Wednesday 9 April 2014

7th April kumbukumbu ya mauaji ya Kimbari nchini Rwanda

April 7, 2014 taifa la Rwanda liliadhimisha kumbukumbu ya kutimiza miaka 20 tangu kutokea kwa mauaji ya Kimbari nchini humo, mwaka 1994... Mauaji ya Kimbari ya Rwanda yalikuwa mauaji ya kihalaiki mnamo mwaka wa 1994 ambapo Watutsi na baadhi ya watu wa kabila la Kihutu waliuliwa na serikali iliyosimamiwa na viongozi wa Kihutu... Katika kipindi cha takriban siku 100, kuanzia kuuliwa kwa Rais wa kipindi hicho, JuvĂ©nal Habyarimana na mwenzake wa Burundi Cyprien Ntaryamira mnamo tarehe 6 April hadi katikati mwa mwezi Julai 1994, angalau watu 800,000 waliuawa, au karibu asilimia 20 (20 %) ya idadi ya watu nchini Rwanda wakati huo…
Team Kibongobongo Blogspot tunatumia fursa hii kuwapa pole ma fans wetu wote raia wa Rwanda, ambao walipoteza ndugu, jamaa na marafiki zao kutokana na mauaji hayo…
Mwenyezi Mungu azidi kuwatia nguvu na aliepushe taifa lenu la Rwanda na mauaji hayo, kamwe yasitokee tena!…
Mungu ibariki Rwanda!... Mungu ibariki Afrika!...

No comments: