Friday 25 July 2014

Msudan aliyehukumiwa kunyongwa akutana na Papa huko Italia

Papa Francis akutana na bi Merian huko Vatican;
Mwanamke raia wa Sudan Merian aliyesamehewa adhabu ya kifo baada ya kubadili dini amesafirishwa hadi nchini Italia baada ya kuwa kwenye ubalozi wa Marekani mjini Khartoum kwa zaidi ya mwezi mmoja.
Meriam Yahia Ibrahim Ishag na familia yake waliondoka na ndege ya serikali ya Italia wakiongozana na Waziri wa nchini Italia Lapo Pistelli.
Baada ya kuwasili Italia bi Merian alikutana na Papa Francis ambaye alimsifu kwa kusimamia dini ya ukristu licha ya tishio la mauti.
Merian alikutana na papa katika makao yake rasmi ya Santa Marta iliyoko kwenye makao makuu ya kanisa Katoloki ya Vatican.
Mkutano huo ulidumu kwa takriban nusu saa .
Baba wa Meriam ni muislamu na kwa Misingi ya sheria ya dini hiyo nchini Sudan Meriam pia ni muislamu na hawezi kubadili dini.
Meriam mwenyewe alilelewa na mama yake ambaye ni mkristo na kusema kuwa hajawahi kuwa muislamu.
Pistelli Naibu waziri wa mambo ya nje wa Italia, aliweka picha yake na Meriam kwenye ukurasa wake wa facebook akisema kuwa wanaelekea kutua mjini Roma.
Mume wa Meriam Daniel Wani, ni mkristo,ana asili ya Sudani kusini na ana uraia wa Marekani.
Mtoto wa Meriam, Maya alizaliwa gerezani mwezi May, muda mfupi baada ya kuhukumiwa kunyongwa hatua iliyosababisha ghadhabu dunia nzima.
Aliachwa huru mwezi Juni baada ya kuwepo kwa mashinikizo.

CHANZO: BBC SWAHILI

No comments: