Tuesday 16 July 2013

Prezzo akataa suluu na Diamond

PREZZO2-2diamond-2
Hizi ni baadhi ya picha kwenye Tamasha la matumain
Prezzo amesema hawezi kumuomba msamaha Diamond kwenye Twitter kwa kuwa anaamini hakuna alichokosea na ni jambo la kitoto…
Akiongea leo mchana kwenye kipindi cha ''Mambo Mseto'' cha Radio Citizen, kinachoendeshwa na Willy M. Tuva, Prezzo amesema Diamond ndiye aliyemchokoza baada ya wasanii hao kutumbuiza mwanzoni mwa mwezi huu kwenye tamasha la Matumaini… Prezzo anadai aligundua kuwa Diamond alimponda kwenye magazeti ya Tanzania kuwa hamuwezi kwa lolote kwenye muziki…
Prezzo alisema: ''Mtu yeyote anamjua Prezzo ni kama rattle snake, ukimchokoza you have to get prepared to be bitten''…
Rapper huyo aliendelea kudai kuwa alimpigia simu Diamond lakini hakupokea na ndio maana aliamua kumdiss kwenye Twitter…
Prezzo alisema: ''Jamaa hakupokea simu nikaona ah! Basi liwalo na liwe, nika decide ku-air my views''…
Hata hivyo,Prezzo amesema hawezi kumuomba msamaha Diamond kwenye Twitter kama anavyomtaka afanye''…
Prezzo alisema: ''Unaona, kwa saa hizi akianza kusema aende kwa Twitter aniombe msamaha, maisha huwa hayaendi hivo… Kwa hivyo vitu vingine naona ni kama ni utoto unaingilia kati, kwani yeye kusema niombe msamaha kwa Twitter… niombe msamaha kwa kosa gani? Kusema ukweli, unajua mimi ni msema ukweli, mimi kuomba msamaha kwa Twitter naona kidogo ni utoto''…
Kwa kumalizia, Prezzo amesema hataki beef na Diamond kwa sababu anamheshimu na anamshukuru Willy Tuva kwa kujaribu kuwasuluhisha…

No comments: