Monday 7 July 2014

Diamond amzawadia gari mama yake

Katika kusherehekea siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mama mzazi wa star anaeipeperusha vilivyo bendera ya Tanzania, kijana Nasib Abdul almaarufu kama Diamond Platnumz au muite Chibu Dangote kama anavyojiita mwenyewe...Diamond ameifanya furaha ya mama yake mzazi kuwa ya kifani na kuanza kudondosha machozi. Mama Nasib amedondosha machozi ya furaha pale alipotoka nje ya geti la nyumbani kwake na kukuta gari ikiwa imepark na kupokea taarifu kuwa hiyo ni zawadi yako toka kwa mtoto wako mpenzi "Diamond Platnumz"...mama akaanzatoa chozi la furaha huku akidhihilisha ya kuwa kweli kijana wake anampenda na kumjali.

Sherehe hiyo ilipambwa na bibie Wema Sepetu na wapambe wake...ikiwa sambamba na wadau mbalimbali na waandishi mbalimbali wa habari.

No comments: