Monday 10 February 2014

Ben Pol kuachia album mpya Feb 11


Mkali wa Rn'B Ben Pol, ametamka kupitia kipindi cha E-News kinachorushwa hewani na EATV na kuwaahidi wadau na wapenzi wa muziki wake kuwa ataachia album yake yenye nyimbo 20 ambayo ataiweka kwenye baadhi ya mitandao ili kuwafanya wadau wake waweze kupata nyimbo zake na kuzisikiliza. 



Amesema nyimbo zitapatikana kwenye mtandao wa SHAZAM, iTUNE na baadhi ya mitandao ambapo utaweza kudownload kwa ghalama ndogo tu na kupata radha.
Kitendo hicho cha Ben Pol kuachia album kimekuwa cha kipekee kwani kwa kipindi hiki wapo wasanii wachache wanaoweza kutengeneza album zaidi ya kutegemea kufanya Tamasha/Show...Ben Pol amesema amefanyahivyo ili kuhakikisha wadau wake wanaweza kuenjoy radha za kwenye album hiyo. Pia ameongeza kusema kuwa kesho Februari 11 ataachia rasmi wimbo wake utakaoitambulisha album hiyo unaokwenda kwa jina la "UNANICHORA" akiwa ameshirikiana na mkali toka Ujerumani "Fundi Samweli"

No comments: