Saturday 19 October 2013

miss TZ 2012 akikana kiswahili

Kufuatia mahojiano yaliyofanywa na redio Dochuvele dhidi ya mrembo huyo ambaye aliiwakirisha Tanzania katika mashindano ya dunia (miss world) bibie Brigitte Alfred... huyo alipoulizwa kuhusu yeye kuwepo kwenye mashindano hayo ya kumsaka mrembo wa dunia na mtangazaji wa wa redio hiyo inayorusha matangazo yake kwa lugha ya kiswahili akawa anajibu kwa lugha ya kigeni (kingereza) ambapo mtangazaji alimlazimu kujibu kwa lugha yetu ya kiswahili kwakuwa ni kipindi kinachorushwa kwa lugha ya kiswahili na husikilizwa na waswahili zaidi hivyo ingekuwa vyema zaidi angejibu kwa lugha ya kiswahili...lakini mrembo huyo alikana kukijua kiswahili hadi hapo mkurugenzi wa masuala hayo ya urembo (mamiss) Mh. Lundenga na baadhi ya viongoz waliokuwepo hapo kumuamuru kujibu kwa kiswahili na ndipo akajibu kwa lugha ya kiswahili napo ni kwa madoido yaleyale ya kuingizia na lugha ya kigeni katikati ya sentensi kadhaa kama.."yes, i'm, as you know, but, am happy...n.k)

Mbali na kitendo hicho alichokifanya dhidi ya mahojiano hayo pia alishaalikwa bungeni mnamo mwezi April kwenye moja ya kikao kilichoongozwa na ofisi ya bunge wakishirikiana na Umoja wa mataifa na mpango wa maendeleo "United Nations Development Programe (UNDP)...Pia mwanadada huyo alilishangaza bunge kwa kutozungumza lugha yake ya asili ya kiswahili kwani hakukuwa na ulazima wa kutumia lugha ya kigeni (Kiingereza.

No comments: