Monday 18 August 2014

Chris Brown vs Mkali wa Chuga

Kama umekuwa mfuatiliaji mzuri wa baadhi ya matukio ya hapa bongo, basi utakuwa si mgeni sana na hili...

Mnamo mwaka 2010/2011 kama sijakosea kuna jamaa alionekana wa ajabu sana hususani style yake ya mavazi mbali na style ya kuimba kwake. Kijana huyo aliyetokelezea kwenye kinyang'anyilo cha kumsaka mkali wa kuimba maarufu kama Bongo Star Search "BSS" ambacho hufanyika kila mwaka na kuweza kuibua vipaji, mkali huyo kutokea pande za Arusha ali'make headline saaana kwa wadau mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari, wenye blogs na baadhi mitandao ya kijamii na kuonekana kama jamaa ametupia vitu vya kushangaza.

"Hii ni old school mazee"....ndilo jibu alilokuwa akijibu wakati akihojiwa na mtangazaji wa BSS.

Sasa hii imekuja kuonekana kwa mkali wa kudance, kuperform show, kuandika nyimbo za RnB, mkali wa kuimba kutoka nchini Marekani ambaye kwa sasa anasumbua na wimbo wake wa "loyal", Chris Brown. Chris Brown yeye amekuja kuitupia hiyo style mwaka huu 2014 kana kwamba amekuwa nyuma ya mkali yule wa Arusha.

SASA NANI MKALI KATI YA CHRIS NA MKALI TOKEA PANDE ZA CHUGA??

No comments: