Wednesday 24 October 2012

SUE a.k.a mzee wa copy

Anaitwa Othuman almaarufu kama SUE mzee wa copy. Huyu nadhani wengi hamumfaham zaidi ya kusikia copy zake tu. Kwa wale waliopata bahati ya kusikia copy zake wanamtambua, baadhi ya ngoma(copy) alizowahi fanya ni pamoja na ile ya BURN IT UP ya R. Kelly ambayo aliita AMINA, hii aliifanya kwa producer Water wakati yupo Easy record @ Morogoro (2006), mbali na hiyo pia ameshakuwa na copy kama TEMPTATION ya P Square, COME TO MA ROOM, GIVE IT UP TO ME ya Sean Paul na zingine nyingi ambazo na hakika hamjapata kuzisikia. Pia amefanya Hali ni Mbovu ni remix ya All the above ya Maino aliifanya kwa producer Maneke (2009)

Mbali na hayo jamaa alishakuwa na plan ya kufanya MIXTAPE ya copy ambayo alipanga kufanya na Ngwear kwa kuwa kipindi kile Ngwear nae alikuwa na itikadi za kucopy ngoma za mbele mfano; CLUBBING ya Marquiz na HOTEL ya Cassidy. Hata hivyo wazo hilo halikuweza kutimia kwa sababu ambazo anazijua yeye mwenyewe na kuamua kufanya for funny yaan anafanya copy kwa kuwa ni hobie yako so hana mpango wa kuachia MIXTAPE wala kufanya for business.
Kama hujapata kusikiliza hata copy yake moja, hizi ni miongoni mwaa copy alizogonga. 
Artist: SUE
Producer: Water
Song: Amina (Burn It Up remix)

 Artist: SUE
Producer: Maneke
Song: Hali ni mbovu (All the above remix)

No comments: