajira binafsi katika Kilimo, Uvuvi, Ufugaji, Biashara na kadhalika. Hivyo, suala la kupunguza ukosefu wa ajira si suala la Serikali pekee bali ni pamoja na Sekta Binafsi. Kila mmoja wenu afanye kila liwezekanalo kuongeza Ajira Nchini. Tukiwa na dhamira ya pamoja tutaweza.

HALI YA USALAMA NCHINI

Mheshimiwa Spika,
50. Hali ya Usalama katika Nchi yetu ni shwari ikiwa ni pamoja na maeneo ya Mipakani na eneo la Bahari ya Hindi, licha ya kuwepo kwa matishio ya Uharamia katika Pwani ya Nchi za Afrika Mashariki. Tarehe 3 Oktoba 2011, Maharamia wenye asili ya Somalia walivamia ufukwe wa Bahari ya Hindi eneo la Mafia kwa lengo la kutaka kuteka meli inayotumika katika utafiti wa mafuta.
Jaribio hilo lilidhibitiwa na Wanajeshi wetu wa Jeshi la Wanamaji wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania. Katika jaribio hilo, Maharamia Saba (7) walikamatwa na hatua za Kisheria dhidi yao zinaendelea kuchukuliwa. Vilevile, kulikuwa na matukio mengine matatu ya uharamia ambapo yalidhibitiwa na hakuna madhara yoyote yaliyotokea kwa upande wa Tanzania.

51. Napenda kutumia fursa hii kulipongeza Jeshi la Wananchi kwa kazi nzuri inayofanya kwa kushirikiana na Jumuiya ya Kimataifa kudhibiti vitendo vya Uharamia katika Pwani ya Nchi za Afrika Mashariki.

Mheshimiwa Spika,
52. Kama mnavyofahamu, kwa sasa katika Ukanda wa Afrika Mashariki kumekuwa na matishio ya Ugaidi, hususan katika Nchi jirani. Hivi karibuni kumezuka matishio ya Kigaidi Nchini Kenya kufuatia Serikali ya Kenya kufunga Mpaka wake na Somalia kama njia ya kupambana na Kikundi cha Wapiganaji wa Kundi la Al-Shabab. Kutokana na hali hii, Nchi yetu imeimarisha Ulinzi katika mipaka yake yote ambapo Idara ya Uhamiaji imewaelekeza Maafisa Uhamiaji wa Mikoa yote na Vituo vyote vya kuingia Nchini kuimarisha Doria na misako katika maeneo yao ili kuzuia Wahamiaji Haramu, hususan Raia wa Somalia wengi wao wakitokea Kenya kuingia Nchini. Aidha, Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Vyombo vingine vya Dola wameweka mikakati ya kukubaliana na tishio hili, ikiwa ni pamoja na kuweka Boti za Doria katika Pwani ya Bahari ya Hindi na Askari wa Doria katika maeneo ya Mipakani.

53. Natoa wito kwa Watanzania wote, hasa wale wanaoishi maeneo ya mipakani mwa Nchi yetu kutoa taarifa katika Vyombo vyetu vya Ulinzi na Usalama pale watakapoona Mtu au Watu ambao nyendo zao hazieleweki. Aidha, niwatake Viongozi wa Serikali za Mitaa na Vijiji kuendelea na zoezi la kuhakiki watu katika maeneo yao na kuchunguza Watu wanaokuja na kuishi katika Vijiji na Mitaa yao bila ya kutoa taarifa kwa Viongozi wa maeneo hayo.

Kazi ya kulinda Nchi yetu na mipaka yake itafanikiwa endapo Wananchi wote watashirikiana kwa karibu na Vyombo vya Ulinzi na Usalama kwa kutoa taarifa pale inapobidi.

KUIBUKA KWA MATUKIO YA UHALIFU KWA WATU WENYE WALEMAVU WA NGOZI

Mheshimiwa Spika,
54. Mwaka 2007, Nchi yetu ilikumbwa na tatizo la imani za kishirikina kwamba Viungo vya Watu Wenye Walemavu wa Ngozi (Albino) vinaweza vikaleta utajiri. Imani hiyo potofu ilisababisha kuibuka kwa kasi kwa vitendo vya mauaji na unyama wa kukata viungo vya Ndugu zetu Walemavu wa Ngozi. Vitendo hivyo vilisikitisha sana, kuona Watu wachache kwa tamaa za kupata utajiri wanawageuza Binadamu wenzao kama Wanyama. Suala hili lilichafua jina na Sifa ya Tanzania ambayo siku zote imekuwa ni Nchi ya Amani, Umoja na Mshikamano.

Mheshimiwa Spika,
55. Serikali kwa kushirikiana na Mashirika Yasiyokuwa ya Kiserikali, Taasisi mbalimbali za Ndani na Nje ya Nchi na Madhehebu ya Dini kwa pamoja tulisimama kidete kupambana na vitendo hivyo. Vilevile, Serikali kupitia Vyombo vya Dola ilichukua hatua kali dhidi ya wahusika. Kwa kuzingatia hilo, Watuhumiwa 94 walikamatwa na Kesi 11 za Mauaji ya Walemavu wa Ngozi zilifikishwa Mahakamani. Kati ya hizo, Kesi Tisa (9) zimekwisha sikilizwa na Kesi Sita (6) zimeshatolewa hukumu ambapo Watuhumiwa Nane (8) wamehukumiwa Kunyongwa. Kutokana na jitihada hizo, Matukio ya Mauaji na Kujeruhiwa kwa Walemavu wa Ngozi yalionekana kupangua sana.

56. Pamoja na hatua hizo zilizochukuliwa na Serikali, bado hivi karibuni kumeripotiwa matukio mawili ya uhalifu yaliyohusisha kukatwa kwa Viungo vya Watoto wawili Wenye Ulemavu wa Ngozi kwa nyakati tofauti. Matukio hayo yalitokea Mikoa ya Mwanza na Shinyanga ambapo tarehe 14 Oktoba 2011 Mtoto wa Darasa la Tatu,

Adam Robert, mwenye Miaka 13 mkazi wa Kijiji cha Nyaluguguna, Kata ya Nyijuda, Wilayani Geita alivamiwa na kukatwa vidole vitatu vya mkono wa kulia mbele ya Wazazi wake na mhusika kutoweka navyo. Katika tukio la pili, tarehe 22 Oktoba 2011, Mtoto Kulwa Lusana, mwenye Miaka 16 Mkazi wa Kijiji cha Mbizi, Kata ya Mega Wilayani Kahama, Mkoa wa Shinyanga alikatwa mkono wa kulia na mhusika kutoweka nao. Watoto hawa wote wanaendelea kupata Matibabu, mmoja katika Hospitali ya Wilaya ya Geita na mwingine Hospitali ya Wilaya ya Kahama.

57. Katika Matukio haya mawili Watu wa karibu na majeruhi hawa wanahisiwa kuhusika kwa namna moja au nyingine na matukio haya wakiwemo Wazazi wao ambao wamekamatwa na Upelelezi wa Mashauri yao unaendelea.

58. Unyama huu unaofanywa na Watu wachache wenye uchu wa utajiri wasiokuwa na utu, unachafua jina zuri la Tanzania Duniani kote na kudhalilisha Watanzania wote. Hivyo, Wadau wote tunahitaji kukemea vitendo hivyo, kuvilaani na kuhakikisha uhalifu huo unatokomezwa.

59. Napenda kusisitiza tena kwamba Watu Wenye Ulemavu wa Ngozi ni Binadamu kama walivyo Binadamu wengine. Wanastahili haki ya kuishi kwa amani na kufurahi katika Nchi yao. Hakuna Mtu, Kikundi chochote ambacho kina haki ya kumfanya Mlemavu wa Ngozi aishi kwa wasiwasi au kwa hofu katika Nchi yake kwa sababu yoyote ile.

60. Narudia tena kuagiza Vyombo vya Dola kuongeza Nguvu katika kuhakikisha Vitendo vya uhalifu dhidi ya Watu Wenye Ulemavu wa Ngozi vinadhibitiwa ipasavyo na Wadau wote tushirikiane kuhakikisha Ndugu zetu hawa wanalindwa. Aidha, natoa wito kwa Wananchi wote, Wazazi, Vijana na Wadau wengine kwamba suala la ulinzi wa Ndugu zetu Walemavu wa Ngozi ni letu sote.

Ni wajibu wa kila mmoja wetu kutoa taarifa juu ya Watu wanaonesha kuwa na mwenendo unaotia mashaka kuhusiana na Ndugu zetu hawa. Tunahitaji ushirikiano katika suala hili, hata kama wanaohisiwa ni Wazazi tafadhali toeni taarifa. Viongozi wa Madhehebu mbalimbali ya Dini, Viongozi wa Serikali na Wazee Maarufu, katika maeneo yenu Kemeeni imani hii potofu inayosababisha Mauaji ya Watu Wenye Ulemavu wa Ngozi na kuwaeleza madhari ya Imani za Kishirikina kwa Ndugu zetu hawa.

61. Aidha, Viongozi wa Serikali za Mitaa, mna jukumu la kubaini makazi ya Walemavu wa Ngozi na kuwapatia ulinzi kila inapobidi. Aidha, ni muhimu kupata namba za simu za Wazazi/Walezi wao ili waweze kufuatiliwa. Kwa upande wa Ndugu zetu Walemavu wa Ngozi, nawaomba ninyi pia toeni taarifa pale mnapoona kufuatwa fuatwa na Watu ambao mnahisi wana nia mbaya, au kutia mashaka.

UTAMADUNI NA MICHEZO

Timu ya Mpira wa Miguu – TAIFA STARS

Mheshimiwa Spika,
62. Watanzania wote tunafahamu na kutambua kuwa Timu yetu ya Taifa ya Mpira wa Miguu –TAIFA STARS - ilicheza na Timu ya Taifa ya Chad huko N’djamena, Chad tarehe 11 Novemba, 2011. Matokeo ya mechi hiyo yalikuwa ni ushindi kwa Timu yetu kwa kuifunga Timu ya Taifa ya Chad Mabao 2-1.

63. Mechi ya marudiano ilifanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam tarehe 15 Novemba, 2011 na matokeo yalikuwa Chad 1 na Tanzania 0. Kwa matokeo hayo, Timu ya Taifa imefaulu kusonga mbele na hivyo kuingia katika kundi C ambalo lina Timu za Morroco, Ivory Coast na Gambia. Mechi hizo ni muhimu sana kwa Taifa kwa kuwa ni maandalizi ya kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika Brazil mwaka 2014. Pamoja na kwamba Timu yetu imefuzu kuingia katika Makundi, lakini ukweli ni kwamba safari yetu bado ni ngumu na ndefu.

Timu tulizopangwa nazo ni ngumu na ni magwiji wa Soka Barani Afrika. Ili kukabiliana na Timu hizo na kupata ushindi tunahitaji maandalizi ya kutosha na Michezo ya kujipima nguvu kwa Timu yetu. Napenda kuwaasa Vijana wetu kuwa, hata kama tungekuwa na Kocha Mzuri kama kiasi gani, lakini kama hawatafanya Mazoezi ya kutosha, kujituma kwa hali na mali kutambua kuwa wanabeba Bendera ya Taifa bado hatutashinda.

Mheshimiwa Spika,
64. Wakati wa mechi za ugenini na zile ya nyumbani, Timu yetu inahitaji kutiwa moyo, kusaidiwa kisaikolojia na zaidi ya yote kuungwa mkono kifedha ili iweze kushinda.
Ninawasihi Watanzania wenzangu tuiunge mkono Timu yetu ya Taifa kwani Ushindi wa Timu yetu ni Ushindi wa Taifa; Ni Ushindi wa Watanzania Wote, Ni Njia ya Kuitangaza Tanzania Duniani na Sote Kama Watanzania Tutapata Sifa na Kujivunia Ushindi Huo.

65. Nawaomba Watanzania, kila mmoja kwa nafasi yake tuisaidie Timu yetu kwa hali na mali ili iweze kuibeba na kuipeperusha bendera ya Tanzania kwa ujasiri mkubwa.
Mlima Kilimanjaro

Mheshimiwa Spika,
66. Kuna suala la Mlima Kilimanjaro ambalo nalo pia haliwezi kuachwa hivi hivi. Tutakumbuka kuwa miezi ya karibuni kulikuwa na kampeni ya kuupigia kura Mlima Kilimanjaro ili uweze kuchanguliwa na kuwa miongoni mwa Maajabu Saba Mapya ya Dunia. Kulikuwa na vivutio 28 vilivyochaguliwa kutoka vivutio 77 kutoka Nchi 220 zilizoshindanishwa mwaka 2007. Tangu Julai 2009, kura zilikuwa zikipigwa na hatima yake ilikuwa ni tarehe 11 Novemba 2011. Matokeo rasmi ya kura hizo yatatangazwa mwanzoni mwa mwaka 2012 lakini katika matokeo ya awali, Mlima Kilimanjaro haukupata nafasi ya kushinda na kuwemo katika Maajabu Saba ya Dunia. Hata hivyo, ulipata nafasi ya kupita katika mchujo wa kwanza na kuwa miongoni mwa vivutio 14 kati ya 28, vilivyoshinda kura za awali. Hili ni jambo la kujivunia na naomba nitumie fursa hii kuwashukuru Watanzania wote ambao walishiriki kutuma ujumbe mfupi wa maneno (sms) ama emails zao kuupigia kura Mlima Kilimanjaro.

Mheshimiwa Spika,
67. Kwa kuwa Maajabu hayo Saba yalikuwa yameamuliwa kwa kura, ninaamini, na ni maoni yangu kuwa Watanzania wengi hawakutumia nafasi hiyo vizuri kuupigia Mlima Kilimanjaro kura. Aidha, taarifa ya kushindanishwa kwa Mlima Kilimanjaro hazikutolewa na kutangazwa mapema na Wizara yenye dhamana na Taasisi zake. Hii ni Changamoto kwetu sote lakini zaidi kwa Wizara ya Maliasili na Utalii ambayo kimsingi ilikuwa na jukumu la kuwa mstari wa mbele katika kuwaelimisha Wananchi kuhusu Mashindano hayo tangu suala hili lilipojulikana mapema mwezi Julai 2011. Pamoja na kwamba hatukupata nafasi, naomba nichukuwe nafasi hii kuzipongeza Kampuni za Simu za Airtel na VODACOM kwa kukubali kufanyakazi na Serikali kufikisha ujumbe kwa Watanzania kuhusu kuupigia Kura Mlima Kilimanjaro. Matarajio ni kwamba Kampuni zingine nazo zitashiriki katika maeneo mengine ya Maendeleo kwa nyakati zijazo.

68. Ninawapongeza Wananchi wote wa Ndani na Nje walioitikia wito wa kuupigia Kura Mlima Kilimanjaro. Aidha, nitumie fursa hii kuzitaka Wizara zote kujipanga vizuri wakati wote kunapotokeza Mashindano ya Kimataifa katika Sekta zao kwa kuweka Uzalendo mbele na kuwa tayari kuipigania Nchi yetu. Ufahamu wa Wananchi upewe kipaumbele na Wananchi washirikishwe kikamilifu.

KUVUTIA UWEKEZAJI KIKANDA

Mheshimiwa Spika,
69. Serikali imedhamiria kuongeza kasi ya kuhamasisha na kuvutia Wawekezaji wa Ndani na wa Nje kuwekeza Nchini ili hatimaye tuweze Kukuza Uchumi na Kuondoa Umaskini kwa haraka. Dhamira hiyo inaendana na matakwa ya Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano hadi 2015 ambao unasisitiza na kutoa kipaumbele katika kuvutia Uwekezaji Nchini. Aidha, ili kuleta uwiano wa maendeleo endelevu Nchini, Serikali inahimiza Mikoa na Wilaya kuunganisha nguvu na kutangaza fursa mbalimbali za Uwekezaji Kikanda kwa kuzingatia Jiografia, Hali ya Hewa, Miundombinu na fursa za Uwekezaji zilizopo katika Mikoa husika.

Mheshimiwa Spika,
70. Ili kutekeleza Azma hiyo, tarehe 17 Oktoba 2011, Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alifungua Kongamano la Uwekezaji katika Ukanda wa Ziwa Tanganyika unaojumuisha Mikoa ya Rukwa, Kigoma na Mkoa tarajiwa wa Katavi. Kongamano hilo ni la kipekee na la aina yake kufanyika katika Mikoa hiyo, ambayo iko nyuma kimaendeleo ikilinganishwa na Mikoa ya Kaskazini, lilikuwa na lengo la kutangaza fursa mbalimbali za Uwekezaji zilizopo katika Ukanda huo kwa Wawekezaji wa Nje na wa Ndani. Miongoni mwa mambo muhimu ambayo Wadau na Washiriki wa Kongamano hilo, walijifunza na kupata uzoefu ni pamoja na:
i) Mikoa hiyo mitatu ina fursa za kipekee na Rasilimali nyingi zenye tija kubwa na zinazofanana katika Sekta za Kilimo, Mifugo, Uvuvi, Utalii, Madini, Misitu na Ufugaji Nyuki. Aidha, Mikoa hiyo ina ardhi nzuri yenye rutuba, Hali ya Hewa inayofanana, imeunganishwa na Reli ya Kati na yote ipo kwenye Ukanda wa Ziwa Tanganyika. Hivyo, ina fursa kubwa ya kuunganisha nguvu na kuvutia Wawekezaji wa ndani na nje kwa pamoja ili kuongeza kasi ya maendeleo katika Ukanda huo;

ii) Mikoa hiyo na Wilaya zake imetenga maeneo maalum ya Uwekezaji na Ardhi kwa ajili ya kuvutia Uwekezaji katika Sekta zenye fursa kubwa za Kiuchumi. Sekta hizo ni za Kilimo, Mifugo, Uvuvi, Makazi, Madini, Viwanda na Biashara.

Hatua hii ni nzuri kwa kuwa itapunguza urasimu katika kuwawezesha Wawekezaji kupata ardhi kwa ajili ya Uwekezaji;

iii) Aidha, Serikali kwa upande wake inajitahidi kuweka Mazingira wezeshi ya kuvutia Uwekezaji ili kufungua Milango zaidi ya Uwekezaji katika maeneo hayo. Mfano wa jitihada ambazo Serikali imeanza kuzifanya ni kuwekeza katika Miundombinu muhimu, hususan Barabara za Mikoa ya Kigoma na Rukwa na kuziunganisha na Mikoa mingine na Nchi Jirani. Miundombinu mingine ni kuimarisha Reli ya Kati, Viwanja vya Ndege, Nishati ya Umeme, Madaraja, Usafiri wa Majini na kushirikiana na Sekta Binafsi kuhakikisha kunakuwepo Hoteli nzuri kwa ajili ya Watalii katika Hifadhi za Taifa za Katavi, Gombe na Mahale;

iv) Zaidi ya hayo ilionekana kuwa upo umuhimu mkubwa kwa Viongozi wa Mikoa, Wilaya na Halmashauri kuhamasisha Wawekezaji wengi wa ndani kuchangamkia fursa za Uwekezaji zilizopo Nchini ili waweze kunufaika na Vivutio vingi vinavyotolewa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania; na

v) Viongozi wa Mikoa na Wilaya wakijipanga vizuri wanaweza kushirikiana na Kituo cha Uwekezaji kuandaa na kuendesha Makongamano ya Kikanda ya kutangaza kwa pamoja fursa za Kuvutia Wawekezaji katika maeneo yao.

Mheshimiwa Spika,
71. Kwa kuzingatia uzoefu huo, natoa wito kwa Wakuu wa Mikoa pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri wote Nchini kushirikiana na Kituo cha Uwekezaji kuanza kuandaa Mipango ya Uwekezaji na kutenga maeneo ya Uwekezaji katika maeneo yao ili kuwarahisishia Wawekezaji wa Ndani na Nje kuwekeza kulingana na fursa zilizopo katika Mikoa na Halmashauri husika.

Mheshimiwa Spika,
72. Sambamba na hatua hiyo, moja ya Maazimio ya Kongamano la Uwekezaji katika Ukanda wa Ziwa Tanganyika ni kuendeleza utaratibu huo katika Kanda nyingine. Kwa kuzingatia Azma hiyo, narejea wito nilioutoa wakati nilipofanya Majumuisho ya Ziara yangu katika Mkoa wa Mara mwezi Septemba 2011 ambapo nilishauri Viongozi wa Mkoa huo wawasiliane na Mikoa jirani kuona uwezekano wa kufanyika kwa Kongamano la Uwekezaji katika Kanda ya Ziwa Victoria. Mimi naamini kuwa Mikoa ya Kanda hiyo inayojumuisha Mikoa ya Mara, Mwanza,
Kagera, Shinyanga na Mikoa tarajiwa ya Geita na Simiyu ina Vivutio vingi na fursa nyingi za Uwekezaji zinazofanana katika Sekta za Kilimo, Mifugo, Uvuvi, Viwanda, Utalii, Madini, Maliasili, n.k. Vilevile, Mikoa hii ina Jiografia, Hali ya Hewa inayofanana na shughuli nyingi za Kibiashara na Kijamii zinazowiana. Hivyo, Mikoa hii inaweza kuunganisha nguvu katika kutangaza na Kuvutia Uwekezaji kwa pamoja.

Mheshimiwa Spika,
73. Mikoa mingine iliyopendekezwa kuunganisha nguvu na kuvutia Uwekezaji kwa pamoja ni ile ya Kanda ya Pwani inayojumuisha Mikoa ya Tanga, Pwani na Morogoro. Napenda kutumia fursa hii kutoa wito kwa Viongozi wa Mikoa niliyoitaja na mingine kujipanga vizuri Kikanda, kuibua fursa za Uwekezaji na kuunganisha nguvu katika kutangaza Vivutio vya Uwekezaji katika maeneo yao. Aidha, nawashauri kutumia kikamilifu uzoefu wa Mikoa ambayo tayari imefanya Makongamano ya Kuvutia Uwekezaji, ikiwemo Kilimanjaro, Tanga, Rukwa na Kigoma.

Mheshimiwa Spika,
74. Katika Hotuba ya Ufunguzi ya Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa Kongamano la Uwekezaji wa Ukanda wa Ziwa Tanganyika, alisema na kusisitiza (kwa lugha aliyoitumia siku hiyo) kuwa:

“It is a statement of fact that Investment is Key to Economic Growth. There is no Growth without Investment. ……… Therefore, where there is growth, know for sure that, there has been Investment at the place. Conversely where there is no growth it is evident that there has been little or no Investment in that place. For these reasons, if we want growth to happen, one thing that we must ensure is continuous and increased Investment”.

Kwa kifupi tafsiri isiyokuwa rasmi ya Kiswahili anachosema ni kwamba:
Ni ukweli usiopingika kwamba Uwekezaji ni Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi. Kwani Bila Uwekezaji Hakuna Maendeleo yoyote yanayoweza kupatikana na Uchumi hauwezi Kukua. Kwa hiyo, ukiona Uchumi unakua, utambue kuwa kuna Uwekezaji umefanyika mahali hapo. Kinyume cha hapo, ni kwamba mahali pasipokuwa na Maendeleo ni Ushahidi tosha kwamba umefanyika Uwekezaji Kidogo au hakuna kabisa Uwekezaji. Kwa mantiki hiyo, kama tunahitaji Maendeleo na Uchumi wetu Ukue ni lazima kuhakikisha kuwepo na Ongezeko la Uwekezaji na Uwekezaji huo uwe endelevu.

75. Hivyo, suala la Kuvutia Uwekezaji wa Ndani na Nje ni Agenda kubwa ya Serikali. Hii ni kutokana na ukweli kwamba chimbuko la maendeleo katika Nchi zote Duniani limetokana na Uwekezaji uliofanyika katika Nchi hizo. Kwa kuzingatia kuwa Nchi yetu ina Rasilimali nyingi, na fursa kubwa za Kuvutia Uwekezaji. Serikali itaendelea kushirikiana na Wawekezaji wa Ndani na Nje kuwekeza Mitaji ili tutumie kikamilifu Rasilimali zetu tuweze Kupunguza Umaskini, Kuongeza Ajira na Kukuza Uchumi wa Taifa letu. Tukifanya hivyo tutaweza kuwanufaisha Watanzania walio wengi zaidi na Taifa kwa ujumla.

Aidha, katika kuvutia Wawekezaji wa Ndani na Nje tunatarajia kupata Mitaji, Teknolojia Mpya, Rasilimali Watu na fursa za Masoko zitakazotuwezesha Kukuza Uchumi na kuleta maendeleo endelevu.

76. Serikali kwa upande wake itaendelea kuweka mazingira mazuri ya kuvutia Wawekezaji Nchini. Aidha, tutajitahidi kuelimisha Wananchi kuhusu umuhimu na faida za Uwekezaji ili nao washiriki kutumia fursa zilizopo kuwekeza katika maeneo yao na kujiletea maendeleo. Natoa wito kwa Waheshimiwa Wabunge na Wananchi kuunga mkono jitihada hizi za Serikali za Kuvutia Uwekezaji Nchini ili kuongeza Ajira, Kukuza Uchumi na Kuondoa Umaskini.
ZOEZI LA UTOAJI WA VITAMBULISHO

Mheshimiwa Spika,
77. Moja ya mambo makubwa ambayo kwa sasa Serikali inayafanyia kazi ni kutekelezwa kwa Mradi wa Vitambulisho vya Taifa. Mapema mwaka huu, Serikali ilisaini Mkataba na Mkandarasi aliyeshinda Zabuni ya kutengeneza Vitambulisho vya Taifa. Hivyo, kazi kubwa iliyopo mbele yetu kwa sasa ni kutengeneza Mfumo na kuweka Utaratibu mzuri kwa kushirikiana na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa ili Wananchi waweze kusajiliwa na hatimaye kupewa Vitambulisho.

Mheshimiwa Spika,
78. Mradi huu una faida nyingi Kisiasa, Kiuchumi, Kiusalama, Kiulinzi na Kijamii. Zipo faida kubwa ambazo tunaweza kuzitaja kama ifuatavyo:

Kwanza: Uboreshaji Daftari la Wapiga Kura. Iwapo zoezi la kutoa Vitambulisho vya Taifa litakamilika kama ilivyopangwa, Serikali itapunguza gharama zinazotumika katika kuboresha Daftari la Wapiga Kura, kwani tayari kutakuwa na Taarifa za Watanzania wenye Sifa za Kupiga Kura, vivyo hivyo tatizo la kughushi Kadi ya Kupigia Kura, litakwisha kwani Kitambulisho kitaweza kutambulisha uhalali wa mtu kupiga kura au la;
Pili: Kwa kuwa Serikali sasa iko katika maandalizi ya utekelezaji wa zoezi la Sensa litakalofanyika mwezi Agosti 2012 kuwepo kwa Vitambulisho vya Taifa, kutahuisha takwimu za Sensa, kwani mbali ya kujua Idadi, Taifa kupitia Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa litakuwa na Idadi kamili ya Watanzania, shughuli zao na mahitaji yao ya msingi na hivyo kuirahisishia Serikali kazi katika kuweka Mipango yake, vikiwemo vipaumbele vya Huduma za Jamii;

Tatu: Kuiongezea Serikali wigo wa ukusanyaji mapato na hivyo kuboresha huduma muhimu za kijamii kama vile afya, elimu pamoja na ulinzi na usalama wa raia na mali zao; na

Nne: Kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo hivi sasa ni Muungano wa Nchi Tano ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda kumeongeza kwa kiasi kikubwa umuhimu wa kuwa na Vitambulisho. Aidha, kuna makubaliano kwamba Wananchi wa Nchi hizi wawe wanaweza kutembeleana bila ya vikwazo na bughudha kwa kutumia Kitambulisho cha Uraia. Tanzania na Uganda ndizo Nchi pekee katika Jumuiya ambazo hazina Vitambulisho vya Taifa. Hata hivyo tayari Uganda wameshaanza mchakato wa kuwa na Vitambulisho vyao.

Mheshimiwa Spika,
79. Kwa taarifa nilizonazo, Vitambulisho vya kwanza vitatolewa kuanzia mwezi Aprili 2012, wakati wa Maadhimisho ya Sherehe za Muungano. Ombi langu kwenu Waheshimiwa Wabunge, Viongozi wa Vyama vya Siasa na Wananchi kwa jumla ni kuunga mkono jitihada hizi za Serikali na kuelimisha Umma faida za zoezi hili Kiuchumi, Kisiasa na Kijamii. Suala la Kitambulisho cha Taifa halina Chama, wala itikadi. Hivyo, suala hili ni la Taifa zima. Sisi sote tuungane pamoja kuhakikisha kwamba mafanikio ya zoezi hili yanapatikana kwa wakati uliopangwa. Vilevile, niwaombe Watendaji wote, kuanzia Serikali za Mitaa, ngazi za Vijiji, Kata, Wilaya, Mikoa hadi Taifa kuwa Wazalendo katika kuthibitisha nani ni Mtanzania na nani si Mtanzania kwa kutoa taarifa sahihi bila uonevu, kwa kuzingatia misingi ya Haki na Sheria ya Nchi. Napenda kuwaasa Watanzania wote kuwa wakweli wakati wote wa kuandikisha na kutoa Vitambulisho ili kujiepusha na Madhara ya Udanganyifu. Hatua kali zitachukuliwa kwa wale wote watakaobainika kudanganya katika zoezi hili.

MAANDALIZI YA SENSA YA WATU NA MAKAZI YA MWAKA 2012

Mheshimiwa Spika,
80. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itafanya Sensa ya Watu na Makazi mwezi Agosti 2012. Sensa hii itakuwa ya Tano tangu tulipopata Uhuru mwaka 1961. Sensa zilizotangulia zilifanyika mwaka 1967, 1978, 1988 na mwaka 2002. Lengo kubwa la Sensa ya mwaka 2012 ni kuchangia katika uboreshaji wa maisha ya Watanzania kwa kutoa takwimu sahihi na kwa wakati kwa ajili ya kupanga mipango ya maendeleo. Taarifa hizi zitasaidia katika kutathmini na kufuatilia utekelezaji wa mipango na programu za maendeleo kama ifuatavyo:

i) Kutoa Takwimu za Idadi ya Watu, taarifa za Kiuchumi na Kijamii katika ngazi zote za Mipango;

ii) Kutathmini utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025 na ile ya Zanzibar ya mwaka 2020;
iii) Kutumika katika kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania (MKUKUTA) – Tanzania Bara na MKUZA – Tanzania Zanzibar);

iv) Kutumika kutathmini hali ya utekelezaji wa Malengo ya Milenia ifikapo mwaka 2015;

v) Kusaidia Serikali kufanya tathmini juu ya ongezeko la idadi ya watu, makazi yao, shughuli zao na athari zake kwa mazingira ili kuwezesha kuweka Sera na Mipango madhubuti ya uboreshaji wa Makazi ya Watu na utunzaji wa Mazingira na pia kusaidia Mamlaka za Serikali za Mitaa kuainisha mahitaji halisi ya miuondombinu na huduma nyingine za Kijamii kama vile Jiji la Dar es Salaam na Miji mingine; na

vi) Kuimarisha Utawala Bora na ukuaji wa Demokrasia Nchini kwa kutumia Takwimu hizo katika kuamua Mipaka mipya ya Majimbo ya Uchaguzi pamoja na Mipaka mingine ya Kiutawala.

Mheshimiwa Spika,
81. Maandalizi ya Sensa hii yalianza mwaka 2004 kwa kazi ya kutenga maeneo ya kuhesabia Watu yajulikanao kitaalamu kama Enumeration Areas. Lengo kubwa la kazi hii ni kuitenga Nchi nzima katika maeneo madogo madogo ya kuhesabia Watu ili ifikapo mwezi Agosti 2012 Watu wote watakaolala Nchini waweze kuhesabiwa mara moja tu.
Hadi mwezi Oktoba 2011, kazi hii ilikuwa imeshakamilika kwa Asilimia 85 na inategemewa kukamilika mwezi Februari, 2012 kama Ratiba ya Sensa inavyoonesha.

82. Kazi nyingine ambayo imeshakamilika ni Sensa ya Majaribio iliyofanyika mwezi Oktoba, 2011 ambayo ilikuwa na lengo la kutathmini utendaji na muundo mzima wa kuendesha zoezi la Sensa mwakani. Lengo lingine la zoezi hilo lilikuwa kutathmini mtiririko mzima wa Maswali yatakayoulizwa kwa Watu wote watakaolala Nchini usiku wa kuamkia usiku wa Sensa pamoja na Teknolojia ya Kisasa itakayotumika katika uchambuzi wa Takwimu.

Mheshimiwa Spika,
83. Changamoto kubwa tuliyo nayo tangu Serikali ianze maandalizi ya Sensa hii mwaka 2004 ni gharama kubwa itakayotumika kujipanga kuhesabu Watu na kuchukua taarifa zao muhimu zikiwemo taarifa za umri, uraia, elimu, hali ya kazi, uzazi, vifo, hali ya ulemavu na mahali waliposhinda (day population) kwa muda usiopungua siku tatu na hususan katika Miji mikubwa. Serikali imejipanga kutenga Rasilimali Fedha za kutosha na kupata Rasilimali Watu ambao ni Walimu wa Shule za Msingi na Sekondari. Lengo ni kujihakikishia kuwa Wananchi hawapotezi muda mrefu kuwasubiri Makarani wa kuhesabu Watu kuwatembelea katika Kaya zao, hususan katika Jiji la
Dar es Salaam. Serikali itajipanga vizuri kupitia Kamati Kuu ya Sensa ambayo inajumuisha Wizara zote na hususan Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuona namna ya kuweza kuwapata Walimu watakaohitajika.

84. Changamoto nyingine ni kuwepo kwa baadhi ya sehemu Nchini ambazo hazifikiki kwa urahisi, hasa sehemu zenye miinuko mikali, wanyama wakali, visiwa vingi vinavyokaliwa na wavuvi na sehemu zenye Watu wanaohamahama. Juhudi zinafanyika kuandaa namna bora ya kufika sehemu hizo kwa kutumia nyenzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutumia ndege, magari maalum, na vyombo vya kuaminika vya majini.

Mheshimiwa Spika,
85. Nichukue nafasi hii kuwashukuru Wananchi kwa kushirikiana na Serikali katika hatua tuliyofikia ya Maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012. Pia niwaombe tena, kuendelea na ushirikiano huo wa kuhakikisha Sensa ya mwaka 2012 inafanikiwa ili kuiwezesha Serikali kupanga Mipango endelevu ya Maendeleo. Wito wangu kwa Waheshimiwa Wabunge ambao mpo karibu na Wananchi ni kuwaomba kuwaelimisha Wananchi katika Majimbo yenu kuhusu umuhimu wa Sensa ya Watu na Makazi ili waweze kushiriki kwa kikamilifu katika Sensa hii. Aidha,
niwakumbushe Wakuu wa Mikoa na Wilaya kutimiza wajibu wao kama wasimamizi wakuu wa zoezi hili katika Mikoa na Wilaya zao.

UWAZI NA UWAJIBIKAJI KATIKA SERIKALI

Mheshimiwa Spika,
86. Nchi yetu imeridhia kujiunga na Mpango wa Ubia katika Uendeshaji wa Shughuli za Serikali kwa Uwazi yaani “Open Government Partnership”. Mpango huu ambao ni juhudi mpya za Kimataifa katika kuendesha Serikali kwa uwazi na ushirikishwaji mkubwa wa Wananchi, ulizinduliwa rasmi na Viongozi wa Nchi za Marekani, Brazil, Indonesia,
Mexico, Norway, Philippines, Afrika ya Kusini na Uingereza mnamo tarehe 20 Septemba 2011 wakati wa Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa huko New York, Marekani. Msisitizo mkubwa wa Mpango huu ni kuongeza Uwazi na Uwajibikaji katika Serikali, kuwawezesha Wananchi kupata taarifa sahihi na kuzitumia kwa maendeleo yao, Kuzuia na Kupambana na Rushwa na kusisitiza matumizi ya Teknolojia na Ubunifu katika kuimarisha Utawala Bora. Kwa kuwa Serikali ya Awamu ya Nne imeamua kutekeleza kwa uwazi shughuli zake, tumedhamiria kushirikiana na Wadau katika ngazi zote kuhakikisha kwamba habari muhimu za utendaji wa Serikali zinatolewa kwa Wananchi na kuwashirikisha katika kufuatilia na kutoa taarifa katika ngazi husika pale wanapoona utendaji hauridhishi.

Mheshimiwa Spika,
87. Ili kuwa Mwanachama wa Mpango huo, Nchi zinatakiwa kuunga mkono Azimio la Uwazi katika Kuendesha Serikali; kuandaa Mpango Kazi kwa kushirikiana na Wananchi na kuweka utaratibu wa uwazi wa kutoa taarifa za utekelezaji wa Mpango Kazi huo.

Napenda kupitia Bunge lako Tukufu kuwataarifu Waheshimiwa Wabunge pamoja na Watanzania wote kwamba maandalizi ya Mpango Kazi Shirikishi umeanza kwa kushirikisha Wadau mbalimbali. Tayari Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utawala Bora amezungumza na Waandishi wa Habari na kueleza kwa undani kuhusu Mpango huo. Vilevile, tarehe 15 Novemba 2011, Serikali ilikutana na Wadau kutoka Sekta Binafsi na Asasi za Kiraia ambapo kwa pamoja walijadili kwa uwazi aina ya Mpango Kazi wa Kitaifa wanaoutaka na kubainisha maeneo ya kuanzia ili kutekeleza Mpango huo wa Uwazi. Mawasiliano zaidi na Wananchi yataendelea kupitia njia za barua, barua pepe,

simu za mkononi na tovuti ambazo anwani zake zimeshatolewa kwa Wananchi. Nawasihi Wananchi washiriki kikamilifu kutoa maoni yao kwa uwazi ili hatimaye tuwe na Mpango Kazi wa Kitaifa kwa manufaa yetu wote. Nawahakikishia Watanzania kwamba, maoni yenu yataheshimiwa na kuzingatiwa ipasavyo katika Mpango huo.

Mpango wa Kuboresha Lishe

Mheshimiwa Spika,
88. Kama nilivyolielezea Bunge lako Tukufu wakati wa Hotuba yangu ya Bajeti mwezi Juni 2011, Serikali imedhamiria kwa dhati kupambana na tatizo la Lishe Duni hapa Nchini. Katika kutekeleza Azma hiyo, tarehe 20 Septemba 2011, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete aliungana na Viongozi mbalimbali Duniani kujadiliana juu ya kuboresha Lishe hasa kwa Nchi zinazoendelea. Katika Mkutano huo, Viongozi hao walionesha dhamira ya kushirikiana na Serikali yetu ili kuongeza kasi ya kupambana na tatizo la lishe Duni hasa kwa siku 1,000 za kwanza za maendeleo ya Mtoto muda ambao Kitaalam ni muhimu sana katika maendeleo yote ya msingi ya Binadamu. Aidha, tarehe 19 Septemba 2011, nilizindua Mkakati wa Kitaifa wa Lishe ambao utakuwa ndiyo Dira ya kutekeleza shughuli zote za kuboresha Lishe hapa Nchini.
Hivi sasa unaandaliwa Mpango wa Utekelezaji wa Mkakati huo utakaoweka malengo na viashiria vitakavyopimika na kuongoza ufuatiliaji na tathmini.

89. Napenda kuwahakikishia Watanzania wote kwamba, suala la kuboresha Lishe linapewa umuhimu mkubwa na kuanzia Mwaka wa Fedha wa 2012/2013, Kasma maalum ya Lishe itaanzishwa kwenye Bajeti zetu. Nawasihi Wananchi kushirikiana na Serikali katika ngazi zote, ili kukabiliana na tatizo hili la Lishe Duni.

MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA

Mheshimiwa Spika,
90. Kama Waheshimiwa Wabunge na Wananchi wanavyofahamu tarehe 9 Desemba 2011, Taifa letu litahitimisha Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara kwa uzito unaostahili. Maadhimisho hayo yalianza mwezi Juni mwaka huu, ambapo Wizara, Taasisi, Mikoa pamoja na Sekta Binafsi zimekuwa zikifanya Maonesho kwenye maeneo yao na sehemu mbalimbali Nchini kuelezea mafanikio yaliyopatikana, changamoto zilizojitokeza pamoja na matarajio ya Miaka 50 ijayo kwa ajili ya Kumbukumbu ya Vizazi vijavyo. Utaratibu huo unafanyika kwa zamu baina ya Wizara na Mikoa na utaendelea hadi tarehe 30 Novemba 2011. Kuanzia tarehe 1 hadi 9 Desemba 2011, Maonesho hayo yatahamia Uwanja wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Dar es Salaam ambapo Wizara zote, Taasisi pamoja na Wadau wengine watashiriki.

Mheshimiwa Spika,
91. Napenda kutumia fursa hii kwa mara nyingine tena kuwatakia Watanzania wote Kheri na Mafanikio katika Kuadhimisha Sherehe za Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Nawaomba Wananchi kuendelea kutembelea maonesho yanayofanyika kwa sasa katika sehemu mbalimbali Nchini ili kujielimisha juu ya mafanikio tuliyopata katika kipindi cha Miaka 50 ya Uhuru wetu wa Tanzania Bara pamoja na kutambua Changamoto zake. Tutambue kuwa tuna kila sababu kama Taifa kujivunia maendeleo tuliyoyapata kwa Miaka 50 kwa kuwa Tumethubutu, Tumeweza na Tunazidi Kusonga Mbele.

HITIMISHO

Mheshimiwa Spika,
92. Napenda kuhitimisha Hotuba yangu kwa kurejea machache kama ifuatavyo:

Moja: Tunayo kazi kubwa iliyoko mbele yetu ya kuunganisha nguvu kukabiliana na athari za Msukosuko wa Uchumi Duniani kwa kujenga Uchumi tulivu na kuhakikisha kuwa tunadhibiti Mfumuko wa Bei na Kushuka kwa Thamani ya Shilingi. Tushirikiane wote katika kila Nyanja zikiwemo Taasisi zetu za Fedha kwa kutekeleza maelekezo yatakayotusaidia kukabiliana na matatizo hayo;

Pili: Jukumu la Kuandaa Katiba ni letu sote Watanzania bila kujali Kabila, Rangi, Jinsia, Dini ama Itikadi za Kisiasa na Vyama. Kwa hili, Watanzania wote tuungane kulinda Umoja wetu, Amani yetu, Utulivu wetu na Mshikamano wetu uliodumu kwa Miaka 50 ya Uhuru wetu;

Tatu: Tumeanza vizuri katika maandalizi ya Msimu wa Kilimo wa Mwaka 2011/2012. Tuwahimize Wakulima na wote wanaohusika na Upatikanaji na Usambazaji wa Mbolea, Mbegu na Pembejeo kuhakikisha kwamba zinawafikia Wakulima kwa wakati. Tuwahimize Wakulima kutumia Mvua zilizoanza kunyesha katika baadhi ya maeneo Nchini kwa kupanda mapema, kwani “Mvua za Kwanza ni za Kupandia”;

Nne: Tunalo jukumu la kuvutia na kufanya Uwekezaji mkubwa katika Nchi yetu. Nawaomba, tuunganishe nguvu zetu kutangaza fursa zilizopo Kikanda kwa ajili ya Uwekezaji katika maeneo yetu. Kila Mkoa utenge Ardhi kwa ajili ya Uwekezaji na kutangaza fursa zilizopo Kikanda ili kuleta msukumo wa pamoja katika kuvutia Wawekezaji kwenye maeneo hayo;

Tano: Bado tunalo tatizo la Vitendo vya Uhalifu Nchini, ikiwa ni pamoja na Uhamiaji Haramu na uhalifu kwa Watu Wenye Ulemavu wa Ngozi.
Nawaomba Wananchi wote kushirikiana na Vyombo vya Dola kuongeza Nguvu katika kuhakikisha Vitendo hivyo vinakomeshwa;

Sita: Serikali imefikia hatua za mwisho za kukamilisha Zoezi la kuandaa Vitambulisho vya Taifa. Tushirikiane kuwaelimisha Wananchi umuhimu wa suala hili ambalo halina Chama wala Itikadi. Tuungane kuhakikisha kwamba mafanikio ya zoezi hili yanapatikana na kila Mtanzania anapata haki yake kwa kupata Kitambulisho cha Taifa; na

Saba: Maandalizi ya Sensa itakayofanyika mwezi Agosti 2012 yanaendelea. Tushirikiane kuwaelimisha Wananchi kuhusu umuhimu wa zoezi hilo.

Mheshimiwa Spika,
93. Nimalizie kwa kuwashukuru wote waliofanikisha Mkutano huu wa Tano wa Bunge. Nikushukuru kipekee wewe Mheshimiwa Spika, Naibu Spika na Wenyeviti wote kwa kutuongoza vizuri ndani ya Bunge hili. Niwashukuru Waheshimiwa Wabunge kwa michango yenu. Namshukuru Katibu wa Bunge, na Wasaidizi wake kwa huduma mbalimbali ambazo zilifanikisha Mkutano huu. Ninawashukuru Maafisa wote wa Serikali pamoja na Madereva waliotuleta hapa salama na ambao wataturudisha kwenye maeneo yetu ya Makazi na Kazi. Mwisho, lakini siyo kwa umuhimu, ninaushukuru Uongozi wa Mkoa wa Dodoma na Vyombo vya Dola kwa kutuangalia vizuri tangu tulipofika hapa Mkoani. Kwa wote, nasema Asanteni Sana!

Mheshimiwa Spika,
94. Nitumie nafasi hii sasa kuwatakia wote safari njema kurudi katika maeneo yenu ya kazi. Vilevile, niwatakie wote Maadhimisho mema ya Miaka 50 ya Uhuru, Sikukuu Njema ya Krismas na Kheri ya Mwaka Mpya wa 2012.
Ninamwomba Mwenyezi Mungu atufikishe sote salama mwaka 2012 ili tuweze sote kukutana katika Mkutano wa Sita wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mheshimiwa Spika,
95. Baada ya kusema hayo, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu sasa liahirishwe hadi siku ya Jumanne tarehe 7 Februari, 2012, Saa Tatu Asubuhi litakapokutana katika Mkutano wa Sita hapa Mjini Dodoma.

96. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.

MAELEZO YA WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA KATIKA MAJUMUISHO YA MAJADILIANO JUU YA MUSWADA WA SHERIA YA MABADILIKO YA KATIBA WA MWAKA 2011
____________________
Mheshimiwa Spika, kwa mara nyingine nachukua fursa hii kukushukuru wewe kwa kunipa nafasi ya kufanya majumuisho ya mjadala kuhusu Muswada wa Mabadiliko ya Katiba wa mwaka 2011. Muswada huu ambao uliwasilishwa Jumatatu, tarehe 14 Novemba, 2011 umejadiliwa na Waheshimiwa Wabunge wengi bila kujadili itikadi za kisiasa na umewavutia Wabunge wengi.  Huu ni ushahidi kwamba suala la mapitio ya Katiba kwa lengo la kupata Katiba Mpya ni ajenda ambayo kila Mtanzania amekuwa akiisubiri kwa hamu ili kutoa maoni yake.  Sina shaka kwamba baada ya kukamilisha tarehe za kutunga Sheria inayopendekezwa na taratibu za kuunda Tume, Watanzania watashiriki kikamilifu katika mchakato wa kutoa maoni yao kwa Tume.

Mheshimiwa Spika, kwa heshima na taadhima napenda kumshukuru sana Mhe. Pindi Hazara Chana, Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala kwa kutoa hotuba nzuri, kwa niaba ya Kamati, ambayo iliainisha maeneo mengi ya Muswada ambayo yalihitaji kufanyiwa kazi.  Ushahidi wa kazi nzuri ya Kamati ni Jedwali la Marekebisho kwa lugha ya Kiingereza na Kiswahili.  Mtakumbuka vile vile kwamba, kuchapishwa tena kwa Muswada kulitokana na ushauri wa Kamati ambayo iliratibu Vikao vya Wadau, Mjini Dodoma, Jijini Dar es Salaam na Zanzibar.

Mheshimiwa Spika, niruhusu sasa niwatambue Waheshimiwa Wabunge waliochangia hoja kuhusu Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011.  Wabunge hao ni:

WALIOCHANGIA KWA KUONGEA
  1. Mhe. Pindi Hazara Chana  -(Mwenyekiti, Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala)
  2. Mhe. Tundu A.M. Lissu (Waziri Kivuli wa Katiba na Sheria na Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani)
  3. Mhe. Anna Kilango Malecela
  4. Mhe. Dr. Augustino L. Mrema
  5. Mhe. Khalifa Suleiman
  6. Mhe. Christopher Ole-Sendeka
  7. Mhe. Dr. Faustine Engelbert Ndugulile
  8. Mhe. Hamad Rashid
  9. Mhe. Mohamed Mnyaa
  10. Mhe. Moses J. Machali
  11. Mhe. Ismail Aden Rage
  12. Mhe. Felista Bura
  13. Mhe. Ummy Mwalimu (Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto).
  14. Mhe. Angela Jasmine Kairuki (Makamu Mwenyekiti Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala)
  15. Mhe. Yahya Kassim Issa
  16. Mhe. George Boniface Simbachawene
  17. Mhe. Capt. John Komba
  18. Mhe. Esther Amos Bulaya
  19. Mhe. Prof. Anna Tibaijuka (Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi)
  20. Mhe. Augustino Manyanda Masele
  21. Mhe. Eng. Hamad Yussuf Masauni
  22. Mhe. Musa Haji Kombo
  23. Mhe. Betty Eliezer Machangu
  24. Mhe. Subira Khamis Mgalu
  25. Mhe. Dr. Seif Suleiman Rashid
  26. Mhe. Munde Tambwe
  27. Mhe. Richard M. Ndassa
  28. Mhe. Gosbert B. Blandes
  29. Mhe. Agripina Z. Buyogela
  30. Mhe. Stephen Masatu Wasira (Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,      Mahusiano ya Kijamii)
  31. Mhe. Kombo Hamis Kombo
  32. Mhe. Fakeria Khamis Shomari
  33. Mhe. Mwigulu Mchemba
  34. Mhe. Said Mohamed Mtanda
  35. Mhe. Andrew J. Chenge
  36. Mhe. Eng. Stella Manyanya
  37. Mhe. Ali Juma Haji
  38. Mhe. Michael Lekule Laizer
  39. Mhe. Assumpta Shunju Mshama
  40. Mhe. Peter Selukamba
  41. Mhe. Amina Nassor Makilagi
  42. Riziki Omari Juma
  43. Mhe. Sara Msafiri
  44. Jenista Mhagama
  45. Mhe. Menrad Intengard Kigola
  46. Mhe. Suleiman Said Jaffa
  47. Mhe. Mohamed Sanya
  48. Mhe. Dr. William Mgimwa
  49. Mhe. Eugine Mwaiposa
  50. Mhe. Serweji
  51. Mhe. Musa Zungu Azan
  52. Mhe. Abdul Karim Shaa
  53. Mhe. John Paul lwanji
  54. Mhe. Livingstone Lusinde
  55. Mhe. Bernadetha Shashu
  56. Mhe. Anna Abdallah
  57. Mhe. Mch. Luckson Mwanjale
  58. Mhe. Jadi Simai Jadi
  59. Mhe. Herbeth J. Mtangi
  60. Mhe. Jarison Rweikiza
  61. Mhe. Ali Hamis Seifu
  62. Mhe. Rashid Ali Abdalah
  63. Mhe. Clara Mwatuka
  64. Mhe. Silvesta Mabumba
  65. Mhe. Zahra Ali Hamad (Naibu Waziri elimu na Mafunzo ya Amali – Serikali ya Mapinduzi Zanzibar)

WALIOCHANGIA KWA NJIA YA MAANDISHI
  1. Mhe. Catherine V. Magige
  2. Mhe. Fatuma A. Mikidadi
  3. Mhe. Zarina Shamte Madabida
  4. Mhe. Abia Muhama Nyabakari
  5. Mhe. Mohamed H. Misanga
  6. Mhe. Diana Mkumbo Chilolo
  7. Mhe. Pereira A. Silima
  8. Mhe. Nasib Suleiman Omar
  9. Mhe. Dr. William Agustino Mgimwa
  10. Mhe. Benedict Ngalama Ole Nangoro
  11. Mhe. Eng. Athuman R. Mfutakamba
  12. Mhe. Moshi Selemani Kakoso
  13. Mhe. Hussein Mussa Mzee
  14. Mhe. Juma Sururu Juma
  15. Mhe. Ignas Aloyce Malocha
  16. Mhe. Dr. Maua A. daftari
  17. Mhe. Faith M. Mitambo
  18. Mhe. Martha M. Mlata
  19. Mhe. Rukia Kassim Ahmed
  20. Mhe. Augustino M. Masele
  21. Mhe. Rosweeter Kasikila
  22. Mhe. Abdul Rajab Mteketa
  23. Mhe. Kaika Telele
  24. Mhe. Dr. Christopher Gabriel  Ishengoma
  25. Mhe. Jitu Vrallah Soni
  26. Mhe. Amina Mohamed Mwidau
  27. Mhe. Vita R. Kawawa
  28. Mhe. Said R. Bwanamdogo
  29. Mhe. Dr. Hamis Kigwangala
  30. Mhe. Shaffin Sumar
  31. Mhe. Zakia Hamdani Meghji
  32. Mhe. Al-Shymaa Kwegyir
  33. Mhe. Mussa Hassain Mussa
  34. Mhe. Ramadhan Haji Saleh
  35. Mhe. Abdallah Sharia Ameir
  36. Mhe. Innocent E. Kalogeris
  37. Mhe. Kheri K. Ameir
  38. Mhe. Neema Mgaya Hamid
  39. Mhe. Hussein Nassor Amar
  40. Mhe. Nimrod Mkono
  41. Mhe. Mohamoud Hassan Mgimwa
  42. Mhe. Waride Bakari Jabu
  43. Mhe. Clara Diana Mwatuka
  44. Mhe. Brig. Gen. (Mst) Hassan Ngwilizi
  45. Mhe. Stephen Ngonyani
  46. Mhe. Cynthia Hilda Ngoye
  47. Mhe. Desderious John Mipata
  48. Mhe. Riziki Omary Juma
  49. Mhe. John Paul Lwanji
  50. Mhe. Deo Filikunjombe
  51. Mhe. Maida Hamad Abdallah
  52. Mhe. Modestus Kilufi
  53. Mhe. Jasson Rweikiza
  54. Mhe. Eustace Katagira
  55. Mhe. Salome D. Mwambu
  56. Mhe. Sylvester M. Mabumba
  57. Mhe. Albert Obama Ntabaliba
  58. Mhe. Ali Hamis Seif
  59. Mhe. Lolesia J. M. Bukwimba
  60. Mhe. Amos Makalla
  61. Mhe. Anastazia Wambura
  62. Mhe. Masoud Abdallah Salim
  63. Mhe. Agnes Hokororo
  64. Mhe. Haroub M. Shamis
  65. Mhe. Aliko Kibena
  66. Mhe. Said Mussa Zubeir
  67. Mhe. Margeret Semwanza Sitta
  68. Mhe. Deogratias Ntukamazina
  69. Mhe. Nyambari Chacha Nyangwine
  70. Mhe. Shawana Bukheti Hassan
  71. Mhe. Dr. Fenella Mukangara (Naibu Waziri Habari,

Utamaduni, Michezo na Vijana)

  1. Mhe. Ritta E. Kabati
  2. Mhe. Maida Hamad Abdallah
  3. Mhe. Mariam Nassoro Kisangi
  4. Mhe. Godfrey Weston Zambi.

Napenda kuwashukuru wadau mbalimbali ambao wametoa maoni ya kuboresha Muswada huu.  Hao ni wafuatao:-

  1. Tanzania Centre for Democracy kwa barua yao ya tarehe 2/6/2011 mapendekezo yao mengi tumeyazingatia.
  2. Chama cha majaji wastaafu.
  3. Jukwaa la Katiba Tanzania.
  4. Wananchi mmoja mmoja n.k.
  5. Tanganyika Law Society.

Mheshimiwa Spika, idadi kubwa ya Waheshimiwa Wabunge waliochangia hoja hii, ni ushahidi tosha kwamba pamekuwapo maoni na ushauri wa kutosha katika kuuboresha Muswada huu. Kama nilivyosema awali, mjadala umevuka mipaka ya itikadi ya vyama vya siasa.  Vyama karibu vyote vilivyo na Wabunge ndani ya Bunge hili, ikiwa ni Chama cha Mapinduzi, Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Chama cha CUF, Chama cha NCCR – MAGEUZI na Chama cha T.L.P. vimeshiriki kujadili na kuuboresha Muswada huu. Michango ya Wabunge wengi iliipongeza Serikali kwa kuwasilisha Muswada wa Sheria ambao utaiwezesha nchi yetu kupata Sheria ambayo itatuongoza katika safari ya kupata Katiba Mpya.  Michango mingi ilirejea vifungu mbalimbali ambavyo tayari Serikali ilikwishavifanyia kazi kutokana na ushauri wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala. Na, kama alivyoeleza Mwanasheria Mkuu wa Serikali, michango yenye lengo la kuboresha zaidi Muswada, kutoka kwa Waheshimiwa Zarina Madabida (Viti Maalum), Godfrey Weston Zambi, (Mbozi Mashariki), Mhe. Christopher Ole Sendeka (Simanjiro), Mohamed Habib Juma Mnyaa (Mkanyageni), Dr. Faustine Engelbert Ndugulile (Kigamboni) Mussa Hassan Zungu (Ilala), Jasson Rweikiza (Bukoba Vijijini) yamefanyiwa kazi katika Jedwali la Nyongeza ambalo Waheshimiwa Wabunge mmegawiwa. Kwa mara nyingine nawashukuru kwa ushauri wenu.

Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo ya jumla, sasa napenda kutoa maelezo kuhusu maeneo mahususi yaliyojadiliwa na Wabunge.  Nitafanya hivyo kwa kuzipanga Hoja katika makundi (cluster).

KUUNDWA KWA TUME

Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani, Mhe. Tundu Lissu, alishauri kwamba:

  1. Muswada huu mpya una tofauti kubwa za kimsingi na Muswada wa zamani.
Mheshimiwa Spika, maudhui na muundo wa Muswada huu hauna tofauti yoyote na Muswada wa mwanzo na  hivyo, mpya kama inavyodaiwa na Mhe. Tundu Lissu.  Maudhui ya Muswada huu ni:

  1. kuunda Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya ili iratibu na kukusanya maoni ya wananchi juu ya Katiba;
  2. kuainisha na kuchambua maoni ya wananchi;
  3. kuainisha masharti kuhusu mabaraza ya kuhalalisha masharti yaliyomo kwenye Rasimu ya Katiba;
  4. kuweka masharti ya utayarishaji wa uwasilishaji wa ripoti kuhusu maoni ya wananchi;
  5. kuweka utaratibu wa kuunda Bunge Maalum; Bunge la Katiba.
  6. kuweka masharti ya uendeshaji wa kura ya maoni. Hivyo maudhui hayajabadilika.

Aidha, Muswada huu una sehemu tano pamoja na majedwali.  Maudhui na muundo wa Muswada wa mwanzo viliboreshwa zaidi kutokana na maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala pamoja na wadau mbalimbali.

  1. Mapendekezo ya Muswada kuhusu uteuzi wa wajumbe, watendaji na watumishi wengine wa Tume yana lengo la kuhakikisha kwamba matokeo ya kazi ya Tume ni yale tu yanayotakiwa na Rais na Serikali yake na chama chake cha CCM (Uk 10)

Hoja hii haina msingi wowote.  Uteuzi wa wajumbe watendaji na watumishi wengine wa Tume unafanyika kwa kuzingatia Katiba iliyopo sasa na sheria za nchi.  Mfumo wa Serikali tuliyonayo unampa Rais ambae ni Kiongozi wa Serikali, Mkuu wa Nchi na Amiri Jeshi Mkuu mamlaka hayo.  Aidha, kwa kuwa Rais wetu amechaguliwa na wananchi anao uhalali wa kusimamia mchakato huu kwa kuteua Tume.  Izingatiwe hapa kwamba Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni mojawapo ya Mambo ya Muungano.  Kwa mujibu wa Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 mamlaka yote ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano juu ya Mambo yote ya Muungano yamo mikononi mwa Rais wa Jamhuri ya Muungano.  Kwa hiyo hakuna namna ambayo mchakato wa kutunga Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania utamweka pembeni Rais Mkuu wa Nchi.  Kwa vyovyote vile iwayo Mamlaka ya Rais yaliyomo katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano, hayawezi kuondolewa na Sheria ya kawaida kama hii.

  1. Badala ya Tume hiyo kuwa “Tume ya Rais” iwe “Tume ya Vyama” (Multiparty Commission) kwa maana kwamba wajumbe wa Tume wateuliwe kufuatana na mapendekezo na makubaliano ya Vyama vya Siasa vyenye uwakilishi Bungeni, vyama vingine vilivyosajiliwa, mashirika ya kijamii, taasisi za kitaaluma na kidini.
Hoja hii imejibiwa kwa kirefu na Mh. Mwanasheria Mkuu wa Serikali.  Ni kweli kuwa Tume ya Vyama iliyopendekezwa na Mhe. Lissu ni moja ya njia zinazotumika kupata Katiba.  Hata hivyo, njia hiyo hutumika mara nyingi pale nchi inapokuwa imetoka katika vita au machafuko kwa madhumuni ya kuleta mardhiano.  Mazingira yetu ni tofauti.  Tumeamua kwa hiari yetu kuingia kwenye mchakato wa kupata Katiba Mpya nchi yetu ikiwa na amani na utulivu.  Aidha, ni vyema tu kafahamu kuwa, moja ya matatizo ya Tume ya vyama ni kila chama kutaka maslahi yake kuzingatiwa na kwa jinsi hiyo mchakato kutokuwa huru kama inavyotakiwa.  Hivyo, Serikali iliona busara kutumia njia ya Tume inayopendekezwa kwenye Muswada ambayo itajumuisha wajumbe wa aina tofauti ili kusaidia kupata maoni ya wananchi wote bila kujali itikadi zao za kisiasa.

  1. Tume ya Vyama itakuwa na uhalali wa kisiasa (political legitimacy) mkubwa zaidi kuliko Tume ya Rais.

Hoja hii pia haina msingi kwa kuwa Rais aliyechaguliwa na wananchi ana uhalali zaidi kuliko chama kimoja kimoja.

  1. Mapendekezo ya ibara ya 10 ya Muswada kuhusu uhuru wa Tume hayatoshelezi hata kidogo na kwamba wajumbe wapatiwe ulinzi wa ajira zao sawa na wanaopatiwa Majaji wa Mahakama ya Tanzania ili kuzuia uwezekano wa wajumbe kuondolewa kwa sababu zisizotokana na utendaji wao wa kitaaluma au ukosefu wa maadili.
Mchakato huu ni wa muda na kazi ya Tume siyo ya kudumu ni ya muda , aidha wajumbe wa Tume ni wateule wa Rais ambao atawateua kwa kuzingatia uadilifu wao hivyo hakuna haja ya kuwekewa ulinzi.  Kazi ya Tume ni dhamana tu ya kutekeleza majukumu na si ajira.

MAMLAKA YA RAIS

Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani, Mhe. Tundu Lissu, alishauri kwamba:

  1. Mfumo wetu wa kikatiba umejengwa juu ya nguzo kuu ya urais wa kifalme, kwa vile Rais, katika mfumo huu ana mamlaka makubwa.

Wabunge wengi wamenisaidia sana kutoa maelezo ya hoja hii na watanzania wamewaelewa.  Si kweli kwamba mfumo wa utawala wa nchi yetu ni wa kifalme.  Mheshimiwa Lissu amepotosha ukweli kuhusu jambo hili.  Nchi yetu inafuata mfumo wa Kirais kwa maana kwamba kwa mujibu wa Ibara ya 33(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano, Rais wa nchi yetu ni Kiongozi wa Serikali, Mkuu wa nchi na Amiri Jeshi Mkuu.  Aidha, ibara ya 40(2) ya Katiba inaweka ukomo wa vipindi viwili vya mtu kuwa Rais.  Namshangaa Mhe. Mwenzangu, msomi hayo anayatoa wapi?

  1. Muswada unaendeleza kivuli kirefu cha Urais wa kifalme katika mchakato wa upatikanaji wa Katiba Mpya.
Mhe. Lissu labda ana ajenda, nyingine lakini mtanzania yoyote anajua maana ya Muswada huu kwa sasa na si upotoshaji anaoufanya kusema kwamba Muswada huu unaendeleza urais wa kifalme. Watanzania wenzangu Muswada unaweka utaratibu wa kutunga Katiba Mpya kwa kuweka utaratibu utakaowawezesha wananchi kutoa maoni yao.

  1. Watu watakaoteuliwa na Rais kuunda Tume ni watu wasiokuwa tishio kwa status quo.
Hizi ni hisia tu na hazina msingi wowote kwa sababu Rais amewekewa vigezo vya aina ya watu ambao atapaswa kuwateua (angalia Ibara ya 6(3) ya Muswada).

  1. Wajumbe wanaoteuliwa na Rais wanakuwa na shinikizo la kutoa matokeo yatakayompendezesha Rais au chama chake.
Hii ni hofu isiyokuwa namsingi wowote. Jukumu la Tume litakuwa ni kuratibu na kukusanya maoni tu. Muswada umeweka mabaraza, Bunge Maalum na utaratibu wa kura ya maoni.  Vyombo hivi vyote vitakuwa na uwezo wa kuchambua na kuunga au kutokuunga mkono yale yatakayokuwa yamewekwa katika Katiba inayopendekezwa.

  1. Mamlaka ya uteuzi wa Tume yaondolewe katika mikono ya Rais.
Mamlaka hayo ya uteuzi  hayapaswi  kuondolewa kwa Rais.

  1. Kwa kuzingatia mapendekezo ya ibara ya 9 ya Muswada, haijulikani Rais atatoa maelekezo gani ya ziada yanayohusu kazi za Tume na namna ya kuzitekeleza.
Ibara ya 9 haimpi Rais mamlaka yoyote ya kutoa maelekezo ya ziada.

  1. Ibara ya 26(2) ya Muswada inayompa Rais mamlaka ya kuitisha tena Bunge la Katiba inaweza kutumiwa kama njia ya kufanya marekebisho kwenye mambo yaliyo kwenye Katiba Mpya ambayo Rais au Serikali yake au chama chake hawayapendi, kabla ya kupigiwa kura maoni na wananchi.
Si kweli kwamba Ibara hiyo imewekwa kwa madhumuni ya kumpa fursa Rais uwezo wa kufanya marekebisho kwa maslahi yake au chama chake. Ibara hii imewekwa ili kulipa Bunge Maalum fursa ya kuboresha zaidi Katiba inayopendekezwa.  Kama mambo ya msingi yanayohitaji kufanyiwa kazi.

HADIDU ZA REJEA

Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani, ameshauri kuwa Rais asipewe mamlaka ya kutoa Hadidu za Rejea Tume na kwamba:

  1. Hadidu za rejea ni muhimu ziwekwe wazi katika Sheria yenyewe badala ya kuwa siri ya Rais.

Hoja hii imeshafanyiwa kazi.  Laiti Mheshimiwa Tundu Lissu angehudhuria vikao vya Kamati ya Kudumu ya Katiba, Sheria na Utawala vilivyofanyika Dar es Salaam na hapa Dodoma angefahamu kuwa Serikali imeafiki Hadidu za Rejea kwa sehemu ya Muswada na kwa mujibu wa Marekebisho hayo Hadidu za Rejea ziko katika ibara za 9 na 16.

  1. Mapendekezo ya ibara ya 8 yanaweza kuleta mkanganyiko na mgogoro wa kisiasa na kisheria usiokuwa na lazima endapo Rais atatoa hadidu za rejea zinazotofautiana na matakwa ya kisheria kama yanavyopendekezwa na ibara ya 9 ya Muswada mpya.
Ibara ya 8 imerekebishwa hili limeshashughulikiwa na kwa kuwa Hadidu za Rejea ni sehemu ya Muswada hakuna kwa mgongano utakaotokea.

  1. Ibara ya 8 ifutwe yote na ibara za 9 na 16 zifafanuliwe vizuri ili kuweka wazi zaidi hadidu za rejea za Tume na namna ya kuzitekeleza.

Jedwali la Marekebisho lilifuta ibara hiyo ya 8 na kuiandika upya kama inavyoonekana katika Jedwali la Marekebisho.

MISINGI MIKUU YA KITAIFA

Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani, alishauri kwamba izungumzwe bila mipaka.  Suala si kuendeleza na kuidumisha tu inakinzana na Ibara ya 98(1)(b) ambayo inaruhusu masuala yaliyopo katika Orodha ya Pili kwenye Nyongeza ya Pili ya Katiba.  Aliendelea kueleza kwamba:

  1. Ibara ya 9(3) ya Muswada linaelekeza kwamba “misingi mikuu ya kitaifa” izungumzwe kwa lengo la kuiendeleza na kuidumisha tu, inakinzana na ibara ya 98(1) (b) ya Katiba ya sasa na pia inazuia kuhoji na/au kupinga mambo ambayo kwa Katiba ya sasa ni ruhusa kuyahoji, kuyapinga na/au hata kuyabadilisha.
  1. Ibara ya 9(2) na (3) ya Muswada zifutwe kabisa ili kuwepo na uhuru kamili wa kujadili, kwa kupinga au kuunga mkono, kila jambo linalohusika na katiba mpya.
Misingi hii ni ya kihistoria na imejengeka kwa muda mrefu.  Ni vema kuienzi.  Kwa maana hiyo, Ibara ya 9(2)(3) hazipaswi kufutwa kwa kuwa zinatoa mwongozo kwa Tume kuzingatia misingi  Mikuu ya Kitaifa na maadili.  Aidha, Tume inaelekezwa kutoa fursa kwa wananchi kujadili na kuboresha masuala hayo.  Katika hali hiyo Ibara hii haikinzani na Ibara 98(1)(b) ya Katiba kwani katika kujadili kuboresha mambo hayo marekebisho yanaweza kufanywa.

UWAKILISHI WA ZANZIBAR

Maelezo yametolewa kwamba:

  1. Ibara za 5, 6(1), 8(1) na (2), 13(2), 18(1) na (2) zinaainisha kwamba utekelezaji wa mamlaka yote ya Rais, Waziri na Mwanasheria Mkuu wa Jamhuri ya Muungano lazima ufanyike kwa “mashauriano na makubaliano” na Rais, Waziri au Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar.  Aidha, kwamba kwa mujibu wa ibara ya 18(1) na (2), mapendekezo hayo yanamfanya Rais wa Zanzibar sio tu kwamba ana mamlaka karibu sawa na Rais wa Jamhuri ya Muungano, bali pia ana kura ya turufu katika mchakato wa Katiba Mpya.

Kwa kuwa suala hili ni la muungano pande zote mbili za muungano huu inapaswa kupewa fursa sawa au kupewa uwiano unaokubalika katika kufanya uamuzi.  Kwa kufanya hivyo ina maana kwamba pande hizi mbili za muungano zina fursa sawa.  Hatua hiyo haimpatii Rais wa Zanzibar Kura ya Turufu bali kwa moja wa viongozi wetu wakuu wahusika wa mchakato huu.

  1. Rais wa Zanzibar asipopatiwa nakala ya ripoti ya Tume au asipokubaliana na Rais wa Jamhuri ya Muungano, basi Muswada wa Katiba hautawasilishwa kwenye Bunge la Katiba.
Hoja hii inapotosha ukweli.  Katika mchakato huu jambo kubwa la kuzingatia ni uaminifu.  Marais wetu ambao wamechaguliwa na wananchi wanajua dhamana kubwa waliyonayo mbele ya Watanzania.  Haitegemewi mazingira anayoyaeleza Mhe. Lissu kutokea.

  1. Mapendekezo ya Muswada yanayomfanya Rais wa Zanzibar kuwa mshiriki sawa na mwamuzi wa mustakabali wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano yanaenda kinyume na Katiba ya sasa na Hati za Muungano.  

Huu ni upotoshaji.  Kwa kuwa suala hili ni la muungano ushiriki sawa wa Rais wa Zanzibar katika uamuzi juu ya Katiba ni muhimu kwa kuzingatia kwamba muungano huu umetokana na mapatano ya nchi hizi mbili.

  1. Ibara ya 6(2) ya Muswada ambayo inaelekeza uwakilishi ulio sawa kwa wajumbe wa Tume na Sekretarieti haina mantiki kwa vile Katiba Mpya itahusu Mambo ya Muungano ambayo ni halali kwa Zanzibar kushirikishwa kwa usawa kabisa, na vile vile masuala yasiyo ya Muungano ambayo Zanzibar haina haki ya kushiriki.
Usawa wa uwakilishi katika Tume na Sekretarieti kati ya pande hizi mbili za muungano unatokana na ukweli kwamba suala lenyewe ni la muungano.

RAIS WA ZANZIBAR

Zimetolewa hoja tatu na Mhe. Tundu Lissu kwamba:

  1. Ibara za 5, 6(1), 8(1) na (2), 13(2), 18(1) na (2) zinaainisha kwamba utekelezaji wa mamlaka yote ya Rais, Waziri na Mwanasheria Mkuu wa Jamhuri ya Muungano lazima ufanyike kwa “mashauriano na makubaliano” na Rais, Waziri au Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar.  Aidha, kwamba kwa mujibu wa ibara ya 18(1) na (2), mapendekezo hayo yanamfanya Rais wa Zanzibar sio tu kwamba ana mamlaka karibu sawa na Rais wa Jamhuri ya Muungano, bali pia ana kura ya turufu katika mchakato wa Katiba Mpya.
  1. Rais wa Zanzibar asipopatiwa nakala ya ripoti ya Tume au asipokubaliana na Rais wa Jamhuri ya Muungano, basi Muswada wa Katiba hautawasilishwa kwenye Bunge la Katiba.
  1. Mapendekezo ya Muswada yanayomfanya Rais wa Zanzibar kuwa mshiriki sawa na mwamuzi wa mustakabali wa Katiba ya
Jamhuri ya Muungano yanaenda kinyume na Katiba ya sasa na Hati za Muungano.

Msingi wa makubaliano kati ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika kila hatua ya mchakato wa kupata Katiba Mpya unatokana na Hati ya Muuungano (The Articles of Union).  Hati hiyo ya Muungano iliyosainiwa tarehe 21 Aprili, 1964 inaonyesha mambo ambayo Waasisi wa Muungano wetu walikubaliana.  Aya ya (vii ya Hati hiyo inaelekeza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akubaliane na Makamu wa Rais ambaye ni Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (sasa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar) kuunda Tume ya kupendekeza Katiba ya Jamhuri ya Muungano na Bunge Maalum.  Naomba kuinukuu aya hiyo.

  “(vii) The President of the United Republic: in agreement with the Vice-President who is the head of the Executive in Zanzibar shall-

  1. Appoint a commission to make proposals for a Constitution for the United Republic;
  2. Summon a Constituent Assembly … for purposes of considering the proposal of the commission …”
Kwa kuzingatia kuwa tunaunda Katiba Mpya ya kuiongoza Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hatuna budi kufuata sharti linalohitaji Marais wa Serikali zetu mbili kukubaliana kama ulivyowekwa kwenye Hati ya Muungano.  Kwa mantiki hiyo hoja ya Mhe. Tundu Lissu haina msingi.

UHALALISHAJI WA KATIBA MPYA

Imependekezwa kwamba:

  1. Pendekezo kwamba Serikali ilete Sheria mahsusi ya kusimamia Uchaguzi wa Kura ya Maoni badala ya uchaguzi huo kuwa chini ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar.

Serikali imepokea ushauri huo na kuukubali.  Sheria hiyo itatungwa na kuletwa ndani ya Bunge hili ili ujadiliwe kuwa sheria.  Baada ya hapo vifungu vya Katiba vitarekebishwa ili sheria hiyo itumike wakati wa kura ya maoni.

  1. Iwapo wingi wa kura ya maoni ni HAPANA, Katiba ya sasa isitumike badala yake mchakato wa Katiba Mpya uanze tena hadi hapo utakapopatikana muafaka wa kitaifa wa Katiba.
Ibara ya 34(3) inaeleza kuwa Sheria tutakayoitunga leo itamalizika matumizi yake baada ya Katiba Mpya kuzinduliwa.  Kutopatikana kwa wingi wa kura za kupitisha Katiba inayopendekezwa haitazuia mchakato wa Katiba kuendelea kufanyika.  Na katika hali hiyo Katiba ya Jamhuri ya mwaka 1977 lazima iendelee kutumika.  Hata Mhe. Lissu amesita kueleza Katiba ambayo itaweza kutumia na jinsi nchi itakavyoongozwa endapo Katiba Mpya haitapitishwa.

Mheshimiwa Spika, kwa mara nyingine tena naomba nikushukuru wewe, Mheshimiwa Waziri Mkuu,  Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala pamoja na Waheshimiwa Wabunge wote kwa namna ambavyo mmechangia katika kukamilisha kazi hii muhimu.

Mheshimiwa spika, naomba kuwasilisha.

MAELEZO YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI AKICHANGIA MJADALA KUHUSU MUSWADA WA SHERIA YA MABADILIKO YA KATIBA WA MWAKA 2011
___________________  
UTANGULIZI
Mheshimiwa Spika, Nakushukuru sasa kwa kunipatia fursa hii ili niweze kuchangia hoja hii ya Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa mwaka 2011.  Nianze kwa kumshukuru Mhe. Waziri Celina Kombani; Naibu Mwanasheria Mkuu, Mwandishi Mkuu wa Sheria; maafisa Waandishi wa Sheria; Makatibu Muhtasi, Makarani na Madreva wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu na Wizara ya Katiba na Sheria.

Kwa aina ya pekee, niwashukuru sana  viongozi wetu, Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete; Makamu wa Rais, Mhe. Dr Mohamed Gharib Bilal; Rais wa Zanzibar, Dr Ali Mohamed Shein;  Mhe. Anna Makinda, Spika kwa uongozi wao katika jambo hili.  Aidha, ninawashukuru sana Mhe. Othman Masoud, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Zanzibar na Wasaidizi wake kwa mchango na ushirikiano wao katika kuuboresha Muswada huu na kusaidia katika kuuandika kwa lugha ya Kiswahili sanifu.

Mambo ya kufafanua:

Muswada huu umechapishwa upya.  Umetafsiriwa katika lugha ya Kiswahili.  Lugha zote mbili zinatumika.  Hata hivyo, Muswada ulio Bungeni ni ule unaosomeka kwa lugha ya kiingereza.  Huo ndio unaofanyiwa rejea ndio ulioletwa na ndio uliotafsiriwa.

Muswada umefanyiwa marekebisho yanayotokana na maoni ya Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala; maoni ya Wadau, Majukwa; Makongamano; barua za wasomaji; na kwa njia nyingine zozote.

Mheshimiwa Spika, Muswada huu umechangiwa na Wabunge wasiopungua 64.  Wengine kati yao wameuliza maswali na kutaka ufafanuzi wa mambo waliyooona hayaeleweki;  wengine wamezungumzia utaratibu ambao wao wanafikiria ungefuatwa katika kushughulikia Muswada huu; wengine wametoa mapendekezo ya kuuboresha Muswada; wengine wametoa tahadhari kwa maono yao.  Mambo yote hayo, ni mambo ya kuzungumzika ingawa muda wa kufanya hivyo hautoshi.

Mheshimwia Spika, jambo moja kubwa lililojitokeza, ni madaraka ya Rais ya kuwateua Wajumbe wa Tume ya Kuratibu Maoni ya Wananchi; na mamlaka yake ya kutengeneza Hadidu za Rejea yaani Terms of Reference.  Ibara ya (5)(6)(8) zinahusika.  Jedwali la Nyongeza limekifanyia marekebisho kifungu hicho.  Wabunge wengi wamelizungumzia kwa ufasaha.  liliibuliwa na maoni ya Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani ni kwamba Muswada huu ungesomwa Mara ya Kwanza.  Kama ulivyofafanua, na kama Mheshimiwa Waziri wa Katiba na Sheria; pia Mhe. George Boniface Simbachawene, (Mb.), Mhe. Andrew John Chenge (Mb.), wamefafanua.  Muswada huu ulikwisha somwa Mara ya Kwanza.  Bunge lako linaongozwa na Kanuni.  Kamati ya Kudumu ya Katiba, Sheria na Utawala iliyokuwa ikiushughulikia Muswada huu ilitoa taarifa ya kumaliza kuujadili Muswada kwa mujibu wa Kanuni 85(1).  Baada ya taarifa hiyo, Muswada ulipangwa katika shughuli za Bunge na kwa kufuata masharti ya Kanuni ya 86(2), Waziri aliuwasilisha. Maneno ya kukejeli yaliyotolewa dhidi ya Spika kwamba aliingilia kazi ya Kamati yanasikitisha.  Kamati haikulalamika kuhusu jambo hili.  Nilipokwenda kwenye Kamati niliwaona na kuwashuhudia Wajumbe wa kamati wa CHADEMA wanashiriki vizuri tu.  Ninakubalina na angalizo la Prof. Anna Kajumlo Tibaijuka (Mb.) wakati alipokuwa anachangia alisema “Tuache propaganda.  Muswada umeboreshwa.

Inashangaza ni Muswada huu tu ndiyo unadaiwa Usomwe mara ya Kwanza mara Mbili.  Kwa mfano Muswada wa Sheria ya Ununuzi wa Umma uliopitishwa Jumatatu tarehe 14 Novemba, 2011, na mwaka jana, Muswada wa Sheria ya Gharama za Uchaguzi, yote ilichapishwa tena lakini suala la kurudia Kusomwa kwa mara ya Kwanza halikujitokeza “Muswada Kusomwa Mara ya Kwanza” ni kitendo kinachoashiria kuanza kwa hatua za kibunge za kujadili na kupitisha au kuukataa Muswada wa Sheria.  Muswada ukipelekwa kwa Spika, naye Spika akiupeleka kwenye Kamati, mantiki ni kwamba marekebisho yanatarajiwa katika Muswada.  Wingi au uchache wa marekebisho haubadili Kanuni ya 83, 84 na 85 za Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la 2007.

UAMUZI WA THELUTHI MBILI MAALUM
Mheshimiwa Spika, Wabunge wengi walichangia kuwa Bunge Maalum liko juu ya Katiba na hivyo liachiwe litunge masharti na kanuni zake katika kupitisha Katiba inayopendekezwa na siyo kama ilivyo katika Ibara ya 24(3) ya Muswada.

Jambo hili linahusu masuala makuu matatu:

Mheshimiwa Spika, Suala la kwanza ni masharti ya Kikatiba.  Ibara ya  4(3) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano inaainisha uwepo wa mambo ya muungano.  Aidha, Nyongeza ya Kwanza katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania inaainisha mambo ya muungano ambapo jambo la kwanza katika nyongeza hiyo ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ibara ya 98 ya Katiba inaweka masharti ya wingi wa kura wa theluthi mbili ya kila upande wa muungano katika kufanya marekebisho ya jambo lolote la muungano.  Kwa kuwa masharti ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano bado yana nguvu kisheria sharti hili la Katiba haliwezi kukiukwa.

Mheshimiwa Spika, Suala la pili linahusu Jambo Kuu la Msingi.  Kwa mujibu wa taratibu za kisheria, mambo yote ya msingi katika kufanikisha utekelezaji wa sheria husika yanawekwa ndani ya Sheria husika na sio katika Kanuni.  Suala la kupitisha uamuzi kwa theluthi mbili kwa kila upande ni la msingi hivyo linastahili kuwekwa kama sharti katika Sheria badala ya Kanuni.  Utaratibu wa maamuzi katika suala lolote ni jambo la msingi. Kwa msingi huo ndio maana utaratibu wa marekebisho wa mambo ya muungano yaliyoainishwa katika Katiba umewekwa ndani ya Katiba yenyewe na sio ndani ya sheria nyengine.

Kwa kuwa, suala la utaratibu wa maamuzi ni suala la msingi na limeshawekewa utaratibu haliwezi kuwekwa ndani ya Kanuni za Bunge Maalum.

Mheshimiwa Spika, Suala la tatu ni Makubaliano ya Pande mbili za Muungano.  Miongoni mwa mambo yaliyoleta mjadala mkubwa katika muswada wa awali wa sheria hii, ni suala la utaratibu katika hatua za maamuzi.  Baada ya majadiliano baina ya Serikali zote mbili, ilikubaliwa kwamba utaratibu ulioainishwa ndani ya Katiba ndio unaopaswa kuainishwa ndani ya sheria ya Mabadiliko ya Katiba.

Mheshimiwa Spika, Kutokana na sababu hizo, Serikali inaona ni sahihi utaratibu huo wa maamuzi kuainishwa ndani ya sheria ya Marekebisho ya Katiba na sio kuwekwa katika Kanuni za Bunge.

IBARA YA 98 YA KATIBA
Mheshimiwa Spika, Katika majadiliano ya Muswada wa Kutunga Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, imeibuka hoja kuhusu uhalali wa kutungwa kwa sheria hiyo. Kwa mujibu wa hoja hiyo, ili mchakato wa kutunga Katiba uweze kuwa halali ni lazima kwanza Ibara ya 98 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ifanyiwe marekebisho kwa kuongeza Ibara ndogo ya tatu ili kuruhusu kutungwa kwa sheria hiyo. Hoja hiyo haina msingi wowote wa Kikatiba au Sheria kwa sababu za msingi zifuatazo:

Tangu ulipopatikana uhuru wa Tanganyika mwaka 1961, nchi yetu imewahi kutunga katiba mara tano yaani Katiba ya Uhuru wa Tanganyika ya mwaka 1961; Katiba ya Jamhuri ya Tanganyika ya mwaka 1962; Katiba ya Muda ya Mwaka 1964, (ambayo  ni kwa mujibu wa Mapatano ya Muungano) ilielekeza kwamba Katiba ya Jamhuri Tanganyika ya mwaka 1962, pamoja na marekebisho yaliyotajwa katika Mapatano ya Muungano, itumike kama Katiba ya Muda; Katiba ya Muda ya mwaka 1965 na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Kwa upande wa Zanzibar, kumekuwepo Katiba ya Uhuru ya mwaka 1963, Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1979, na Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984. Katika uandishi wa Katiba zote hizo, hayajawahi kufanyika marekebisho au mabadiliko yoyote ndani ya Katiba hizo ili kuhalalisha kuandikwa kwa  Katiba Mpya.

Katika kutunga Katiba ya Jamhuri ya Tanganyika ya mwaka 1962, iliundwa Tume iliyoteuliwa na Rais ambayo ilisimamia mchakato mzima wa kupata Katiba ya nchi hadi ilipopitishwa na Bunge. Katiba za  Muda za Muungano na kutungwa kwa Katiba ya Kudumu, yaani, Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977, vilitokana na Mapatano ya Muungano kati ya Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ya mwaka 1964. Mapatano hayo, kupitia Sheria ya Bunge
  The Union of Tanganyika and Zanzibar Act,  No. 22 of 1964 ambayo, pamoja na mambo mengine iliweka masharti ya kuundwa kwa Tume ya kuratibu maoni ya wananchi na kuundwa Bunge la Katiba lililowezesha kutungwa kwa Katiba ya Mwaka 1977.

Katika Mabadiliko ya Tano ya Katiba, karibu kila Ibara iliyokuwemo katika Toleo la Mwaka 1977, ilibadilishwa na kuipatia Katiba hiyo sura mpya. Lakini, kwa kuwa mabadiliko hayo yalifanyika chini ya Ibara ya 98, hatukuwa na Katiba Mpya. Ibara hiyo inaruhusu Bunge kubadilisha Katiba lakini Bunge halina mamlaka ya kuifuta Katiba. Hata hivyo, Bunge linayo mamlaka ya kuweka utaratibu utakaowezesha kuwepo kwa Bunge la Katiba. Kwa upande wa Zanzibar ilipata Katiba mwaka 1979 kupitia Amri ya Kikatiba (Constitutional Decree) iliyopitishwa na Baraza la Mapinduzi. Aidha, Katiba ya mwaka 1984 ilipitishwa na Baraza la Wawakilishi kupitia mchakato ambao haukuainishwa katika Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1979.

Uamuzi wa Mahakama
Hoja kuhusu uhalali wa mchakato wa katiba mpya bila ya kubadilisha masharti ya Katiba iliyopo, lilijitokeza pia katika mchakato wa kupata Katiba mpya ya Jamhuri ya Kenya ya mwaka 2010.  Baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuwasilisha Muswada wa Sheria ya Kutungwa kwa Katiba Mpya na kupitishwa na Bunge, baadhi ya wananchi wa Kenya waliipinga sheria hiyo mahakamani kwa madai kwamba ilikiuka Katiba ya nchi kwa kuwa Katiba ya Kenya haikuwa na masharti yanayoruhusu kutunga katiba mpya.
 Njoya & Others v Attorney General and Others[2004]LLR4788(HCK)


Mahakama Kuu ya Kenya iliamua kwamba mamlaka ya kutunga katiba waliyonayo wananchi hayana mpaka na hayawezi kuwekewa masharti na chombo chochote. (The constituent power to frame a constitution is unfettered by any external restrictions).

Wakati ikiamua kuhusu suala hili Mahakama ilijielekeza katika Kifungu cha 47 cha Katiba ya zamani ya Kenya (kifungu hicho kina maudhui sawa na Ibara ya 98 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) ambapo ilisema kwamba Bunge halikuwa na halina sababu ya kuingiza masharti hayo na kwamba hata kama Katiba ya nchi itakuwa imeweka masharti hayo, jambo ambalo linaweza kuwa ni uzoefu mzuri, bado kuwa na kifungu kama hicho katika katiba hakuongezi manufaa yoyote. Maana ya uamuzi huo ni kwamba mamlaka ya kutunga Katiba yapo nje ya Bunge la kawaida.

Wananchi ambao ndio msingi wa mamlaka yote, wanapohitaji kutunga Katiba Mpya hawahitaji kupewa mamlaka ya kufanya hivyo.  Profesa Yash Ghai na Profesa Palamagamba Kabudi wametukumbusha kuwa Wananchi wanapohitaji kufanya hivyo, wanakuwa juu ya Katiba yenyewe.

MADAI YA MABARAZA YA KATIBA
Mheshimiwa Spika, Yametolewa mapendekezo kuhusu kuanzisha Baraza la Katiba (Constitutional Conference).  Hoja hii inadai kwamba yangefanyika mabadiliko kwenye Ibara ya 98 ili kuweka utaratibu wa kuunda kwa Mabaraza ya Katiba ambayo yangetoa maoni na mapendekezo katika Rasimu ya Katiba.  Rasimu ya Katiba itawasilishwa kwenye Bunge Maalum la Katiba.  Wajumbe wa Baraza la Katiba watokane na vyama vya siasa, asasi za Kiraia na uwakilishi wa makundi mbali mbali ya kijamii.

Utaratibu huu unaopendekezwa ni moja ya njia zinazotumika katika kupata Katiba Mpya katika mazingira kama yafuatayo:-
Nchi inapotoka katika ukoloni kwenda kujitawala kama ilivyokuwa Tanganyika ambapo Baraza la Katiba lilikutana Karimjee mwaka 1962 na kwa Zanzibar lilifanyika Lancaster mwaka 1963;
Nchi inapotoka katika Utawala wa Kijeshi kama vile Ghana wakati wa Jerry Rawlings na Uganda wakati wa Museveni kuingia madarakani;
Nchi inapokuwa imetoka katika machafuko ya kisiasa;
Nchi inapotoka katika vita kama ilivyokuwa kwa Afghanistan.

Katika nchi nyingine.  Wajumbe wa Baraza la Katiba wanatokana na masharti ya sheria.  Rais angeweza kuitumia Sheria ya Uchunguzi yaani “The Commission of Inquiry Act, [Cap. 32 R.E 2002].  Baada ya kutafakari,  ndio maana, kwa mwongozo wa Katiba iliyopo na Vyombo vya Kikatiba vilivyopo kama vile, Bunge, tunaweka utaratibu huu unaopendekezwa katika Muswada ili utufikishe kwenye Katiba Mpya.

Utaratibu unaopendekezwa ni mzuri kwa kuwa unatoa fursa zifuatazo kwa Tume:
kuwatumia Wataalam elekezi katika kutafiti na kutoa ushauri;
kupata maoni na ushauri wa makundi mbali mbali ya kijamii kama vile-
asasi za kijamii;
asasi za kidini;
vyama vya siasa;
taasisi za elimu ya juu;
vyama vya wafanyakazi;
makundi yenye mahitaji maalum;
vyama vya wakulima;
vyama vya wafugaji; na
vikundi vingine vya watu waliojiunga pamoja kwa malengo yanayofanana.
Maoni, ushauri na mapendekezo ya makundi haya ndiyo yatakayokuwepo kwenye Rasimu ya Katiba.

Baada ya kupata Rasimu ya Katiba, Tume itachapisha Rasimu ya Muswada kwenye Gazeti la Serikali na magazeti ya kawaida ili wananchi waelewe maudhui yake.  Baada ya hatua hiyo Tume itaunda Mabaraza ya Katiba ili kupata maoni zaidi ya wananchi.  Utaratibu huu unatoa uwakilishi kwa uwazi zaidi, tofauti na chombo kinachopendekezwa na Mhe. Tundu Lissu, Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani kuhusu masuala ya Katiba na Sheria, na Mhe. Moses Machali. Mhe. Lissu amependekeza “Constitutional Conference” ya kuteua wajumbe wa Tume na Mhe. Machali amependekeza “Multiparty Commission”.  Hata hivyo, suala la nani hatimaye, atawateua Wajumbe wa Tume, haliwezi kuwa la vyama vya siasa kama ilivyotokea nchini Kenya na kama alivyoshauri Mhe. Tundu Lissu.  Kwa sababu ya tofauti za kiitikadi itakuwa vigumu kufikia mwafaka baina ya Tume ya aina hiyo.  Jambo ambalo linaleta kuzua vurugu.

Tumejifunza na tusikubali kufanya makosa kama jirani zetu.  Kwa kuzingatia ukweli kwamba tunaanzisha mchakato huu bila shuruti, ni vema tuchukue tahadhari.  Wanasiasa watapata fursa ya kutoa maoni kupitia mabaraza na makundi ya vyama vya siasa lakini pia watakuwa Wajumbe wa Bunge Maalum.  Vile vile, watashiriki katika kuwaelimisha wananchi kuipigia kura ya maoni Katiba inayopendekezwa. Kutokana na maelezo haya, sikubaliani na mantiki kuhusu ama “Constitutional Conference” ya aina aliyopendekeza Mhe. Lissu au “Multiparty Commission” kama alivyopendekeza Mhe. Machali kwa kuwa uzoefu umeonyesha kwamba makundi haya yana asili ya kuteka nyara mchakato wa Katiba, na kuugeuza kuwa suala la kisiasa, kikabila au undugu.