Wednesday 9 April 2014

R.I.P Hassan baunsa

Taarifa zilizotufikia muda huu ni kuwa baunsa maarufu nchini, Braza Hassan amefariki dunia.

Hassan alikuwa baunsa hususan kwenye matamasha makubwa na kuwalinda wageni "wasanii" wanaokuja kwenye matamasha hayo...pia alipewa nafasi ya kuwa kiongozi wa ulinzi kwenye ziara ya Killi "Killi Tour".

Wasanii na baadhi ya wadau wa muziki wameoneshwa kuguswa na kifo cha baunsa huyo.

Bado hatujapata kujua chanzo cha kifo chake, ila mazishi yatafanyika siku ya kesho 10th April jijini DSM.

R.I.P Braza Hassan

No comments: