Tuesday 3 September 2013

Dayna afunguka kuhusu kuibiwa wimbo wa "Number One" na Diamond

Msanii wa muziki wa bongo fleva  mwenye maskani yake mjini Morogoro, ambaye pia ni msanii pekee wa kike anafanya vizuri kutoka Morogoro, Dayna Nyange. amefunguka kuhusu tuhuma za kuibiwa nyimbo yake kupitia akaunti yake ya instagram, leo akiongea na marafiki inasemekana amekerwa na kitendo cha Diamond Platinum kuchukua idea ya beat iliyotumika kwenye wimbo mpya 'Number 1'
Huu ndio ujumbe wa Dayna Nyange#Kuna msanii mwenzangu nilikubaliana nae Ku Fanya nae kazi #kumshilikisha ktk wimbo wng nikampatia Na demo ya wimbo wangu Ila kanizunguka karudi tena studio Na katumia bit ile ile kafanyia kazi yamani #kaiimbiayy .kwa makubaliano yao Bila mimi Kujuaa chochote.

Akiongea na Chanzo cha habari hii; Dayna alisema “Kukweli nimekwazika sana  pia imeniuma, kwani sikutarajia msanii kama Diamond anaweza KUIBA nyimbo yangu na kwenda kuifanya yeye. Unajua nilikuwa nataka nimshirikishe kwenye nyimbo yangu ambayo nimefanya kwa Shedy Clever pale Tabata, hivyo nikarekodi demo, nikamtafuta na kumpatia ili aweze kusikia na kujua jinsi gani ataweza kuimba. Baada ya muda nikamtafuta tena ili tufanye kabisa ile nyimbo, ndipo akaanza kusema yupo bize nisubiri. Lakini nashangaa sasa hivi naisikia ile nyimbo ameeimba yeye tena harafu kibaya zaidi ametumia beat ile ile  pia na mashairi yale yale. Kiukweli alichokifanya sio kitu kizuri, kwani watu wote tunatafuta maisha sasa yeye ameangalia zaidi maslahi yake. Na usiku wa jana ndio ametoka kuitambulisha rasmi video ya wimbo huo..." alifunguka Dayna juzi kwenye moja ya mahojihano aliyofanya na chanzo chetu.
Nilikuwa namheshimu sana ila kwa hili nashindwa kusema kitu maana imenigusa sana, nyimbo yangu ilikuwa inaitwa my number one. Mpaka sasa bado sijajua nifanye kitu gani nipo katika kufikiri cha kufanya..." aliongeza msanii huyo huku akiwa katika masikitiko makubwa.
"Hii ndiyo habari ya mujini...ila kwasasa Dayna ameiachia Demo ya wimbo huo kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya media hapa town" kama tutaipata tutaiweka hapa muweze kuisikiliza

No comments: