Friday 12 July 2013

Pole Prof Jay na Z-Anto kwa kupoteza mama

Siku ya juzi (Tarehe 08)kuna taarifa zilitufikia TeamKibongobongo kuwa msanii wa kitambo kidogo anayewika mbaka sasa kwenye muziki wa bongofleva, Joseph Haule a.k.a Prof Jay amempoteza mama yake mzazi Rosemary Majanjara aliyepata ajali kwa kugongwa na gari akiwa anavuka barabara huko maeneo ya Mbezi Mwisho jijini DSM.
Leo tena tumepokea taarifa ya kusikitisha baada ya msanii Z Anto nae kupotelewa na mama yake mzazi aliyekuwa amelazwa katika hospital ya Mhimbili, jijini DSM.


Z Anto Wa Malavdav
Nw nipo muhimbili nmemleta mama hali yake c nzuri kabisa, ingawa kuumwa sio kufa ila kwa hali aliyonayo lolote laweza kutokea. naomben dua zenu ndugu zangu.
Z Anto amesema Mama yake, alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya ini kwa muda mrefu, lakini kwa takribani miezi miwili iliyopita hali yake ilianza kubadilika, na leo hii walimpeleka hospitali ya taifa ya Muhimbili, ambapo alifariki muda mchache baadae.

TeamKibongobongo tunatoa pole kwa ndugu, jamaa wa marehem wote......

No comments: