Monday 6 January 2014

R.I.P Eusebio Ferreira Da Silva

January 05 shirikisho la soka duniani, FIFA limeingiwa na majonzi makubwa baada ya kuondokewa na mmoja wa wali wa soka walioweza kutamba enzi hizo, EUSEBIO FERREIRA DA SILVA. Eusebio aliyekuwa mzaliwa wa Msumbiji na kupewa uraia wa Ureno kipindi bado Msumbiji inatawaliwa na Ureno, alipewa uraia wa kireno baada ya kuichezea timu ya taifa kwa mara 64 nakuweza kushinda magoli 41 na mnamo mwaka 1966 kuwa mchezaji bora wa dunia. 

Eusebio amefariki dunia akiwa na miaka 71, akiwa ameshacheza soka nakuwa mfungaji bora wa barani ulaya 1968-1973 na kuwa mchezaji bora wa barani humo mnamo mwaka 1965. 1974 amestaafu soka kwa kupata jeraha la goti...Eusebio mbaka anastaafu soka alikwishacheza jumla ya mechi 715 na kushinda magoli 725.
Eusebio amefariki dunia baada ya maradhi yaliyokuwa yakimsumbua kwa muda kidogo baada ya kufikishwa katika hospitali ya Lisabona na kulazwa kwa takribani wiki moja...kwa mujibu wa chanzo cha habari hii kinasema Eusebio alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa uliofahamika "hypertension" na kisha kupelekea  "bronchopneumonia" na kusababisha umauti wa staa huyo wa soka.

No comments: