Friday 25 July 2014

Pata kumfahamu Koffi Olomide

Natumaini kuwa si mgeni sana na jina hili la Kofii Olomide hususani kwa kile kizazi cha 2000's kushuka chini na hasa hasa wale vijana wazamani kwenye miaka 1990's.

Koffi Olomide ni msanii mkubwa wa muziki wa Dance wengi upenda kuuita "Lingala" kutoka huko nchi ya Demokrasia ya Congo.
Jina kamili la mwana'lingala huyu ni Antoine Christophe Agbepa Mumba, maarufu kama Koffi Olomide alizaliwa miaka 58 iliyopita (Julai 13, 1956) siku ya Ijumaa huko Kisangani Demokrasia ya Congo. Jina hilo la Koffi alipewa na mama yake mzazi akiwa na maana ya kuzaliwa kwake siku hiyo ya ijumaa (Friday).

Koffi amezaliwa na kukulia kwenye familia ya hali ya kawaida ikiwa na maana kwamba familia yao haikuwa ya juu kiuwezo wa ya chini (middle class - Family)

Alianza kujifunza kuimba na kuandika mashairi akiwa na umri mdogo na kuwashangaza majirani zake hususani umahiri wake wa kutunga mashairi na kupiga gita.

ELIMU: Koffi aliweza kubainika na baadhi ya wanafunzi wenzie na walimu wake kuwa ni miongoni mwa wanafunzi wenye akili sana darasani na kuweza kubahatika kupata scholarship ya kwenda kusoma huko Bordeaux nchini Ufaransa, ambako alichukua degree yake ya Biashara na Uchumi. Koffi alireportiwa kuwa ana'hold masters ya degree ya Hesabu aliyochukulia huko Paris, kwenye chuo cha Paris University, nchini Ufaransa.
Koffi alirudi nchini Kondo mnamo mwaka 1970's na kuweza kujiunga na Band ya Papa Wemba, Viva la Musica, alianza kama mtunzi na mwandishi katika band hiyo na muongozaji wa sauti pia. Mnamo mwaka 1986 Koffi alianzisha band yake aliyoipa jina la Quartier Latin, ambayo imeweza kusherehekea uwepo wake wa miaka 20 mnamo mwaka 2006.

FAMILIA: Koffi ameoa na ni baba wa watotowatano; Nzau Twengi Aristote, Elvis, Minou Miss Univers, Didi Stone Nike, Rocky, Del pirlo Mourhino and Saint James Rolls. Baba yake na Koffi ambaye hayuko poa kiafya anaishi Paris nchini Ufaransa na mama yake mzazi yupo Kinshasa, nchini Kongo na ni mfanyabiashara wa samani (jewelley) kwenye soko la Zando. Pia Koffi ana kaka yake mkubwa, Johny Ko ambaye anaishi Paris na mdogo wake Tutu Roba ambaye anaishi huko London, Uingereza.

No comments: