Thursday 23 October 2014

Sauti Sol waibuka Best African Act-MTV EMA

Kundi la muziki kutoka nchini Kenya la Sauti Sol, limewamwaga wasanii wengine kutoka Afrika ambao walikuwa wakiwania tuzo za MTV EMA kupitia kipengere cha "Best African Act" na kuweza kuibuka washindi. Baadhi ya wasanii waliotupwa kule na kundi hilo ni; Davido kutoka nchini Nigeria, Diamond Platnumz kutoka Tanzania pia wakiwemo na wasanii wengine wawili.

Kwa sasa Sauti Sol wanahitaji kura za pamoja kutoka bara zima la Afrika ili wakaiwakirishe Afrika katika kinyang'anyiro cha kuwania tuzo hizo kama "Worldwide Act" kwa mwaka 2014. Kwenye kinyang'anyiro hicho watachuana na wasanii wengine walioweza kupita kwenye mabara yao na kuwania tuzo hiyo.
 
Watakaowania tuzo hizo ni;
Sauti Sol (Africa)
Yo Yoh Honey Singh (Asia/India)
Mohamed Assaf (Middle East)

No comments: