kiukweli,
nasikitishwa sana jins baadhi ya wasanii kutwa wanavyolazimisha
kunitengenezea ugomvi wa kilazima pasipo kuwa na sababu, mara wengine
wakizusha eti Nimewatusi kwenye Media, Mara sjui Nimepost kuwakashif,
yaani ilimradi tu....kwanini Wanamuziki wa Tanzania Tunashindwa
kubadilika... mbona mi nahangaika na muziki wangu kimpango wangu...
Mnasema nyie ndio mnaojua kuimba mie sijui "sinatatizo"... Mnasema nyie
ndio wenye sauti nzuri yangu mbaya "Sina tatizo"... sasa mbona tena bado
mnanifatilia na kutokujua kwangu... Nafkiri ni vyema mkaanza kutumia
ujuzi wenu kukuza sanaa ya nchi yetu na kuleta heshima na maendeleo
nchini, kuliko kupika majungu..... Watu wanataka kazi!
No comments:
Post a Comment