Wengi wenu najua mnamkumbuka mwanadada huyu aliyewika miaka
ya 1990’s, hususani kupitia filamu ya SARAFINA. Sarafina ni jina la muusika
mkuu wa kwenye filamu hiyona pia ni jina lililobeba tittle ya filamu hiyo
iliyojaribu kuelezea maisha halisi ya nchini Afrika ya kusini dhidi ya ubaguzi
wa rangi.
Leleti Khumalo
ukipenda muite Sarafina kama wengi
wenu mnavyomjua, amezaliwa miaka 44 iliyopita (30 March 1970)huko KwaMashu
kaskazini mwa Durban, nchini Afrika Kusini. Sarafina alianza kubainika kuwa
anakipaji na mwenye nia ya kuwa muigizaji tangu akiwa mdogo na ndipo baba yake
mzazi kuamua kumpeleka kwenye kikundi cha dance “AMAJIKA”.
Mnamo mwaka 1985 alijiunga na kikundi cha muziki “Mbongeni
Ngema’s music”. Sarafina aliweza kuuvaa uhusika kwa kuweza kuigiza maigizo ya
jukwaani na kushinda NAACP Image Award kama Muigizaji bora wa kike kwenye
jukwaa mnamo mwaka 1987.
Mwaka 1992 aliweza kuungana na baadhi ya waigizaji maarufu
wakiwemo; Whoopi Goldberg, Mariam Makeba
na John Kani na kuweza kuigiza
filamu yake iliyompa umaarufu ya Sarafina.
Mbali na kuweza kuwa muigizaji maarufu Afrika na dunia
nzima, Sarafina mwaka 1993 alitoa Album yake ya Leleti and Sarafina ambayo iliweza kuuza na kumpa pato kubwa.
No comments:
Post a Comment