Monday 19 May 2014

Diamond azidi itangaza Tanzania

Baada ya masiku kadhaa kutajwa kuwa ndiye msanii anayeongoza kwenye Top 20 za tuzo za KORA - 2014 kwa wiki ya 17, Msanii kutoka Tanzania Diamond Platnumz ameipa tena heshima kubwa bendera ya Tanzania kwa kuwa kwenye kipengele cha msanii bora wa Kimataifa (Best International Act). 
Hii ni hatua kubwa kwa Diamond baada ya siku chache tu nyuma alitangazwa kwenye tuzo za MTV Base (Mama Awards).
Diamond Platnumz kwenye kipengele hiki cha tuzo kubwa za Television ya burudani Marekani ya BET yupo kama Best International Act Africa na anawania tuzo hii na wasanii Davido kutoka Nigeria, Mafikizolo kutoka South Africa, Tiwa Savage kutoka Nigeria, Toofan na Sarkodie kutoka Ghana.
BET imetumia twitter kutoa hii taarifa kama kuthibitisha uchaguzi wa Diamond na kumpa hongera kama msanii peke kutoka Africa Mashariki...
 
Kila la kheri Diamond!... Endelea kuipeperusha bendera ya taifa letu!

1 comment:

Unknown said...

diamond he is the good artist and he support to win