Saturday, 10 November 2012

walter chilambo ndio habari ya mujini!!

Mchakato ulikuwa ni mgumu sana kubaini nani atanyakua kile kitita cha million 50 kwani walioingia kwenye top 5 walikuwa niwakali pia wana vipaji binafsi, kwa majaji iliwalazimu kutupiana mzigo wakutangaza matokea.
washiriki walioweza kuingia top 5 ni pamoja na Msami Nkwabi, Salmah kutoka Zanzibar, Wababa, na Walter Chilambo.
Kwa kuonesha kipaji alichonacho kijana Walter aliweza kuishangaza Tanzania na kuweza kutimiza ndoto zake kwa kuibuka mshindi wa EPIQ BONGO STAR SEARCH 2012 na kunyakuwa kitita cha Tshs 50million.
 Walter akikabidhiwa kitita cha 50mil.
 Hii ndio iliyokuwa top 5
Majaji wakifuatilia show kwa umakini sana
 Walter akiimba na Ben Pol
 Mshindi #3 Wababa akifanya collabo na Mwasiti
 Linah na Amin wakitumbuiza kwenye mashindano hayo
 Walter alipoimba na Ditto, naweza sema ndio moja ya collabo iliyofanyapoa kwenye mashindano hayo
mshindi #2 Salmah toka Zanzibar akifanya collabo na Linex
"Picha kwa hisani ya blogs mbalimbali"

No comments: