Sunday 6 May 2012

HII NDIO STYLE YA USAFIRI WA KIBONGO

Kwa takribani sasa ni miaka minne au mitatu na nusu tangu usafiri wa kutumia pikipiki kukithiri hapa Tanzania, baada ya kuwa ajira kwa vijana walio wengi kama ilivyokuwa nchini Nigeria. Usafiri huo maarufu kama Bodaboda, umechukua nafasi kubwa sana katika nyanja ya usafiri hapa bongo. Kama sijakosea kuna mikoa kama Songea, Tanga, Arusha, Mwanza na Morogoro nadhani ndio inaongoza kwa kuwa na utumiaji mkubwa sana wa aina hii ya usafiri. Kwa mikoa kama Iringa, Dodoma na baadhi ya mikoa mingine ya hapa nchini ndio inaanza kuongezeka utumiaji wa aina hii ya usafiri.
Pia aina hii ya usafiri ambayo imechangia kwa kiasi kikubwa kwa baadhi ya vyombo vya usafiri kama Tax, Daladala, Baiskeli na Bajaj kukosa soko kutokana na bei ya bodaboda na haraka ya usafiri huo.
Hata hivyo ndio imechangia kuleta vifo vinavyotokana na ajali za usafiri huo, pia watu kutapeliwa kwa wingi.
Japo serikali kupitia jeshi la polisi, wameweka sheria mbalimbali katika kuzibiti ongezeko la ajali na kusababisha vifo vya maelfu ya watu. Baadhi ya sheria hizo ni kuwalazimu madereva wavae element wanapokuwa safarini pia hata abiria wawe na element pindi wapandapo chombo hicho. Pia wamezuia kitendo cha abiria kupakizana zaidi ya mmoja (MSHIKAKI) ambayo ndio sababu kubwa ya ajali za pikipiki kana kwamba bado wabongo hatusikii kwa tamaa za pesa na kurahisisha matumizi ya pesa. Pia wamezuia mwendo kasi wa chombo hicho japo bado ni tatizo kwa madereva wengi. Leseni na baadhi ya kadi ambazo zitaonesha kuwa dereva ni mzoefu na mjuzi wa chombo hicho, pia limekuwa shida maana waliowengi ujifunza leo na kesho madereva.
HIZI NI BAADHI YA PICHA ZIKIONESHA USAFIRI
UNAVYOTUMIKA KATIKA HALI YA HATARI
Hii ndio kubwa kuliko, yaan hadi jamaa wa
usalama nae kakwea mishkaki.

No comments: