Wanafunzi hao walikuwa wakiimba nyimbo mbalimbali za kuhamasishana wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali kwa lengo la kuushinikiza uongozi wa chuo hicho kurudisha serikali ya wanafunzi (MUHASSO).
miongoni mwa wanafunzi waliotiwa mbaroni
tayari kwa kupambana na vurumai hizo
Rais mstaafu Ally Hassan Mwinyi akiingia pamoja na
baadhi ya wakuu wa chuo cha sayansi Muhimbili
baadhi ya wahitimu
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho, Deogratias Ntukumazina alitoa ahadi kwa wanafunzi hao ya kuirudisha Serikali ya Wanafunzi pindi watakapofuta kesi waliyofungua Mahakama Kuu kauli ambayo ilipingwa vikali na wanafunzi hao na kutishia kuvuruga shughuli za mahafali zilizokuwa zimesimama kwa muda kutokana na wanafunzi hao kufanya mkutano wao uongozi wa Chuo mbele ya Jukwaa ambalo sherehe za kuwatunuku wahitimu zingefanyika kutokana na kugoma kuondoka mahali hapo hata baada ya uongozi wa Chuo kuwataka kufanya hivyo jambo ambalo lilisababisha Jeshi la Polisi kuongeza nguvu ili kuwatawanya.Hali ilivyokuwa mbaya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile alitoa amri kwa Polisi waliokuwa wakilinda Usalama kutumia nguvu jambo ambalo lilisababisha baadhi ya wazazi waliofika katika mahafali hayo kukimbia ovyo na kuanguka na watoto na kusababisha baadhi yao kuumia kutokana na mawe yaliyokuwa yakirushwa na wanafunzi na baadhi ya viti kuvunjwa na wanafunzi hao, katika kurupushani hiyo baadhi ya wanafunzi walikamatwa na Polisi.
Katika Mahafali hayo ambayo baadaye yalifanyika chini ya ulinzi mkali baada ya polisi kuwatawanya wanafunzi hao baada ya njia ya majadiliano kushindikana kutokana na jazba za wanafunzi hao waliokuwa walikuwa wakidai serikali ya wanafunzi irudishwe leo.
Hata hivyo Kwa mujibu wa mmoja wa wanafunzi hao aliyetambulika kwa jina la Njechele Boniface alisema kuwa walianza kukusanyika chuoni hapo majira ya saa mbili asubuhi ili kufanya mkutano wao na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo, Deogratias Ntukumazina ili kuepuka kuingiliana na shughuli za mahafali hayo lakini Mwenyekiti wa Baraza la Chuo alifika chuoni hapo majira ya saa sita mchana na kusababisha kuingiliana kwa mkutano huo na shughuli za mahafali hayo.
No comments:
Post a Comment