Tuesday 7 February 2012

"RESPECT NYERERE" COMING SOON

Siku chache zijazo,msanii Steve Nyerere,ambaye 
yaelekea ameamua kujikita katika filamu zenye 
uhalisia fulani hususani zenye mrengo wa kisiasa
anatarajiwa kuzindua filamu yake mpya
inayokwenda kwa jina Respect Nyerere 
ikiwa ni filamu kuhusu baadhi ya matukio au 
mambo yatokanayo na maisha ya Baba wa Taifa,
Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Steve Nyerere hivi karibuni alitoa filamu ya
Mr.President ambayo ni filamu yenye 
matukio sambamba na maisha ya Rais wa sasa,
Jakaya Mrisho Kikwete,amesema filamu ya  
Respect Nyerere itazinduliwa rasmi
14 Feb 2012 katika Hotel ya Serena jijini Dar-es-salaam.

No comments: