Monday 10 March 2014

R.I.P Mdau Olais Lotta

Juzi usiku kuamkia siku ya jana Team Kibongobongo tulipokea taarifa za msiba kutoka kwa mdau wa Blog hii na page yetu, kuwa tumepoteza madau aliyekuwa akitoa support kubwa sana kutoka pande za Arusha... Mdau huyo aliyefahamika kwa jina la Olais Lotta, amefikwa na umauti akiwa safarini kurudi kwa Arusha akitokea jijini Dar es salaam baada ya kupata ajali. Kwa mujibu wa mtoa taarifa, amesema haikuweza kufahamika chanzo cha ajali hiyo zaidi ya kufahamu kuwa gari aliyopanda marehemu Olais ambayo ni ya binafsi ilipata ajali maeneo ya Kibaha na ndipo Olais akapoteza uhai wake.
Team_Kibongobongo tunatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki wote wa karibu wa mdau Olais Lotta. Pumzika kwa Amani kaka Olais nasi tupo nyuma yako.

No comments: