Nov 11, 2012. maelfu ya wakristo wanaoishi Malaysia walikesha kwa kuimba, kusali kwa kuweka mishumaa kwa kile walichokiona kwenye madirisha ya hospitali ya magonjwa ya moyo ghorofa ya saba (Subang Jaya), nchini Malaysi. Tukio hili lilifanya maelfu ya wananchi wa Malaysia kushangazwa na tukio hilo la kuonekana kwa taswira ya bikira maria na Yesu. Wapo waliotoka Singapole (300 kilometa) na baadhi ya maeneo yaliyo karibu na mji huo kuja kujionea tukio hili la kustahajabisha.
Haikuchukua muda kwa picha hizo kuonekana kwenye mitandao ya kijamii kama facebook na twitter. Kwa mujibu wa madaktari na wauguzi wa hospital hiyo hawakuwa na la kusema zaidi ya kushangazwa pia na tukio hilo.
Taswira zilizoonekana dirishani mwa hospital hiyo toka ghorofa ya 7 na ndio zilizo'appear kwenye mitandao ya kijamii (facebook na twitter)
Baadhi ya wakristo wakisali chini ya taswira hizo
"speacial thanks to Aziza Mkwata for this news"
No comments:
Post a Comment