Monday 3 February 2014

Happy 10th Birthday Facebook

FACEBOOK ni miongoni mwa mitandao ya kijamii iliyoweza kuiteka dunia hasa katika nyanja ya mawasiliano kwa kupitia mtandao (Internet). Facebook ilianzishwa mnamo mwaka 2004, February 04 huko Cambridge Massachusetts, United States na kijana aliyefahamika kwa jina la Mark Zuckerberg akishirikiana na wanafunzi wenzie wa Harvard University wakiwemo Eduardo Saverin, Andrew McCollum, Dustin Moskovitz na Chris Hughes. 
Mwanzo kabisa Zuckerberg na wenzake waliuita jina la TheFacebook kabla ya kuwa Facebook, mtandao huo wa kijamii ulianza kutumika chuoni hapo "Harvard" kwa baadhi ya wanafunzi na baadae kuenea sehemu mbalimbali ikiwemo maeneo ya Boston, Ivy League pamoja na Stanford University ambapo ulikuwa ukiruhusu kutumika kwa wanafunzi wa high school na walio naumri kuanzia miaka 13 na kuendelea. Facebook imeongeza utumiaji kwa sasa ambapo utumiwa na watu wa rika lolote hususani wenye uwezo wa ku'access internet.

Hivyo basi siku ya leo tarehe 04 February, Facebook inatimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake...Team_Kibongobongo tunawatakia #Happy 10th birthday nyote mnaotumia mtandao huu wa kijamii.

No comments: