Thursday 15 May 2014

Hali ya video queen wa "Ice Cream" ya Noorah ni mbaya

Aliekuwa video queen wa wimbo wa Noorah "Ice Cream" akimshirikisha Suma Lee uliowika takribani miaka 6 iliyopita, sasa ni muathirika mkubwa wa madawa ya kulevya.
Video Queen huyo, ambae anajulikana kwa jina la Doreen, sasa ni teja anaepatikana maeneo ya Sinza Makaburini, Inasemekana ana hali mbaya sana hasa tumbo likiwa limemvimba sana mithili ya mwanamke mwenye mimba huku miguu yake ikiwa imemvimba na hali yake kuwa dhoofu sana.
Hivyo kwa mtanzania yeyote atakayeguswa na hali ya dada huyo..basi ajitolee kumsaidia dada huyo.

CHANZO: Dj Fetty Blog

No comments: