Wednesday 8 May 2013

Ferguson atangaza kustaafu Man U

Kocha wa Manchester United Sir Alex Ferguson ametangaza kuachia ngazi kama meneja wa Manchester United baada ya miaka 27 akiitumikia klabu hiyo...

Mzee Ferguson alisema yakuwa hatoiacha kabisa United bali atakuwa mmoja wa washauri wakuu ndani ya bodi ya klabu hiyo...
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 71 anajiandaa kuaga umati wa mashabiki Uwanja wa Old Trafford Jumapili baada ya mechi ya United dhidi ya Swansea, wakati watakapokabidhiwa taji la ubingwa wa Ligi Kuu England, hilo likiwa la 13 chini ya Ferguson...
Mazungumzo yanaendelea kumsaka mrithi wake na kocha wa Everton, David Moyes ni miongoni mwa wanaopewa nafasi...

No comments: