Wednesday 11 September 2013

Binadamu wa ajabu aliyezaliwa China

Habari zilizopo ni kwamba bado kuna utata wa kwamba huyo kiumbe wa ajabu ni jamii ya Yeren au China, kutokana na maelezo ya mama mzazi wa kiumbe huyo amesema mimba ya huyo kiumbe aliipata baada ya kubakwa na kijana wa Yeren ambaye ni muwindaji wa hapo China...

Kwa mujibu wa mama huyo alisema baada ya kubakwa na muwindaji huyo mwenye asili ya Kiyeren, jamaa alitokomea na yeye kuachwa kikijini hapo mbaka miezi 9 ilipofika na kujifungua kiumbe huyo wa ajabu mwenye maumbile tofauti na binadamu wa kawaida, akiwa na umbile refu kwa kila kiungo, hana shingo kama ya binadamu wa kawaida, ana nywele za mnyama kama manyoya, haongei chochote kana kwamba anauwezo wa kusikia.

Kiumbe huyo ana umri wa takribani miaka 33 na bado kwa baadhi ya wakazi wa eneo hilo hawamjui kutokana na kufichwa ndani na mama yake.

Kwa mujibu wa wataalamu wamesema, mara nyingi kiumbe kama huyo anazaliwa akiwa na "Microcephaly" ambapo wengi huwa na maumbile tofauti na binadamu wa kawaida na huwa na muda mchache wa kuishi na ubongo wenye uelewa mdogo. Hata hivyo wataalamu wa suala kama hilo wameshindwa kutambua umbile la kiumbe huyo na namna alivyoishi kwa muda mrefu tofauti na viumbe wengine wenye tatizo kama hilo.

No comments: