Drake na Rihanna walionekana kuwa kivutio kikubwa sana pale walipopanda steji moja na kuimba nyimbo walizokwishafanya collabo.
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana wakiwa kwenye ziara ya mwanamuziki Drake kutoka Cash Money, ambayo ni ziara yake huko Paris nchini Ufaransa iliyoitwa "Would You Like A Tour"...ndipo dada huyo aliweza kumsindikiza mkali huyo aliyewahi kuwa mpenzi wake kitambo flani.
Drake alianza kutoa burudani kwa kuimba nyimbo zake kadhaa mbaka hapo alipotaka kuimba wimbo wa "Pour It Up" alioufanya na Rihanna, ndipo mwanadadashostito huyo akaona ni kheri akampe shavu bby wake wa longtime... kitendo hicho kilikonga sana mashabiki waliohudhuria tamasha hilo kwani hawakutegemea kama kitendo hicho kingeweza kutokea. Rihanna aliendelea kumpa'tough jamaa yake (Drake) mbaka hapo walipopanda na wimbo wa "Take Care" walioufanya wote mwaka 2012 na ndipo burudani ikashamiri zaidi baada ya wawili hao kuanza kubambiana kimahaba mahaba na kuleta hamasa kubwa sana kwa wadau waliohudhuria tamasha hilo.
No comments:
Post a Comment