Tuesday 4 March 2014

Drake ahamia kwa dada wa Rihanna

Drake na Samantha dada wa Rihanna
Mkali kutoka nchini Marekani akiwakilisha lile kundi la YMCMB lenye wakali kibao wakiwemo; Birdman, Bow Wow, Nick Minaj, Lil Twist, Wayne na Busta Rhymes, hapa namzungumzia Drake a.k.a Drizy aliyewahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwadadashosti Rihanna kwa kipindi cha nyuma. Kama umekuwa mfuatiliaji wa habari mbalimbali za mastaa utakuwa uliisikia hii story kuwa, wiki iliyopita kuna story zilienea kuwa wawili hao  bado wanapendana kwa maana walionekana wakibambiana "kukumbatiana" kwenye show ya Drake aliyoifanya juma lililopita huko Paris nchini Ufaransa. Wakali hao walipanda kwenye jukwaa na kuanza kuimba pamoja baadhi ya nyimbo walizowahi kufanya na wakaona bado haitoshi wakasanuka na kubambiana kwa hisia za kimapenzi
Drake na Rihanna wakiimba jukwaa moja
Bado story hizo hazijapoa... Drake Drizy aja na mupya ambayo wengi imewaweka kwenye maswali yasiyo na majibu ya haraka baada ya kuonekana Drake akiwa na dada yake Rihanna anayefahamika kwa jina la "Samantha". Wawili hao ambao kitambo waliwahi kuwa mashemeji wamezua balaa kwenye vyombo vya habari vya huko Marekani, ikiwa kila shabiki na mdau wa Drake anajiuliza je, Drake amehamia kwa dada yake Rihanna au bado anaipenda familia ya Rihanna ikiwa na maana kuwa ni kweli Drake ameamua kurudiana na Rihanna hivyo basi si tatizo Drake kuwa karibu na ndugu wa Rihanna.

No comments: