Friday 15 August 2014

Future na Ciara wapigana chini

Ni miezi mitatu sasa tangu Future na Ciara wabahatike kupata mtoto wa kiume, na kufikia hatua za kufunga ndoa baada ya kuvishana pete, hatimaye wawili hao wapigana chini.

Kwa mujibu wa mtandao wa "US Weekly" wa nchini Marekani ume'report kuwa chanzo cha kuvunjika kwa mahusiano ya maarufu hao ni kutokana na usaliti uliofanywa na Rapper kutoka Atlanta "Future" kumsaliti mwanadadashost huyo "Ciara". Mbali na Ciara kufanya mahojiano na moja ya chombo cha habari na kusema wamejiandaa fresh na mipango yao ya harusi lakini jana imekuja habari ya wapendanao hao kumwagana.

Kwa mtazamo wa haraka umedadisi kuwa Future ndiyo tabia yake kwakuwa anawatoto watatu mbali na huyo wa Ciara ambao wako na mama tofauti.

No comments: