Hii ndio hali halisi ilivyo huko Dafur nchini Sudan ambako wananchi wa nchi hiyo wanaishi kwenye mazingira magumu kwa kukosa maji, chakula na malazi... ikiwa kama mahitaji muhimu yote wanayapata kwa taabu sana, hivyo basi ni dhahiri viumbe hawa wanapata taabu sana.
Wananchi hao ambao wanaishi kwa kutegemea misaada mbalimbali kutoka kwenye shirika la umoja wa mataifa (UN) kuweza kuendesha maisha yao kwa kupatiwa chakula na sehemu ya kujihifadhi, bado imekuwa hatarishi pia kwenye suala la maradhi na uzazi kwa wakina mama ambao wamekuwa wakijifungua kwenye mazingira hatarishi.
No comments:
Post a Comment