Monday 22 July 2013

Barua ya Lauryn Hill akiwa jela

Barua kutoka kwa "Lauryn Hill" ilichapishwa Jumamosi (Julai 20) kupitia chanzo kisicho fahamika. Chanzo hicho kiliripoti kuwa, "Hill alisema angependa basi kila mtu ajue kwamba yeye anaendelea vizuri."

"Nafahamu tangu nikiwa mdogo sana kuangalia jambo lenye kusudio na namna katika kila kitu, ikiwa ni pamoja na majaribu," Hill aliandika. "Ingawa nimechukua baadhi ya marekebisho, siwezi kukana favor nilizopata nikiwa hapa, na mapokezi kutoka kwa jamii ya watu ambao licha ya hali zao, nimegundua njia ya kipekee ya kuwafanya wawe."  Hill aliongeza.

Hill ambaye kwa sasa anatumikia kifungo katika gereza la Danbury, Conn kwa adhabu ya miezi mitatu  baada ya kukutwa na hatia mnamo mwaka jana ya kushindwa kulipa kodi ya zaidi ya dola milioni 1.8 za mapato kutoka 2005-2007.

Kwa mwaka uliopita, aliyekuwa muimbaji wa kundi la Fugees ametuma Tumblr post lyrics na updates, kufafanua uvumi uliokuwepo na kutoa maoni yake juu ya ubaguzi wa rangi na ukosefu wa haki, ikiwa ni pamoja na kuhusiana na madai yake ya ukwepaji kodi.

"Asanteni,..kwa kuweza kuniandikia barua za ushauri na kuniombea japokuwa sina uwezo wa kuzijibu barua zote, ila mtambue nazipata, nazisoma na kuzitilia maanani
"....aliandika mkali huyo.

No comments: