Friday 16 August 2013

Tamko la Mwakyembe kuhusu madawa ya kulevya

Waziri Harrison George Mwakyembe ametoa tamko kuhusu ishu ya madawa ya kulevya hususani kwa wale waliohusika na ishu hiyo iliyopelekea kukamatwa kwa wanadada warembo wa kitanzania...

Warembo hao walikamatwa nchini Afrika ya Kusini wakiwa na madawa ya kulevya yenye thamani ya Billion 6 za kitanzania na mbaka sasa kesi yao inaendelea kwenye mkono wa sheria...

Tukio hilo la kusafirisha madawa hayo limewahusisha baadhi ya wakuu wa idara ya ulinzi katika uwanja wa ndege wa Mwl. Julius Kambalage Nyerere jijini DSM. Waziri huyo wa usafirishaji na uchukuzi Mh. Harrison Mwakyembe ametoa tamko la kuwatimua wahusika hao wa idara hiyo ya ulinzi katika uwanja huo wa Mwl. Nyerere, kwa mujibu wa chanzo cha habari inadaiwa kuwa ni Wahusika wanne waliotimuliwa kazi na waziri huyo.

Hata hivyo Mwakyembe amesema tamko hilo halitaishia hapo atahakikisha atadili na kila muhusika aliyehusika kwenye matukio kama hayo ya upitishaji wa madawa ya kulevya either kwa kuingiza au kutoa.

No comments: