Inasemekana ndio vijana wanaotikisa kwa upande wa R n B kwenye musiki wa bongoflavour, kutoka kushoto;
BELLE 9, BARNABA & DIAMOND. Naweza kusema ni miongoni mwa wasanii wanaoweka soko la sanaa juu na kufanya ipendwe zaidi tofauti na hapo awali na kupelekea vijana wengi kujikita kwenye sanaa kama ajira yao. Belle 9 aliyetamba na kibao cha
Sumu ya penzi, Masogange, We ni wangu alichomshirikisha Mr. Blue na hivi sasa anatamba na singo yake inayoitwa
Nilipe Nisepe aliyofanya kwa produza Mona. Barnaba aliyetamba na kibao cha
Njia panda akiwa na Pipi, Ushawahi,Wrong namba, sasa hivi anatamba na Milele Daima. Kwa Diamond a.k.a rais wa wasafi alitamba na
kamwambie,Mbagala,Nitarejea na sasa anasumbua na kibao cha Moyo wangu.