Thursday, 15 November 2012

picha ya diamond iliyo'make headline kwenye mitandao ya kijamii

Hii ndio iliyo'editiwa na kusambaa mitandaoni
Hii ndio picha halisi
Kwa mtazamo wa kina zaidi naona iko haja ya wasani wetu pamoja na watu wengine kuwa makini sana katika suala la upigaji wa picha za nusu uchi kwa sababu ni rahisi sana kwa watu wenye ujuzi kuzi edit picha.
Sote tunakumbuka kuwa wakati wa fiesta ya mwaka huu iliyofanyika jijini Da es salaam October 5, 2012,diamond na kundi lake walivua nguo na kubakiza boksa tu.... Nadhani lengo lao lilikuwa ni kukuza jina. Bahati mbaya sana lengo hilo halikutimia na badala yake jamii iliwashangaa na kuwachukulia vibaya....... 
Mshangao huo haukuishia hapo kwani watu wasio na kazi nao wamekuja na lao jipya baada ya kuziedit picha hizo na kuzisambaza mitandaoni hasa facebook na twitter. 
Kiukweli picha hii imefanya baadhi ya wadau wa musiki wafikilie vibaya kwa kile alichokifanya msanii huyo anayetamba kwa show hapa nchini na nje ya nchi.
Binafsi imenishtua sana kuona moja ya picha zilizoeditiwa kwani imemshushia 'personality' msanii huyo...Hivyo nyie wasanii na wanajamii wengine tubadilike jaman mambo haya ni uzalilishaji mnaojitakia wenyewe!!

No comments: