Wednesday, 23 November 2011

JB ASEMA KAZI YA KUIGIZA INALIPA SANA!

JB "JACOB STEVEN"
Mwigizaji nguli wa filamu nchini Jacob Steven maarufu kama JB, amesifu sanaa hiyo na kusema wasanii waliofanikiwa katika fani hiyo kwa sasa wana utajiri mkubwa.
JB amepiga hatua kwa mafanikio na kupata umaarufu na sasa anapigana vikumbo na Steven Kanumba na Vicent Kigosi wanaotamba pia.

Akizungumza na blog hii JB alisema, “Kazi ya filamu sasa ni ajira safi kwa mtu yeyote, ukifanikiwa katika filamu wewe ni tajiri, kutokana na kipato utakachokuwa unakipata. Kama unatoa kazi za kwako tegemea mamilioni, lakini pia ukishirikishwa malipo yanajulikana, utalipwa kwa kiwango chako maana kila msanii ana dau lake.”

JB amesifu pia ushindani uliopo, kwani kila mmoja akitamani kuwa juu ya mwenzake na kusema ni moja ya mafanikio

No comments: