Wednesday, 23 November 2011

TRACK LIST IN "MAC + DEVIN GO TO HIGH SCHOOL"

Snoop Dogg and Wiz Khalifa send out smoke signals with the soundtrack to their 2012 buddy film, Mac and Devin Go to High School, available December 13. The weed aficionados, who play Mac Johnson (Snoop) and Devin Overstreet (Wiz) in the stoner comedy, roll with Mike Posner (“French Inhale”), Juicy J (“Smokin’ On”), and Bruno Mars (“Young, Wild & Free”) on the 12 joints. Blaze up the tracklisting below.Mac and Devin Go to High School Soundtrack
1. “Smokin’ On” feat. Juicy J
2. “I Get Lifted”
3. “You Can Put it in a Zag, I’mma Put it in a Blunt”
4. “6:30”
5. “Talent Show”
6. “Let’s Go Study”
7. “Young, Wild & Free” feat. Bruno Mars
8. “OG” feat. Curren$y
9. “French Inhale” feat. Mike Posner
10. “It Could Be Easy”
11. “World Class”
12. “That…

JIGGALA: NEW ARTIST FROM MORO TOWN

 
JIGGALA/GY Msanii toka pande za Morogoro 
anayekuja vizuri kwenye game ya bongo flavour,
aliwahi fanya kazi na maproduza mahili hapa nawazungumzia 
Mika Mwamba na P Funk Majani miaka ya 2002.
Jiggala kwenye miaka ya nyuma aliwahi kuwa kundi moja na 
msanii maarufu hapa bongo "Squezer" wakiunda kundi la 
Easy Domp Camp lililokuwa na maskani yake huko 
Mji kasoro "Morogoro" na likisimamishwa na wasanii kadhaa akiwemo 
Jiggala ambapo kipindi hicho anajiita GY, Squezer na Nash G ambaye hivi sasa ni
mtangazaji wa redio Abood fm ya moro town.
Pia Jiggala aliwai toa ngoma kadhaa ambazo hazikuonesha mafanikio 
kwa upande wake japo zilikuwa kali, Alitoa ngoma iliyokwenda kwa jina la 
PARTY YA LEO aliyoifanya kwa super producer P Funk majani akimshirikisha BX.
Kwasasa kaja kivingine kabisa na ngoma inayokwenda kwa jina la Queen Waley.
Sikiliza ngoma hapa chini....




AJALI YA LOLI UBUNGO MITAA YA RIVERSIDE

Katikati ni gari ndogo nyekundu iliyokandamizwa chini ya gari kubwa jeupe la mafuta. kuna mtu yuko hai bado hajatolewa. habari zinasema watu watatu wamekufa kati yao mama mjamzito ambaye kichwa na kiwiliwili vimetengana.
Wakijaribu kunasua mwili wa wahanga hao wa ajali na miili ya waliokufa katika ajalia hiyo. Kama inavyoonekana hali ilikuwa ni mbaya sana watu wakiagalia kilichotokea bila kuaminai lakini ndiyo hivyo tena.
Watu wakiangalia tukio hilo leo mchana maeneo ya Ubungo River Side jijini Dar es salaam.

NEW TRACK: BAO LA KETE BY AT


JB ASEMA KAZI YA KUIGIZA INALIPA SANA!

JB "JACOB STEVEN"
Mwigizaji nguli wa filamu nchini Jacob Steven maarufu kama JB, amesifu sanaa hiyo na kusema wasanii waliofanikiwa katika fani hiyo kwa sasa wana utajiri mkubwa.
JB amepiga hatua kwa mafanikio na kupata umaarufu na sasa anapigana vikumbo na Steven Kanumba na Vicent Kigosi wanaotamba pia.

Akizungumza na blog hii JB alisema, “Kazi ya filamu sasa ni ajira safi kwa mtu yeyote, ukifanikiwa katika filamu wewe ni tajiri, kutokana na kipato utakachokuwa unakipata. Kama unatoa kazi za kwako tegemea mamilioni, lakini pia ukishirikishwa malipo yanajulikana, utalipwa kwa kiwango chako maana kila msanii ana dau lake.”

JB amesifu pia ushindani uliopo, kwani kila mmoja akitamani kuwa juu ya mwenzake na kusema ni moja ya mafanikio

SHILOLE KUJA NA “MAJIRANI LAWAMA”…!!

MISS SHILOLE 
Msanii wa Bongo movies Zuweza Mohamed anayefahamika kama Shilole, ameamua kugeukia katika uimbaji na tayari ameshatunga na kurekodi wimbo mmoja ambao utafahamika kama “Majirani Lawama”. Amesema wimbo huo ameshautengenezea video na upo katika maadhi ya Mduara, ndani ya wimbo huo kawashirikisha wasanii wenzake wa filamu ambao hakutaka kuwataja majina. Akiongea na DarTalk amesema, “Napenda sana kuimba muziki wa mahadhi ya mduara, mashabiki wangu wakae mkao wa kula muda si mrefu wimbo utaruka hewani”.