Ni siku chache zimepita tangu PNC atangaze rasmi kujitoa Mtanashati
Entertainment na kujiunga na crew nyingine ambayo nayo ikatangaza
kufurahia kwake kumpata msanii huyo ambaye walidai na recording za ngoma
zao zimeshaanza.
Lakini siku ya jana Big Boss wa Mtanashati ambaye ni Ostazi Juma
aliweka wazi kwenye mitandao ya kijamii juu ya tukio la kurudi kwa PNC
na kumuomba msamaha na kuhitaji arudi tena kundini. Kama haitoshi kuweka
wazi huko kuliambatana na maneno haya
Status ya kwanza: “hahaha jamani mziki ni kazi pnc arudi kuomba msamaha ili aendelee kufanya kazi mtanashati.”
Status ya pili: “jamani mziki ni mgumu sana, pnc karudi kwa kuomba msamaha kwa boss wake Ostaz juma.”
Mbali na picha hizo ambazo zimeleta gumzo kubwa mitandaoni haikuishia
hapo bali Ostaz alitupia na video inayochukua sekunde kumi na sita
inayomuonesha PNC akiomba radhi kwa bosi wake huyo wa zamani ili arudi
kwenye usimamizi wa Mtanashati Entertainment.
Habai hii kwa hisani ya Baabkubwa magazine
1 comment:
ni ujinga na kudhalilishana tu
Post a Comment