Thursday 22 August 2013

Drake kuachia Album Cover mbili za "Nothing was the same"

Mkali toka YMCMB, Drake amesema ataachia Cover mbili tofauti za Album yake mpya anayotarajia kuiachia mwezi September, 24 mwaka huu. Cover hizo zilizobuniwa na kuchorwa na mtaalamu wa kuchora wa miaka mingi nchini humo, Kadir Nelson...zitaitamburisha vyema Albun hiyo, hivyo wadau wa Drake wameombwa watoe maoni yao juu ya Album Covers hizo na wapendekeze wenyewe ipi itawavutia zaidi.

Kadir Nelson, ni mchoraji na mbunifu wa miaka mingi aliyejizolea umaarufu kupitia sanaa yake hiyo hususan kwa kuweza kuonesha kipaji chake kwenye baadhi ya events zilizowahi kufanyika kama the U.S. Postal Service, Michael Jackson,Sports Illustrated, Coca-Cola, and Dreamworks. Pia ameshatoa illustrated za kwenye baadhi ya vitabu vilivyowaelezea watu mashuhuli duniani kama Nelson Mandela, Joel Luis na Martin Luther King, Jr.

No comments: