Friday 16 August 2013

Uzuri wamnyima uongozi dada wa Iran

Msichana mrembo kutoka Iran amejikuta akikosa nafasi ya uongozi katika halmashauri ya jiji lake kwa kuambiwa kuwa yeye ni mzuri sana, hivyo amepitiliza sifa za nafasi hiyo…
Nina Siahkali Moradi (mwenye umri wa miaka 27) alikuwa miongoni mwa wagombea katika uchaguzi wa halmashauri ya jiji la Qazvin Iran, ambapo baada ya kura kuhesabiwa, alikamata nafasi ya 14. Lakini hata hivyo, wiki moja baadae, kura zake zilifutwa na kiongozi wa halmashauri ya jiji hilo kwa maneno ya kejeli akimwambia ‘we don’t want a catwalk model on the council’…
Katika uchaguzi huo, Nina alipata kura 10,000 na kumfanya akamate nafasi ya 14 kati ya 163, lakini wapinzani wake katika uchaguzi huo walilalamika kuwa Moradi alipigiwa kura kwa sababu ni mzuri sana, anavutia, pia mdogo…
Kwa mujibu wa The Independent, baraza huvhukua washindi 13 wa juu na mgombea anayeshika nafasi ya 14 huwekwa kama ‘reserve’…

No comments: