Sunday 2 March 2014

Mwanamke akatwa mguu na kumwagiwa tindikali huko Serengeti

"Ni zaidi ya miezi sita tangu nifanyiwe ukatili na mume wangu na mama mkwe. Nahangaika kuuguza mguu niliokatwa kwa panga kunyunyiziwa maji ya betri. sijui kama utapona. Kichanga nacho kinasumbua, jamani nimekosa nini mimi kwa Mungu".
Ni maneno kutoka kwa mama huyo aliyetambulika kwa jina la Anna Sabai (20) mkazi wa kitongoji cha Manyata kijiji cha Nyamakendo kata ya Mbalibali, Wilayani Serengeti mkoa wa Manyara. Ni maneno yenye kutia simanzi na yanayowezaamsha kilio.

CHANZO: BESTIZZO.COM

No comments: