Friday, 16 September 2011

SOKO LA SIDO JIJINI MBEYA LILIVYOTEKETEA

Leo majira ya saa 3 asubuhi soko la SIDO jijini Mbeya liliteketea kwa moto.
 KIKOSI CHA ZIMAMOTO KIKIJITAHIDI KUUZIMA MOTO HUO

Soko la SIDO lililokuwa mbadala baada ya soko Kuu la Mwanjelwa mjini Mbeya kuteketea kwa moto Disemba 12, 2006, na kusababisha vilio, simanzi na watu 20 kujeruhiwa, baadhi yao kupoteza fahamu baada ya mali zao za mamilioni ya fedha kuharibiwa, nalo limeteketea kwa moto.

Waandishi waliowasiliana na blogu wanaripoti kuwa tukio la kuteketea kwa soko limetokea leo asubuhi majira saa 3:10 na moto huo bado unaendelea kuwakaBaada ya eneo la katikati la soko kulipuka na kuanza kuwaka moto huku tayari wafanyabiashara wakiwa wameshafungua maduka na vibanda vyao wakiendelea na biashara, ndipo waliposhuhudia moto huo.

Walioshuhudia tukio hilo wanasema wafanyabiashara walianza harakati za kuuzima moto huo bila mafanikio huku wengine wakijitahidi kuokoa mali zao kwa ziondoa eneo la soko, “kwa kweli moto ni mkubwa na hatujui chanzo chake nini kwani ghafla tumeona moto ukiwaka eneo la soko upande wa katikatika wa soko hilo hivyo kila mtu anashangaa ulikoanzia moto huu” alisema mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Francis James.

Alisema kuwa magari ya zimamoto ya halmashauri ya jiji la Mbeya yamefika eneo la tukio lakini yameshindwa kuuzima moto huo baada ya kuonesha kuongezeka kwa kasi kuwa mkubwa na badala yake wananchi kufanya juhudi ya kuokoa mali zao, “Kwa sasa tayari jeshi la polisi limefika hapa kwa ajili ya kuwasaidia wananchi kuokoa mali zao ikiwa ni pamoja na kuzuia vibaka kuiba mali za watu kwani hali ni mbaya wafanyabiashara na wananchi wengi wamechanginikiwa kutokana na magari hayo kushindwa kuzima moto huo”alisemaKatibu wa soko kuu la zamani la Mwanjelwa Godfrey Haule alisema kuwa uwezekano wa kuuzima moto ni mgumu kutokana na moto kuendelea kuongezeka kwa kasi na kwamba gari la zimamoto limeondoka eneo la tukio baada ya kuishiwa maji na kwenda kuongeza maji.

Haule alisema kuwa moto huo ulianza kuwaka katika ya soko katika vibanda vya wakina mama lishe (mama ntilie) ambapo moto huo ungeweza kuzimwa mapema lakini walishindwa kufanya hivyo kutokana na kukosa maji kwa sababu mabomba ya yaliyopo katika soko hilo hayatoi maji na hivyo kusubiria magari ya ziamoto ambayo pia yameshindwa kuuzima moto huo.

“Mabomba ya soko yangekuwa yanatoa maji tungefanikiwa kuuzima moto mapema lakini tulishindwa baada ya kwenda kungulia mabomba hayo yakakawa hayatoki maji na lilikuja hapa gari la zimamoto pia limeshindwa kuuzima moto huo kutokana na kuwa mkubwa walivhoambulia na kiushiwa maji katioka gari na kwenda kuongeza mengine.”alisema
Soko Kuu la Mwanjelwa la jijini Mbeya liliteketea kwa moto Disemba 12, 2006 uliteketeza zaidi ya vibanda 506 na mali zenye thamani ya mamilioni ya shilingi.

Disemba 1, 2010 soko kuu la Uhindini jijini humo liliteketea kwa moto pia. Soko hilo lilikuwa linategemewa na wakazi wengi wa Mkoa wa Mbeya na nchi jirani za Zambia na Malawi ambao walikuwa wakilitumia kwa mahitaji ya vyakula, mavazi na mahitaji mengine muhimu.

Zimamoto liliwahi kufika eneo la tukio, lakini lilishindwa kutoa msaada wowote kutokana na miundo mbinu mibovu ya soko hilo la Mwanjelwa iliyolizuia magari kuingia ndani na kuzima moto ambapo Serikali Mkoani Mbeya liliomba eneo la muda la SIDO kwa ajili ya kupata soko mbadala na wafanyabiashara kuhamishia biashara zao hapo ambapo pia soko hilo limeteketea kwa moto.

Wakati huo huo askari wa kikosi cha kutuliza ghasia FFU wamelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya vibaka ambao walikuwa wakipora mali za wafanyabiashara katika eneo hilo huku baadhi ya wananchi wenye jazba wakiwacharanga mapanga vibaka hao.
 
Imeelezwa kuwa watu kadhaa wamejeruhiwa kwa kipigo na wananchi kwa tuhuma za wizi wa mali huku wafanyabiashara nao wakijeruhiwa kwa moto wakati wakijaribu kuokoa mali zao kwa kuzima moto huo.