Wednesday, 2 May 2012

MOJA YA AJALI ZILIZOLIZA WATANZANIA WENGI 2011

Watu 13 walifariki dunia na wengine kujeruhiwa vibaya katika ajali ya basi aina ya Coaster lenye namba za usajili T 361 BGE lililokuwa limebeba wanamuziki wa kundi la Five Stars Modern Taarab waliokuwa wakitokea Kyela-Mbeya kueleka jijini Dar.
Ajali hiyo ilitokea mwaka jana tarehe 22 Mei 2011 majira ya saa mbili usiku ndani ya hifadhi za wanyama za Mikumi mkoani Morogoro, baada ya gari hilo kuligonga kwa nyuma roli aina ya Scania lenye namba za usajili T 848 APE lililokuwa linavuta tela lenye namba za usajili T 559 BDL liliokuwa na mzigo wa mbao.
Waliopoteza maisha katika ajali hiyo ni:
Issa Kijoti, Omar Tolu, Haji Babu, Sheba Juma, Omar Hashim, Tizo Mgunga, Hamisa Mipango, Husna Mapande, Samir Maulid, Hasan Ngereza, Rama Kinyoya, Nasoro Madenge na mcheza shoo wakitu tigo mmoja.


Baadhi ya wakazi wa Morogoro wakiwa mahala
zilipolazwa maiti (MOCHWALI)
baadhi ya waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo na wa
 tatu ndio Issa Kijoti aliyekuwa mwimbaji mashuhuri
 wa bendi hiyo ya Five Star Mordem Taarabu

 Baadhi ya vyombo vya muziki vikiwa vimeharibika
Hili ndilo gari waliloligonga kwa nyuma na kusababisha 
ajali iliyopoteza wapenzi, ndugu na jamaa
zetu wa Five Star Modern Taarab
mnamo tarehe 22 Mei, mwaka 2011
Mungu azilaze roho za marehemu mahali
pema peponi, AMEEEEEEEEEEN!!

No comments: