Thursday 19 September 2013

Hatimae wezi wa mtandao wakamatwa

mrembo huyu ni mmoja wa watuhumiwa wa kesi hii ya wizi wa mtandao baada ya kutumia kitambulisho chake na kutaka kuja kurudisha line ambaye sio yake kwa kuahidiwa kupewa pesa kidogo kama ujira wake na katika melezo yake akasema hawatambui wahusika wenzake kwani amekutana nao tu sinza na wakampa dili hilo na kuamua kuchukua bajaji ambao iliwaleta mpaka ofisi za tigo buguruni rozana

huyu ndio staring mwenyewe aliyechonga mchongo wote na kumshawishi huyo mwanadada kutumia kitambuluisho chake kufanyia wizi huo wa kimtandao

watuhumiwa wenzake wakificha sura zao huku wakitoa maelezo kwa wafanyakazi wa tigo na walinzi waliowatia chini ya ulinzi baaada ya kuweka mtego mzuri wa kuyanasa mataperli haya ya kimtandao 

hiki ndio kitambulisho alichotaka kukitumia mwanamke huyo kuswap line ambayo sio yake lakini aliweka jina la mhusika wa line na namba alizokuwa anapiga mara nyingi lakini sura yake bahati mbaya kwa umakini wa mfanyakaiz mmoja wa tiGO kwa jina Octavian Rweyendera alifanikiwa kubaini udanganyifu huo na kuamuru awekwe chini ya ulinzi mara moja 
aliyesimama hapo yeye alibiwa kiasi cha milioni moja kwa njia ya simu banking ya NMB baada ya line kuharibika ghafla kumbe mmoja wa watuhumiwa alirenew na kuiba pesa

hiki pia ni kitambulisho cha mteja huyo hapo juu aliyeibiwa pesa kwenye acount yake ya NMB kiasi cha milioni moja kwa njia ya sim banking baada ya mmoja wa hawa watuhumiwa kuja kurudisha yake hii kwa kutumia kitambulisho hiki ambacho kimetengenezwa kwani si halisi na hatimaye kufanikiwa kuiba pesa kwa sim banking baadae 
hapa mtuhumiiwa mmoja akiwan kajilaza chini kwa kugoma kutoa maelezo kwa walinzi waliowaweka chini ya ulinzi

wakiwa ndani ya gari ya polisi kuelekea kituo cha polisi buguruni

Umati wa watu uliofurika kushuhudia tukio hilo la aina yake 

mmoja ya wafanyakazi mahiri wa tigo bw Octavian Rweyendera amabaye alifanikisha kukamatwa kwa watuhum,iwa hao akitoa maelezo kwa baadhi ya maafande wa polisi jinsi wathumiwa walivyotaka kufanya wizi huo wa kimtandao 

Askari polisi wakimsikiliza kwa makini jinsi watuhumiwa hao walivyokamatwa

TIZAMA VIDEO YA TUKIO ZIMAHAPA CHINI

CHANZO:mwanahabariuswazi.blogspot.com

2 comments:

Anonymous said...

sasa huyo dada si mumfire na mumwache.

Anonymous said...

Duuh