Tuesday, 16 April 2013

ndege iliyokosea njia na kuanguka baharini

Ndege moja ya nchini Indonesia iliyokuwa imebeba abilia zaidi ya 130 ilikosea njia ya kutua kwenye kiwanja cha ndege cha Bali siku ya jumamosi na kutua kwenye bahari, huku ikiacha idadi kubwa ya watu wakiwa majeruhi. Abilia walipiga kelele kwa woga wakati ndege hiyo iliposhindwa kutua kwenye njia ya ndege iliyopo kwenye kisiwa maarufu cha Denpasar, huku ikielezwa kwamba hali ya hewa ilikuwa shwari na hakukuwa na tatizo lolote.
Mara baada ya kuanguka kwenye bahari ndege hiyo ilienda na kuelea si mbali na usawa wa njia ya kutulia ndege. “Ndege ilikuwa inakaribia kutua na gafla akaangukia baharini. Watu ndani ya ndege walihamaki na kuanza kupiga kelele,” alisema Dewi, mmoja kati ya abilia ambae alikuwa na majeraha madogo.

No comments: