Saturday 9 June 2012

NYANDU TOZI APATA MTOTO WA KIUME

NYANDU TOZ
Baada ya hivi karibuni kupatwa na majaribu ya kuibiwa gari lake kabla ya kulipata few days later, ex member wa Dar Skendo, rapper Dogo Hamidu aka Nyandu Tozi usiku wa kuamkia leo amefanikiwa kupata mtoto wa kiume baada ya his long time girlfriend kujifungua.
Akiongea na baabkubwamgazine.com, Nyandu alisema anashukuru mwenyezi mungu kwa demu wake kufanikiwa kujifungua salama huku akizaa mtoto wa kiume ambaye sikuzote alikuwa akitamani kuwa nae. "Alhamdulilah nimefanikiwa kupata mtoto wa kiume, nashukuru mama watoto amejifungua salama na mtoto yupo kwenye afya safi kabisa."
Talking about the name of his new baby Nyandu alisema:
"Mwanangu nimeamua kumuita Herry, ni jina la rafiki na ndugu yangu Herry Sameer "Mr.Blue. Hili jina zuri sana ambalo nalipenda na pili ni jina la mtu ambaye namkubali na kumheshimu sana, Mr.Blue Cabayser ni mtu ambaye tuna historia ndefu ya urafiki ambao sasa umekuwa kama undugu. Na pia kumpa mwanangu jina hili ni kitendo cha kutimiza ahadi niliyompa marehemu mama yake Mr.Blue ambaye nilimwambia kama nikija kufanikiwa kuzaa mtoto wa kiume ningempa jina la Herry."
SOURCE BABKUBWA MAGAZINE

No comments: