Monday 1 August 2011

IJUE SABABU YA LOON KUSLIM

Chauncey Lamont Hawkins al-maarufu kama Loon au Amir Junaid Muhadith, aliyezaliwa June 20, 1975 huko Harlem, New York Marekan. Ni African-American rapper ambaye amewahi fanya kazi zilizotamba kwenye game la musik ikiwemo kibao cha I NEED A GIRL part 1 na part 2, 2002 alivyofanya na P. Diddy. Loon aliyekuwa chini ya Label ya BADBOYS iliyo chini ya P. Diddy kabla ya kujitoa na kuanzisha Label yake iliyoitwa BOSS UP ENTERTAINMENT baada ya kutoka na album yake ya kwanza aliyoiita LOON october 21, 2003, kisha kufuatia na album zingine zikiwemo NO FRIENDS august 29, 2006 na WIZARD OF HARLEM october 17, 2006. Pia ameshafanya kazi na Nako 2 Nako Soldiers iliyoitwa 'Loon Bongo' chini ya producer Dunga studio za Mandugu Digital.
Mbali na music Loon pia amewahi kucheza movie kama State Of Property 2 na Death Of A Dynasty iliyo'directed by Damon Dash.
Miaka ya hivi karibuni Rapper huyo alitangaza rasmi kujiunga na dini ya kiislam, ambapo alibadirisha jina lake toka Chauncey Lamont Hawkins na kuitwa Amir Muhadith. Loon ameshatembelea Mecca, Saud Arabia na ile miji mikubwa yenye iman ya kiislam. May 26, 2010 alitembelea Ngome ya McMurray, Alberta, Canada na kuzungumzia maisha yake na kwanini ameamua kuslim na kuwa muislam.
Mwanzoni mwa 2009 Loon alifanya mazungumzo na mtangazaji wa Al-jalzirla alisema kuwa sababu ya yeye kuslim ni kushawishiwa na sheikhe au maalim Alii, ambaye aliandika Quaran kwenye maandishi ya kingereza na kukiuza nchi mbalimbali, Loon baada ya kukinunua kitabu hicho alikisoma na kuingiwa na iman iliyomfanya aslim na kuwa muislam kamili. Hata hivyo kuhusu music amesema hawezi kuacha bali hata imba tena Hip Hop na R 'n B ila ataimba Kaswida kama anavyofanya sasa.
 Amir Muhadith a.k.a Loon moja ya mahojiano
Picha tofauti zikimuonesha Loon alivyokuwa mwanzo na hivi sasa

No comments: